Kifungo hatari sana katika maisha

Dec 5, 2019
62
99
Ni kheri ufungwe Gerezani kuliko kufungwa akili ya kujitambua.

Ukiwa Gerezani utakula, ndugu, rafiki na jamaa watakutembelea na kukutia moyo, siku moja utakuwa huru hata kwa msamaha wa Rais.

Lakini ukifungwa akili ya kujitambua mabaya yote kwako huwa mema, na mema yote kwako huwa mabaya.

Ukifungwa akili ya kujitambua kamwe hautokuwa mtu wa shukrani hata utendewe mazuri kiasi kwa kiwango cha standard gauge.

Ukifungwa akili ya kujitambua ubongo wako utatawaliwa na chuki, wivu wa kutokata maendeleo kwa wenzio, maovu na mabaya nyakati zote.

Ukifungwa akili ya kujitambua unaweza kulipiwa mahali na mkeo alafu unajimwambafai umeoa kumbe umeolewa maana umelipiwa mahali na mkeo.

Ukifungwa akili ya kujitambua unaweza kutangaza unamiliki hoteli ya kifahari nyota 5 kumbe hata kodi ya kupanga unalipiwa na mke wako.

Ukifungwa akili ya kujitambua unaweza kumtongoza mwanamke na kujimwambafai kuwa wewe ni doctor, Eng, Prof. kumbe ni form four failure.

Ukifungwa akili ya kujitambua unaweza kushuhudia uongo, ukajitakia mabaya ya milele ili upate tu msaada wa siku moja.

Ukifungwa akili ya kujitambua utajiona umri wako bado mdogo wakati una miaka 35+

Ukifungwa akili ya kujitambua utakuwa mtu wa kusaidiwa tu bila wewe kusaidia wengine, utakuwa mtu wa kujiruhumia mwenyewe bila kuhurumia aliye jirani yako.

Ukifungwa akili ya kujitambua muda mwingi utakuwa mtu wa kuwaza ngono hata kama huna hata Tsh. 500/= mfukoni.

Ukifungwa akili ya kujitambua utakuwa mtu wa kuwachukia walioshindwa kukusaidia wakati upo na shida ilihali hiyo shida ilikuwa lazima uitatue mwenyewe.

Ukifungwa akili ya kujitambua utakuwa mtu wa kutengeneza matatizo na kuwalaumu wengine.

Ukifungwa akili ya kujitambua utakuwa mtu wa lala na kukaa nyumbani bila kazi au kibarua chochote huku ukitegemea pesa za msaada ndiyo zikulishe.

Ukifungwa akili ya kujitambua unaweza kuikataa mimba yako halali na kutelekeza familia kwa kigezo cha maisha kuwa magumu.

Ukifungwa akili ya kujitambua hata ukutane na mwanamke sahihi kwa 96% akikosea moja tu lenye asilimia 1% utamuona ni mbaya na kuzifuta 96% za mazuri yake.

Ukifungwa akili ya kujitambua hata kila siku uhudhurie kanisani na misikitini unakuwa mtu ambaye hauna hata punge ya hofu ya Mungu zaidi ya maigizo.

Ukifungwa akili ya kujitambua utakuwa ni mtu wa kutengeneza matukio ya uongo bila haya wala hofu yeyote ili uweze kusaidiwa.

Ukifungwa akili ya kujitambua unakuwa mtu wa kutamani uwe tajiri wakati umekaa tu nyumbani bila shughuli yeyote inayokuingizia kipato.

Ukifungwa akili ya kujitambua unakuwa mtu muongo, usiyekuwa na uaminifu kabsa kwa ndugu, rafiki na jamaa hata mfereji unaokuletea maji ya unauziba kwa mikono yako mwenyewe.

Ukifungwa akili ya kujitambua unakuwa mtu kutoa siri zako za ndani na kuzipeleka kwenye mitandao ya kijamii kuomba msaada wakati ulikuwa na nafasi na mwenza wako mkaongea na kuyamaliza.

Ukifungwa akili ya kujitambua unaweza kuwa mtu wa kumili simu janja nzuri ya bei kubwa, flat screen ya bei kubwa, laptop ya bei kubwa alafu unahangaika na kulalamika huna mtaji wa kufungua genge la matunda au banda la chips.

Ukifungwa akili ya kujitambua una kuwa mtu wa madeni kila kona hata maisha yako yanakuwa ya bahati nasibu.

Ukifungwa akili ya kujitambua mtu mwenye miaka 30 unafanya mambo ya mtu mwenye miaka 15.

Ukifungwa akili ya kujitambua daima huwezi kuwa mtu wa maendeleo, mafanikio chanya, hasira na maisha, mchumia juani, mwenye shukrani, future nzuri, kutambua wajibu wako na majukumu yako.

KUFUNGWA AKILI YA KUJITAMBUA NI ZAIDI YA UTUMWA.

KWENYE JAMII ZETU KUNA WATU WA AINA HII

NAOMBA MCHANGO WAKO WA MAWAZO WAFANYE NINI ILI WAONDOKANE NA HII HALI YA KUFUNGWA KWA AKILI YA KUJITAMBUA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kujikimbushia historia na mambo yanyuma yaliyo kuumiza na kupita na yakukufanya kushindwa kwenda mbele

PIA HUKU NI KUFUNGWA KWA AKILI
 
Yakobo 1:5-8 Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
5 Lakini kama mtu ye yote kati yenu akipungukiwa na hekima, basi na amwombe Mungu, ambaye huwapa watu wote kwa ukarimu pasipo kulaumu, naye atapewa. 6 Lakini aombe kwa imani pasipo shaka yo yote; maana mwenye mashaka ni kama wimbi la bahari ambalo husu kumwa na upepo, likitupwa huku na huku. 7 Mtu kama huyo asidhani atapata kitu cho chote kutoka kwa Bwana; 8 kwa maana yeye ni mtu mwenye nia mbili asiyekuwa na msimamo katika jambo lo lote.
 
1 Wafalme 3:7-14

7Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, umeniweka mimi mtumishi wako kuwa mfalme mahali pa baba yangu Daudi, ijapokuwa ningali mtoto mdogo na sijui namna ya kutekeleza wajibu huu. 8Na hapa umeniweka kati ya watu wako ambao umewachagua; nao ni wengi hata hawawezi kuhesabika kwa wingi wao. 9Kwa hiyo, nakuomba unipe mimi mtumishi wako moyo wa kusikia ili kuamua watu wako, niweze kutambua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuhukumu watu wako walio wengi hivi?”
10Ombi hili la Solomoni lilimfurahisha Mwenyezi-Mungu, 11naye akamwambia, “Kwa kuwa umetoa ombi hili, na hukujiombea maisha marefu au mali, na wala hukuomba adui zako waangamizwe, bali umejiombea utambuzi wa kutoa hukumu au kutenda haki 12basi, sasa nakutimizia kama ulivyoomba. Tazama, nakupa hekima na akili kiasi ambacho hapana mtu mwingine aliyepata kuwa nacho kabla yako, na wala hatatokea mwingine kama wewe baada yako. 13Pia, nitakupa yale ambayo hukuomba: Nitakupa utajiri na heshima zaidi ya mfalme mwingine yeyote wa nyakati zako. 14Tena kama ukifuata njia na maagizo yangu na kushika amri zangu kama alivyofanya baba yako Daudi, basi, nitakupa maisha marefu.”
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom