Kifupi sisi hatuna culture ya kuwa na vision na kuweka goals, tunaelea tu.....

Tatizo letu haliko mahali popote isipokuwe kwenye uongozi; wakati tulipopata uhuru kulikuwa na matarajio. Matarajio kwamba na sisi "tunaweza".

The whole concept of "self determination" presumes some sort of readiness on the part of the people demanding it. Mnakumbuka ule wimbo wa enzi zile "juzi na jana siyo leo"? Tulipopata uhuru tulikuwa na matarajio kuwa we could do better than the colonialists and we could pave our own path into the virgin territory of own history.

Kwa hiyo, wazazi wetu walikuwa na jukumu kubwa la kutuongoza katika kuweza. Ni kwa sababu hiyo utaona wale vijana wa miaka ya sitini na sabini mwanzoni they were the most confident, most ambitions most daring and I'll propose most ready to lead. Mafundi wetu walioshirikiana na wachina kujenga Tazara, waliojenga barabara, kubuni miradi ya mashule na vyuo mbalimbali n.k vyote vilikuwa na lengo la kutupa hisia kuwa na sisi tunaweza.

Tulifikia mahali tukaweza kufuta ujinga zaidi ya asilimia 80; tuliweza kuja na kampeni ya nyumba bora ambapo vijiji vya ujamaa (ambavyo kuna watu wanaamini vimefeli) uliweza kukuta watu wanajenga nyumba za matofali ya kuchoma na serikali inawasaidia mabati ya kuezekea (nilioni mwenyewe kwa macho yangu kule Mkongo, Songea mwanzoni mwa 1980s); tulikuja na kampeni ya "mtu ni afya" na kampeni ya "chakula bora" (mnakumbuka "kuleni kuku, mayai, mboga samaki maziwa"..? Vyote hivyo vilikuwa vinatulenga kutupa uwezo wa kufanya.

Tukaanza kujenga viwanda vyetu vya nguo vikiwa na wachoraji na wabunifu wake; tukawa na UFI pale Ubungo, tukawa na viwanda vya viatu (Bora!), tukajaribu kujipa uwezo wa ndani sisi wenyewe; pole pole tukajenga betri, radio za nation na phillips (sauti safi, sauti kubwa, ndiyo yenyewe!) vyote hivi vilifanyika Tanzania. Nimesahau kukumbushia na baskeli zetu za "swala!).

Nyerere alitaka tuwe na uwezo sisi wenyewe kufanya mambo yaliyo ndani ya uwezo wetu. Hakutaka tubweteke kwa kutegemea vya nje. Sabuni (mbuni, malaika n.k), mafuta, n.k vingi tulikuwa tunafanya sisi wenyewe. Ukienda kwenye maduka yetu ya RTC utakuta bidhaa zetu. Wakenya wakija na Blue Band sisi tunaibuka na TanBond; maziwa ya mgando, chai, n.k (what else can I say!).

Lakini Nyerere alipoondoka tukaambiwa kuwa ameshindwa. Tukakubali kuwa ameshindwa. Tukakumbatia mtu mwenye uwezo. Mwinyi akaingia na kuja na kitu kinachoitwa ruhusa (maarufu kama Ruksa). Hakujali nini tunaweza kufanya sisi akasema Watanzana wamenyimwa anasa. Hivyo, akafungulia vya wageni kuja nchini na mara moja kuanza kuua vya kwetu; tukaanza kupoteza ule uwezo tuliotaka kujijengea; tukakubali kuwa hatuwezi.

Tukaanza kuagiza mitumba (wenyewe tukacheka kuvaa nguo za vitambaa vya mwatex na urafiki!), tukaanza kuingiza kwa nguvu Kimbo na wenzake, tukaanza kuona vya muhimu ni Televisheni n.k (wapo watu wanalalamika ati kwanini hatukuwa na TV wakati wa Nyerere!); elimu ya watu wazima ikatupwa pembeni, usalama wa taifa ukaharibiwa na matokeo yake Mkapa anapoingia hakurudi kwenye fikra za Mwalimu akaja na dhana yake ya wawekezaji.

