Kifuatacho baada ya Dkt. Magufuli...

Ngaliwe

Senior Member
Dec 30, 2015
161
364
KUONDOKA mapema kwa Rais John Magufuli, kumeiacha Tanzania katika njia panda, wananchi wakijiuliza ni nini kitafuata baada ya hapa.

Nini hatma ya Tanzania baada ya Magufuli? Ndilo swali kubwa kwa sasa kwa watanzania na bila shaka Afrika na dunia yote. Baada ya kazi kubwa ya ujasiri mkubwa aliyoifanya Rais Magufuli kwa takribani mika sita na kubadilisha kabisa Tanzania, nini kitafuata baada ya kundoka kwake ni agenda muhimu kwa mustakabali wa taifa.

Mamilioni ya wananchi waliotokwa na machozi na wengine kutopata usingizi siku walipotangaziwa habari cha kifo chake, waliojipanga barabara na kujaa viwajani toka Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Mwanza na baadaye njia nzima toka Mwanza mpaka Chato, vilio, kuzimia na kila aina ya masikito makubwa yalikuwa yanatuma ujumbe mmoja tu, Rais Magufuli alikuwa kweli rais wa wanyonge, aliwakuwa rais aliyegusa maisha yao kwa karibu sana.

Pamoja na kumlilia kipenzi chao, kilio na majonzi yale yalibeba ujumbe mmoja muhimu na mahsusi, nini itakuwa hatma yao, nini hatma ya Tanzania. Na swali hili linajengwa siyo kwa kwa wasiwasi wa kuingiakatika machafuko, hapana, walau katika hilo Tanzania tumevuka mbali.

Msingi wa swali hilo ulikuwa katika msingi wa ustawi wa watu, hasa waanchi wanyonge ambao miaka sita ya Rais Magufuli wameshuhudia ikigusa maisha yao, katika afya, elimu, usafiri, biashara na karibu katika kila jambo kwenye maisha yao.

Rais alikuwa ni kama baba wa kila familia moja moja, kuondoka kwake siyo tu wanaona hawana rais, lakini kwa jinsi alivyogusa maisha yao kwa kuondoa dhuluma, kunyayaswa na wenye pesa, wanajikuta njiapanda, baada ya baba kuondoka nani tena atakuwa mlinzi wa maslahi yao kama familia, kama taifa, nani atawalinda dhidi ya uhuni na uharamia wa wenye pesa kwenye viwanja vyao, mashamba yao, na ukandamizwaji mwingine wa haki zao.

Haya yote ni kazi anayopaswa kujitwishwa Rais Samia Suluhu Hassan, kama alivyosema mweyewe jiji Dodoma kwamba amekuwa mwanafunzi makini wa Rais Magufuli na kwamba sasa amefunzu, na akatuhakikishia watanzania kwamba nchi iko salama chini yake.

Kwa hakika Tanzania chini ya Rais Samia iko salama, anao uwezo wa kuyafanya aliyokuwa akiyafanya Rais Magufuli, kwa sababu amekuwa sehemu muhimu sana ya mabadiliko haya tuliyoyashuhudia Tanzania katika uongozi wao wa awamu ya tano.

Rais Samia si mgeni katika mipango na miradi yote ambayo imetekelezwa na inayoendelea kutekelezwa nchini, kwa hili ni muhimu tumuamini na tumuunge mkono katika kuhakikisha kuwa Tanzania mpya inajengwa na kukamilika kwa umakini mkubwa.

Aidha ni muhimu sana, Rais Samia akiwa na wasaidizi wa mfanano wa Magufuli ili wamsaidie kwenda haraka na kasi ambayo walikuwa wamefikia yeye na Hayati Magufuli. Ameanza vyema kwa uteuzi wa Makamu wa Rais, kwa sababu ni kweli kwamba wapo watu wachache ambao hawakuwa wanafurahishwa na anachokifanya Rais Magufuli, na hivyo wasingependa mfumo na aina yake ya uongozi uendelee.

pp.jpg

Hawa ni wale wanaliokuwa wanatumia uongozi kwa maslahi yao binafsi, hawakujali sana kama wananchi wanapata umeme vijiini, wana zahanati na vituo vya afya, kuna miundombinu imara ya kutosha, wananchi wanafanya kazi kwa uhuru katika nchi yao, na wala haikuwasumbua wafanyabiashara wakubwa walipokuwa wakikwepa kodi, kwa sababu wao walikuwa wanafaidika na hali hiyo.

