Kifungu gani cha sheria rais anapodanganya umma achukuliwe hatua? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifungu gani cha sheria rais anapodanganya umma achukuliwe hatua?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mkono, May 25, 2010.

 1. M

  Mkono JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sitaki kusahau issue ya muhimu eti kisa Liyumba kaenda jela miaka miwili,hukumu gani hii inayohamasisha wizi wa mali za umma yaani ni nani ataogopa kuiba zaidi ya bilioni 200 kwa kwenda jela miaka 2! Utani huu jamani.Tuachane na huo usanii ,siku zimepita tangu mkuu wa kaya alivyotoa hotuba kali dhidi ya wafanyakazi kuwataka kusitisha mgomo uliokuwa uanze pasipo kikomo.Baada ya hotuba ile ilithibitika rais alidanganya kwa kudai TUCTA walitakiwa kuhudhuria kikao saa 4 wao wakaonyesha walivyotakiwa kufika saa 8 mchana,hilo likapita na hadi leo sijaisikia ikulu ikiomba radhi au kutoa ufafanuzi.Likiwa linataka kusahaulika mara professor Bakari[kama ntakuwa sijakosea] akatukumbusha hesabu za primary .WAFANYAKAZI 350000 X Tsh 315000= ? Mkuu wa kaya ambaye wakati nikiwa mdogo nilikuwa nidhani anapaswa kuwa mtu mwenye akili kuliko wote yeye jibu lake lilikuwa 6bilioni.
  OMBI
  1.Naamini JF kuna watu wanahusika na malipo ya watumishi hivyo naomba mnisaidie kuonyesha serikali itatumia kiasi gani cha pesa iwapo itawalipa mshahara waliokuwa wakiutaka.
  2.Ndani ya JF kuna watu washeria nisaidieni kwenye sheria zetu ama katiba kama kuna kipengele chochote huyu mtu anayeonekana mzushi,mchonganishi anavyoweza kushughulikiwa.
   
Loading...