Wakaanza kukaribisha wawekezaji kwenye kila kitu hata vile ambavyo sisi wenyewe tuliviweza (fikiria NBC na Bima) wakaanza kubinafsisha hata vyenye faida. Badala ya kutafuta mbinu ya kutengeneza vya kwetu na kutupa uwezo wakatuletea hadi polisi ili kulazimisha wageni watuendeshee Tanesco; Tukageuka na kuwa taifa la watu duni na tegemezi.

Akaja ndugu yetu Kikwete; akiwa ni mwathirika wa fikra tegemezi ameendelea kueneza itikadi ya uongo kuwa bila wageni hatuwezi kuendelea, bila wawekezaji hatuwezi kitu. Amepita huko na huko akiomba wenye akili kuja kutuendeshea uchumi wetu. Wawekezaji kwenye kila kitu na Watanzania wakibakia kuwa wadau tu. Matokeo yake Tanzania ya leo hata mkoloni anatushangaa! Tumefikaje hapa?

Ninachosema ni kuwa hatukuanza hivyo. Rudi tuwaulize wazee wetu, jamani kina Salim walikuwa wanavutia nje ya nje, tulikuwa na wasomi waliobobea miaka hiyo, tulikuwa na wataalamu wengi tu na wenye uwezo. Leo hii, tumebakia kuomba omba utaalamu. Leo hii ukienda kwenye maduka yetu utakuta hadi vitunguu toka nje! mazuria toka ng'ambo na kandambili na viatu toka nje!

Mtanzania hana fahari ya kitu chake tena; hizo ofisi za serikali ni ngapi zimenunua fanicha toka ndani? Ni ofisi ngapi zinatumia maua toka ndani, marumaru wanazotandaza katika nyumba zao zinatoka wapi? Uliza kuhusu mapazia?

Mtu mmoja alisema ufisadi ukikomeshwa tutaandamana; siwezi kushangaa. Kwa sababu kwa mara ya kwanza tunaweza kulazimishwa kujiangalia sisi wenyewe! Kuna siku ambayo tutaitwa kuita nguvu kutoka ndani yetu na kutafuta asili ya nguvu hiyo kutoka kwa watu wetu. Lakini yote inaanzia na uongozi kwanza.

Uongozi wenye fikra tegemezi, hauwezi kuongoza taifa kuelekea kujiamini.

Bob Marley put it better..

Old pirates, yes, they rob I;
Sold I to the merchant ships,
Minutes after they took I
From the bottomless pit.
But my hand was made strong
By the 'and of the Almighty.
We forward in this generation
Triumphantly.
Won't you help to sing
This songs of freedom
'Cause all I ever have:
Redemption songs;
Redemption songs.

Emancipate yourselves from mental slavery;
None but ourselves can free our minds.
Have no fear for atomic energy,
'Cause none of them can stop the time.

How long shall they kill our prophets,
While we stand aside and look? Ooh!
Some say it's just a part of it:
We've got to fullfil the book.

Won't you help to sing
This songs of freedom-
'Cause all I ever have:
Redemption songs;
Redemption songs;
Redemption songs.
---
/Guitar break/

None but ourselves can free our mind.

Wo! Have no fear for atomic energy,
'Cause none of them-a can-a stop-a the time.
How long shall they kill our prophets,
While we stand aside and look?
Yes, some say it's just a part of it:
We've got to fullfil the book.
Won't you have to sing
This songs of freedom? -
'Cause all I ever had:
Redemption songs -
All I ever had:
Redemption songs:
These songs of freedom,
Songs of freedom.
Mwanakijiji una maelezo mazuri marefu yanayolenga historia yetu kiuongozii kwa mapana.

