Kifungu cha 9(3) cha sheria ya madini (2010) ni msumari wa moto!

8625bb589e346f3ee77425beda8c1f8b.jpg

Wakati wabunge wa CCM wakipitisha sheria za madini
 
Unasema hao ma proffesa wskamatwe Kwa lipi ,wao walivyoona katika kamati yao ndo hayo na kama nikupitiwa kama binadamu yyt hiyo IPO au unataka kusema ripoti hiyo imepikwa?
Wameupotosha umma kwa kuzusha mambo ambayo hayapo na kulitia hasara taifa kwanza kuwafadhili, pili mgogoro wa makinikia kutugharimu
 
Huyu aliyeleta hii posti eti naye ni mTZ???

Tuache ujuaji mwingi, ilimradi tu na wewe uonekane umeposti au una uelewa wa sheria.

Katika wizi mwingi unaotendeka, umeona hilo ndilo la maana saana??? Hata kama MAKOSA hayo yamefanywa na baadhi ya waTZ kwa makusudi mazima, lazima wameshawishiwa kufanya hivyo, na hili jambo halikuanza leo; rejea BOGUS TREATIES ya kina Carl Peters etc.

Sasa, baada ya kuungana kuondoa huu ujinga, mnajitokeza kama mazombie na kuleta ujuaji!!! Sikuwahi kudhani kuwa kutafuta KIKI kunaweza mvua nguo mtu hadharani kwa kiwango hiki.

Pengine mkae chini na kuanza kutafakari kama KUWA MPINZANI maana yake ndio hio!!!

Kwani huyu mleta thread ana kosa gani, yeye amejaribu kuonyesha sehemu ya sheria ambayo inaweza kuwa tata, badala ya kumpongeza kwa kupoteza muda wake unamlaumu.

Kwa hiyo ulitaka akubali tu, huyu anaweza kuwa mzalendo zaidi yako wewe ambaye unataka kupiga kelele tu kama kasuku.

Jamani tuwe na moyo wa kukubali mawazo ya watu wengine, wote tunaitakia mema nchi yetu, tusifanye haya mambo kuwa ya kisiasa.

Vita hii inahitaji kupiganwa kiakili zaidi, sio kukurupuka, watatushinda.
Raisi wetu ameonyesha njia, tumuunge mkono na kumsaidia , binafsi ningeshauri Bungeni wabunge wote kwanza waondoe tofauti na wachangie miswada yote ya mabadiriko ya sheria bila kuweka ushabiki wa kisiasa, hapo ndio watakuwa wameonyesha uzalendo wa kweli.
 
Ni vizuri kuungana kuondoa ujinga lakini sharti na sisi tulioungana tuwe na werevu japo kidogo.
Utawezaje kuondoa ujinga wakati ukiwa mjinga zaidi ya ujinga wenyewe!? Na sababu ya ujinga wetu hata wale waliotushika mkono tusianguke shimoni tulikataa kuwasikiliza na kuwafukuza, sasa huu 'muungano' wa sasa hauwezi kuleta matokeo yaleyale kama ya mwanzo!? Kumbuka hii sheria ni ya Tanzania sio ya ACACIA.
Nafikiri umeshasikia fununu za nani atakuwa mwenyekiti wa kujadili haya na 'mpiga bakora' keshasema kuwa hana kosa mpaka mahakama iprove hivyo.
Teh! Teh! Teh!
 
Mkuu sasa povu la nini kwa wapinzani wakati sheria hii ya madini ilipitishwa na maCCM wenzako. Mtoa mada katoa hoja kwamba kampuni mama ikishasajiliwa affiliations zake au subsidies hazihitaji usajili hivyo kamati ineingia mkenge kulaumu Acacia wakati sheria imeelekeza hivo

Sasa kwanni usije na tafsiri nyingine ya kifungu hiki zaidi unaanza kusema wamehongwa sijui wasaliti sijui mpinzani yaani unaacha kulaumu maccm wenzako waliosaini hii sheria unakuja kulaumu wapinzani kwa kuhoji kipengele kimoja tu cha sheria za maccm???

Kazi kweli tunayo kma ndo maoni ya watanzania wote yapo kma yako
Hongera kwa kumpa darasa la bure
 
Mkuu wengine tusio na utaalamu wa sheria mnatuacha njiapanda..... ina maana unaweza pewa leseni ya madini kma hujasajiliwa popote hapa Tanzania??? Embu tusaidie hapa
Leseni wanazo nne za BRELLA. Tatu ni za migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara na ya nne ni ya African Barrick Gold Ltd.

Hoja ni brand name yao ya Acacia nayo isajiliwe? Sheria ya madini (2010) kifungu cha 9(3) inasema hakuna uhaja huo
 
Kwani huyu mleta thread ana kosa gani, yeye amejaribu kuonyesha sehemu ya sheria ambayo inaweza kuwa tata, badala ya kumpongeza kwa kupoteza muda wake unamlaumu.

Kwa hiyo ulitaka akubali tu, huyu anaweza kuwa mzalendo zaidi yako wewe ambaye unataka kupiga kelele tu kama kasuku.

