Kigali Mbali . . . Kigali Mbaaali Tukumbukane . . .

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Nashukuru nimeenda na kurudi salama.

Wacha picha ziongeee . . . . (at your own risk)

attachment.php

Wana ndege zaidi ya 10 ingawa ni Nchi ndogo, sijui tunazo ngapi. Huduma zao ni nzuri sana. Wachangamfu, wanapendeza . . . Gooo Goooo Kagame! Tofauti na Airline ya Watani wa jadi ambao Wanaongoza Africa lakini Hostess wao Mmmmh . . . naomba nisiseme.

Chakushangaza zaidi, kila binti unayekutana naye, kwa umbo na sura ni mzuri.

attachment.php

Nimetembea jamani . . . Kaskazini, Kusini, Mashariki, Magharibi . . . lakini kote sijaona . .

Nimeshindwa kujua ni wimbo gani unafaa kati ya hizi?

1. Kigali siendi tena . . . Kigali siendi tena . . . Kigali siendi tena, kuna dogo dogo nyingi . .

Ama?

2. Kigali Mbali . . . Kigali Mbaali . . Tukumbukane kwa barua . . .

attachment.php
 
Attachments

  • DSC00050.jpg
    DSC00050.jpg
    36.2 KB · Views: 2,482
  • DSC00055.jpg
    DSC00055.jpg
    46 KB · Views: 2,480
  • DSC00057.jpg
    DSC00057.jpg
    47.9 KB · Views: 2,471
Already missing Kigali . . .

Mji Mzuriiiiiiiiiiiiii . . . Msafiiiiiiiiiiiiiii . . . Very Organized! I wish . .
 
Wakati kaanchi kenyewe ni kama mkoa wa mbeya au iringa tuu!
Big up Kagame waache watz waendelee na porojo
 
Da,SM kweli wakaka weusi ni wazuri.watazame hao wanavyovutia.nami itabidi niende kigali,ila sasa ntaenda kumsalimia nani.........?
 
Wakati kaanchi kenyewe ni kama mkoa wa mbeya au iringa tuu!
Big up Kagame waache watz waendelee na porojo

Nitajisikia vema sana kumpigia kura kagame kuwa Rais wangu wa Afrika Mashariki . . .
 
Da,SM kweli wakaka weusi ni wazuri.watazame hao wanavyovutia.nami itabidi niende kigali,ila sasa ntaenda kumsalimia nani.........?

FL, penye nia pana njia. Nitaku-escort.

Mission: Kuangalia uwezekano wa kufungua ofisi ya JF.

Walau FL hutarudi.

Yaani sijui hawa wadada walifinyangwa au walizaliwa. Maana kila unayekutana naye ni balaa.

Kumbe na wewe unawaangalia wakaka.
 
kaka kama thread yako "imepungukiwa vitu flani" muhimu sana ili ikae vizuri jukwaa hili...navyo si vingine ila ni pamoja na picha za mabinti wa kitutsi na ki-nynkole wapatikanao kaskazini mashariki mwa rwanda.... hawa mabinti ni watamu zaidi ya kila kitamu ukijuacho chini ya jua...
i happen to date a rwandesse lady ...wazeiyahhh.. ni balaaaaa... sema hawakati mauno kitu gogo kaa dada zetu wa hapo juu kaskazini...ila kwa kuwala na kuwalamba jamani watamu
 
Kaka, huko umeenda mbali sana ingawa ni taarifa ya ziada.

Nasema hivi: Wanafaa kuwaangali, wanavutia macho. Hakika ni kama maua mazuri na yanapendeza.
 
.....Sorry sijaona cha ajabu hapo (urembo) labda hayo maendeleo ya rwanda.....!
 
Thanks Superman
Picha pia hufundisha, je tunaelewa somo lakini? Au tunajiburudisha tu na visura?