Unasema Mwalimu alikuwa na dira ya kutufanya tujitegemee kwa yeye kusimamia hayo yote (maendeleo ya viwanda nk) uliyobainisha.

Wasiwasi wangu ni je kwa ni nn Mwalimu kama kiongozi pekee mkuu wa taifa hili inakuwaje aliyetawala kwa kipindi kirefu misingi yake ya uongozii iyumbee kwa muda mfupi namna hiyoo baada ya yeye tena kuwaachia wanachama wa chama chake (tukianzia na sera ya Ruksa na kuendeleaa)...

Bado taifa hili halijaweza kuwa na misingi imara na thabiti ya maendeleo ya watu wake..suala la amani, umoja wa kitaifa na ukarimu wa watanzania nacheleaa kukubali ni asili yaoo zaidi kuliko uhamasishaji wa kisiasa uliofanywa na viongozi.

Mataifa mengi yaliyosonga mbele kimaendeleo yanajivunia misingi imara iliyowekwaa na waasisi wake katika nyanja mbali mbali za maendeleo. Ndo maana Afrika haihitaji watu imara bali taasisi imara za kusimamiaa masilahi ya nchi hizoo..Umeonyesha wasiwasi wa Rwanda baada ya Kagame kuondoka madarakani kwa sababu unaamini katika uimara wa MTU na sio TAASISI...

Tanzania kama Taifa tunahitaji dira ya kuwa na taasisi imara (Serikali, Bunge, Mahakama) katika kusimamiaa maendeleo ya wananchi wake.Hiii yote yawezekana kwa kupata viongozi wenye DIRA ya kusimamia utekelezaji huo kuwepoo.
 
mbona maneno makali! haijalishi kama wote watarudi huko nyumbani; ulimwengu hauendi hivyo. Kama mnawahitaji kama maexpatriate hakikisheni mnatangaza ofa kama ma expatriates. Kama watalaalamu waliopo sasa nyumbani hawasikilizwi na kufuatwa unafikiri wakija wataalamu watanzania kutoka majuu ndio watasikilizwa? As a matter of fact mbona wapo wengi wamesharudi, wanasikilizwa?

Maendeleo ya Tanzania yasilaumiwe kukosekana kwa watalaamu ambao hawapo.

Mzee Mwanakijiji, heshima mbele mkuu, ni kweli kabisa kuwa tatizo kubwa tulilonalo linalopelekea tusiwe na maendeleo ni uongozi. Mimi nitatoa mfano wa nchi yetu Tanzania enzi za Mwalimu; katika jitihada za kujitosheleza na wataalam Mwalimu aliwapeleka wanafunzi wengi miaka ya sitini hadi thememanaini kusoma nje ya nchi na wengi wao walihitimu na unlike other African countries watanzania wengi walirudi nyumbani kufanya kazi na hawakuzamia huko majuu!! Wataalam wetu walikuwa na nafasi za kufanya kazi huko ughaibuni lakini wengi wao walirudi kwa sababu ya uongozi wa wakati huo; wakati ule viongozi walikuwa wanaonesha mfano kwa kutenda yale waliyoyahubili, kwa kifupi hawakuwa wanafiki na hiyo ndio ilikuwa chachu iliyowavutia wataalam wengi kurudu nyumbani kuijenga nchi yao!! Nitakwenda mbali zaidi na kusema kuwa hata ile vita ya Kagera dhidi ya Amin, tuliweza kumshinda kwasababu ya uongozi imara tuliokuwa nao ulioweza kuwaunganisha wananchi pamoja na viongozi wao kuwa kitu kimoja , leo hii Mungu apishe mbali sidhani kama nchi yetu ina uongozi wa kuleta umoja wa kitaifa unaoweza kuhimili janga kama lile!! kwakifupi nakubaliana na wewe kuwa the buck for the plight we are in stops with the LEADERSHIP period.
 
Back
Top Bottom