Kifo cha Rais Magufuli kimewapa fursa watu hawa, si wengi lakini wana nguvu, haraka sana hata kabla hatujamzika shujaa wetu, wameshaanza kufuta nyazo zake. Wameanza vita mitandaoni kushambulia na kuwachafua watu wenye mitazamo inayofanana na Hayati Magufuli, kwa hofu kwamba kuendelea kwa uwepo wao kutaendelea kuwanyima fursa ya kupora rasilimali za nchi hii kama alivyowanyima nafasi hiyo Rais Magufuli.

Wahanga wa kwanza katika vita hii ni wale walioaminiwa kwa dhati na Hayati Magufuli, ambao kwa uadilifu, uchapa kazi wao, wameanza kushambuliwa ili wachafuke waonekane hawafai mbele ya jamii ili kuwapa nafasi waliozoea vya kunyonga, waje kupora tena rasilimali zetu.

Uwezo wa watu hawa kubeba maono ya Rais ya Magufuli na kuyatafsiri kwa vitendo ndicho kinachowaogopesha wale wanaotamani wafute historia na ushawishi wa Magufuli katika serikali ya Rais Samia, ndiyo maana wameanza mapema kurusha mawe na kuwachafua wasaidizi wake muhimu kwa malengo ya kutimiza dhamira yao hii ovu.

Ni vyema tumuombee Rais Samia asimame imara katika kuamua dira na mwelekeo wa Tanzania chini ya uongozi wake. Tunaambiwa tayari ziko juhudi za kutaka kuweka watu ambao kazi yao ya kwanza itakuwa ni kuanza kufuta kila aina ya urithi wa Magufuli na kuturudisha tuliko toka, kama kikundi hiki cha watu wenye nguvu wakifanikiwa kupenyeza ‘watu wao’ kwa sababu zozote zile, itakuwa ni msiba mwingine kwa Taifa.

Matumaini yetu ni kwamba Rais atasimama imara kuepuka ushawishi mbaya wa aina hii kwa ajili ya maslahi ya chama, Taifa na mamilioni ya watanzania ambao maisha yao yaliguswa na kipenzi chao, Rais Hayati John Magufuli.

ASANTE SANA JOHN
 
Ume filter image ukampachika mwendazake ili ionekane walikuwa wote hapo kumbe ni edited.
 
YEHODAYA

Huyu ni mshirika au ni ile ID yako ya msaada uliyokuwa umeihifadhi kwa shughuli maalum wakati muafaka?

Kwa hakika umekuja kwa kasi mpya, nguvu mpya na ari kweri kweri.

Hiiiiii.
Yehodaya hawezi pangilia namna hii art tofauti...yehodaya anachamba na dharau juu.
 
Mmembiwa na nani kuwa wanawekwa watu wa kufuta ya Magufuli?

Kila Rais anakuwa na mipango yake, hata aliyepita alikuwa na yake.

Mbona wakati uliopita hakukuwa na washauri kama sasa mitandaoni.

Tanzania yetu...
 
Hii ripoti ya CAG imetuonyesha, kutufundisha na kutuonya kuwa tunahitaji taasisi imara na siyo mtu mmoja mwizi na fisadi anaejidai na kujinadi imara.

Kwa ushahidi wa ripoti hii ya CAG Magufuli alikuwa ni kiongozi populist ambae alikuwa ni mwizi, fisadi na mzembe wa mali za uma aliekuwa anajificha kwenye chaka la siasa za propaganda ili kuaminika.
 
KUONDOKA mapema kwa Rais John Magufuli, kumeiacha Tanzania katika njia panda, wananchi wakijiuliza ni nini kitafuata baada ya hapa.
Wewe bado upo njia panda? Mbona watu wapo na Mama na tayari madduddu ya Magufuli yanaonekana wazi?

