What up Mo...
Hili wazo lako sio zuri. Sio zuri kwa sababu ingawa lengo lako linaweza kuwa zuri, lakini itakuwia vigumu sana kuwaelewesha wananchi ya mikoa ambayo itajisikia na kujiona imekuwa neglected. Wazo hili linaweza kupandikiza chuki ambazo gharama yake itakuwa kubwa sana.
Hapo juu umetaja mikoa hiyo mitano lakini hujautaja mkoa wangu wa Shinyanga. Unadhani akina ngosha hawatajisikia kutelekezwa? Wakiamua kujitenga na kuanzisha taifa lao utawalaumu?
What it do homie....
Nimetoa mfano wa hiyo mikoa kama mwanzo lakini inaweza kufanywa analysis mikoa ipi mitano itakuwa na potential ya huge payoff kwenye investments za kilimo zenye kuajiri watu wengi, then forward linkage ili kuwepo na mahitaji ya nguvukazi ili vijana wapunguze kuja dar na kuhamia kwenye mikoa hiyo. Baada ya muda, unachagua mikoa mingine mitano mpaka nchi nzima inaendelea baada ya miaka kama 25.
Kwa mwendo wa sasa hivi ni tunapiga marktime, hela zinatumika ovyo lakini hakuna impact ya kureduce unemployment.
Naongea hivi sababu hawa vibaka wamemuattack mtu wangu wa karibu sana juzi na by grace of God he survived and he is ok.
Lazima ufumbuzi upatikane kuhusu vijana waliojaa Dar bila shughuli yoyote, otherwise tunakoenda itakuwa vita. Lazima watu wakae chini na long term strategy sio zimamoto, hili ni tatizo kubwa mno.