Kifungo cha Charles Taylor kinatoa fundisho gani kwa watawala wa Kiafrika?

Tuyuku

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
3,292
1,919
Bwana vita Charles Taylor, rais wa zamani wa Liberia anaingia ndani ya nondo za magereza kwa miaka 50. Amepatikana na hatia ya kufadhili vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Sierra Leone.

Kuna somo ambalo watawala wa Kiafrika wanapaswa kujifunza. Kila kitu kina mwisho. Enzi na utukufu wa viongozi ambao hufikia hatua na kujiona wao ni miungu watu huwa una mwisho wake.

Watawala wanaojifanya wapo juu ya sheria. Watawala wanaotumia vyombo vya dola kuwauwa raia ovyo wanapodai haki zao. Watawala wanaotorosha mabilioni ya fedha kwenye mabenki ya nje na kujitajirisha wao na familia zao. Hakuna mbabe wa kudumu duniani.

Napenda kuwakumbusha watawala wa Kiafrika kuwa wakati wao ukifika watakwenda tu na maji. Wasijisahau wakadhani wana uwezo wa kimungu wa kufanya kila jambo na wasifanywe kitu.

Kila kitu kina mwisho. Utawala wao una mwisho. Wasijisahau wakadhani wamepata kila kitu.

Wakati akitawala, nani aliwahi kufikiri ipo siku bwana vita CT atakwenda jela? Kama hilo limewezekana, mengi mengine yanawezekana.

Kazi kwenu.
 
You can run but you cannot hide. I pity Bashir the long arm of icc will catch up sooner or later.
 
Na Ghadaf alipaswa ashtakiwe hivi siyo kumuua..
Taylor anatia huruma ukimuangalia
 
Back
Top Bottom