Mabel; wajibu wangu ilikuwa ni kuchokoza mada na dondoo zote nimeziweka. kazi kwet sote kutafuta somo ni nini. You can ask me any question. Kigali is the best so far. The gals are cool. Kigali is whaawww!
 
.....Sorry sijaona cha ajabu hapo (urembo) labda hayo maendeleo ya rwanda.....!

Well . . . mada inajieleza. Nime-Compare na Ku-Contrast. Tofauti ipo. Fungua macho Mkuu. Au tembea ujionee.
 
Mabel; wajibu wangu ilikuwa ni kuchokoza mada na dondoo zote nimeziweka. kazi kwet sote kutafuta somo ni nini. You can ask me any question. Kigali is the best so far. The gals are cool. Kigali is whaawww!

Ahsante Superman, ni nini contribution ya raia wa Rwanda(kama umeongea nao) katika maendelea ya taifa lao, ambapo taifa letu hili lenye wajinga wengi tunaweza kujifunza? Maana hii kila siku sijua JK, CCM ... taifa linakufa inabidi wananchi wenyewe tusimame, na wanachi wa Rwanda wanaweza kuwa mfano kwetu
 
Good question Mkuu.

Niliyoyaona na kuyasikia:

1. Kila mwananchi anatakiwa akubali na kukiri kuwa kulikuwa na Genocide na kuwa kulikataa hili ni kosa kisheria. Msingi wake ni kumfanya kila mtu akumbuke walikotoka na kuepuka kutokea madhara kama yale. Hilo pia linawafanya wawe na mshikamano wa kuijenga nchi yao.

2. Nilifika usiku, nilishangaa kuona usiku kulikuwa na White guys wanaranda randa mitaani na wazawa tena kwa furaha tu. Hii ni majira ya saa nne na kuendelea. lakini pia niliona police na JWTZ wa kule wakilinda mji/mitaa very strategically. Jamani Kigali ni shwari. Ingekuwa TZ nina uhakika mtu angepigwa roba.

3. Kuna mtu alisahau au kundondosha miwani ya bei mbaya Airport. Nimeshuhudia mdau akifanya jitihada ya kuifikisha security kuwa ameiokota. Ingekuwa bongo sijui ingekuwa vipi.

4. Watoto wa kike wako wengi katika nyanja ya Jeshini na Police na Security. Kazi ni kazi hakuna mchezo. Sasa na uzuri wao ni balaa. Askari wa kike aliniomba nifungue bag langu la laptop akague Airport, du, ilikuwa ni neema tu.

5. Barabara zinajengwa mjini na nyingi ni nzuri. Lami almost kila mahali na mji ni msafi. Taa za barabarani kila mahali. Traffic laws zinafwatwa sana. Hakuna msongamano wa mahari kama Nairobi, Kampala au DSM.

6. Nimeambiwa Kagame kila mwanzo wa mwaka anakuwa na makubaliano binafsi na appointee wake wote huku kila moja akiwa na targets zake binafsi. Mwishoni mwa mwaka kuna assesment. Kama performance yako ikiwa below standard anakutoa. Kwa hiyo watu wanafanya kazi.

7. Corruption at your own risk. Jamaa akisikia umetuhumiwa kwa rushwa, kwanza anakutoa katika cheo chako kisha unafanyiwa uchunguzi. Ukibainika ni majungu, unapewa promotion. Kama ni kweli, imekula kwako unaenda mahakamani.

8. Utawala wa sheria kama kawa, nilijaribu kuingia na za kichina china kama za bongo katika mambo fulani ili kupima kama jamaa wata-bend, lakili nilipiga hola.

9. majengo mapya ni mazuri na construction inaendelea.

10. Sehemy yao kama ya Kariakoo wanaiita "Commercialle", ina mitaa ya biashara mingi lakini well organized na misafi.

And many more. Watanzania tuna mengi ya kujifunza.
 
Na si hivyo East Africa Integration wanaipa kipau mbele.
 
Back
Top Bottom