Jamani tuwe na moyo wa kukubali mawazo ya watu wengine, wote tunaitakia mema nchi yetu, tusifanye haya mambo kuwa ya kisiasa.

Vita hii inahitaji kupiganwa kiakili zaidi, sio kukurupuka, watatushinda.
Raisi wetu ameonyesha njia, tumuunge mkono na kumsaidia , binafsi ningeshauri Bungeni wabunge wote kwanza waondoe tofauti na wachangie miswada yote ya mabdiriko ya sheria bila kuweka ushabiki, hapo ndio watakuwa wameonyesha uzalendo wa kweli.
Ndiyo shida kubwa tuliyonayo. Kushabikia kudhulumiwa. Hawa Acacia watatupiga hela ya kuzika mipango mingi iliyomo kwenye bajeti bado watakatufikisha hapo watadai wao ni wazalendo na sisi wasaliti
 
Labda tujiulize hivi kwanini kamati ya pili haikujiridhisha na kifungu cha 9(3) cha sheria ya madini ya mwaka 2010?
Ushatoa mchanganuo wa vifungu ambavyo ACACIA watawajibika navyo...

Sasa wewe kama Mtanzania, raia wa hapa TZ, twaomba mchanganuo kisheria utakaowezesha nchi ipate haki yake, uje na vipengele kama hivyo hivyo ili tuwakabe koo, na twajuwa utaweza maana umekokotoa vizuri kwa nguvu zote kuhusu ACACIA.
Hii ni kama kweli waipenda nchi yako...kama msemo wa hayati JFK wa marekani alivyosema tafadhali...Tunasubiri..
 
Leseni wanazo nne za BRELLA. Tatu ni za migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara na ya nne ni ya African Barrick Gold Ltd.

Hoja ni brand name yao ya Acacia nayo isajiliwe? Sheria ya madini (2010) kifungu cha 9(3) inasema hakuna uhaja huo

Umemaliza mijitu ya CCM ilitaka kunitoa roho
 
Unasema hao ma proffesa wskamatwe Kwa lipi ,wao walivyoona katika kamati yao ndo hayo na kama nikupitiwa kama binadamu yyt hiyo IPO au unataka kusema ripoti hiyo imepikwa?
Ndiyo. Mengi ya mambo yao wamekopi na kubandika toka kamati za miaka ya nyuma.
 
Huyu aliyeleta hii posti eti naye ni mTZ???

Tuache ujuaji mwingi, ilimradi tu na wewe uonekane umeposti au una uelewa wa sheria.

Katika wizi mwingi unaotendeka, umeona hilo ndilo la maana saana??? Hata kama MAKOSA hayo yamefanywa na baadhi ya waTZ kwa makusudi mazima, lazima wameshawishiwa kufanya hivyo, na hili jambo halikuanza leo; rejea BOGUS TREATIES ya kina Carl Peters etc.

Sasa, baada ya kuungana kuondoa huu ujinga, mnajitokeza kama mazombie na kuleta ujuaji!!! Sikuwahi kudhani kuwa kutafuta KIKI kunaweza mvua nguo mtu hadharani kwa kiwango hiki.

Pengine mkae chini na kuanza kutafakari kama KUWA MPINZANI maana yake ndio hio!!!
Acha kuandika Ujinga....wakati wale wagonga Meza wenu kule mjengoni wanapitisha Sheria yakufilisihi NCH ulikuwa wapi
 
Hapana mkuu usichoke tuelimishane,Je ni nani parent company kati ya Accasia na Barick gold mine company?
Kwa sababu inaonekana kwenye kifungu tajwa, kama parent company imeishasajiriwa,hakuna haja
ya kusajiri kampuni mtoto itakayozaliwa chini yake,sasa kwa hapa mbona aliyesajiliwa(barick)
ni mtoto na asiye na usajiri(Accasia) ni baba? hapo iko vipi?
 
Labda tujiulize hivi kwanini kamati ya pili haikujiridhisha na kifungu cha 9(3) cha sheria ya madini ya mwaka 2010?

Kifungu tajwa kinamwondelea Mchimbaji wa madini aliyesajiliwa uhaja wa kusajili tena kampuni tanzu katika kufanya kazi za uchimbaji, usafirishaji wa madini.

Kwa lugha rafiki, baada ya African Barrick Gold Ltd kusajiliwa kuwa ni mmiliki wa North Mara Gold mine Ltd, Bulyanhulu Gold mine Ltd na Pangea Minerals Ltd ambapo migodi yote imesajiliwa hawakuwa na uhaja tena wa kusajili kampuni tanzu yake ya Acacia.

Sasa sijui walimeza maharagwe ya wapi hii kamati ya pili ya Makinikia kudai Acacia ilipaswa isajiliwe wakati sheria ya madini (2010), kifungu na. 9(3) kinawazuia wasisajili tena kampuni tanzu.

View attachment 523736View attachment 523737
Lakini mkuu hii ni sheria ya madini ya 2010. ACACIA hawakuanza shughuli zao 1998 kweli? Je sheria za madini za huko nyuma zilisema nini kuhusu hili?
 
Back
Top Bottom