KUONDOKA mapema kwa Rais John Magufuli, kumeiacha Tanzania katika njia panda, wananchi wakijiuliza ni nini kitafuata baada ya hapa.

Nini hatma ya Tanzania baada ya Magufuli? Ndilo swali kubwa kwa sasa kwa watanzania na bila shaka Afrika na dunia yote. Baada ya kazi kubwa ya ujasiri mkubwa aliyoifanya Rais Magufuli kwa takribani mika sita na kubadilisha kabisa Tanzania, nini kitafuata baada ya kundoka kwake ni agenda muhimu kwa mustakabali wa taifa.

Mamilioni ya wananchi waliotokwa na machozi na wengine kutopata usingizi siku walipotangaziwa habari cha kifo chake, waliojipanga barabara na kujaa viwajani toka Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Mwanza na baadaye njia nzima toka Mwanza mpaka Chato, vilio, kuzimia na kila aina ya masikito makubwa yalikuwa yanatuma ujumbe mmoja tu, Rais Magufuli alikuwa kweli rais wa wanyonge, aliwakuwa rais aliyegusa maisha yao kwa karibu sana.

Pamoja na kumlilia kipenzi chao, kilio na majonzi yale yalibeba ujumbe mmoja muhimu na mahsusi, nini itakuwa hatma yao, nini hatma ya Tanzania. Na swali hili linajengwa siyo kwa kwa wasiwasi wa kuingiakatika machafuko, hapana, walau katika hilo Tanzania tumevuka mbali.

Msingi wa swali hilo ulikuwa katika msingi wa ustawi wa watu, hasa waanchi wanyonge ambao miaka sita ya Rais Magufuli wameshuhudia ikigusa maisha yao, katika afya, elimu, usafiri, biashara na karibu katika kila jambo kwenye maisha yao.

Rais alikuwa ni kama baba wa kila familia moja moja, kuondoka kwake siyo tu wanaona hawana rais, lakini kwa jinsi alivyogusa maisha yao kwa kuondoa dhuluma, kunyayaswa na wenye pesa, wanajikuta njiapanda, baada ya baba kuondoka nani tena atakuwa mlinzi wa maslahi yao kama familia, kama taifa, nani atawalinda dhidi ya uhuni na uharamia wa wenye pesa kwenye viwanja vyao, mashamba yao, na ukandamizwaji mwingine wa haki zao.

Haya yote ni kazi anayopaswa kujitwishwa Rais Samia Suluhu Hassan, kama alivyosema mweyewe jiji Dodoma kwamba amekuwa mwanafunzi makini wa Rais Magufuli na kwamba sasa amefunzu, na akatuhakikishia watanzania kwamba nchi iko salama chini yake.

Kwa hakika Tanzania chini ya Rais Samia iko salama, anao uwezo wa kuyafanya aliyokuwa akiyafanya Rais Magufuli, kwa sababu amekuwa sehemu muhimu sana ya mabadiliko haya tuliyoyashuhudia Tanzania katika uongozi wao wa awamu ya tano.

Rais Samia si mgeni katika mipango na miradi yote ambayo imetekelezwa na inayoendelea kutekelezwa nchini, kwa hili ni muhimu tumuamini na tumuunge mkono katika kuhakikisha kuwa Tanzania mpya inajengwa na kukamilika kwa umakini mkubwa.

Aidha ni muhimu sana, Rais Samia akiwa na wasaidizi wa mfanano wa Magufuli ili wamsaidie kwenda haraka na kasi ambayo walikuwa wamefikia yeye na Hayati Magufuli. Ameanza vyema kwa uteuzi wa Makamu wa Rais, kwa sababu ni kweli kwamba wapo watu wachache ambao hawakuwa wanafurahishwa na anachokifanya Rais Magufuli, na hivyo wasingependa mfumo na aina yake ya uongozi uendelee.
View attachment 1747420

Hawa ni wale wanaliokuwa wanatumia uongozi kwa maslahi yao binafsi, hawakujali sana kama wananchi wanapata umeme vijiini, wana zahanati na vituo vya afya, kuna miundombinu imara ya kutosha, wananchi wanafanya kazi kwa uhuru katika nchi yao, na wala haikuwasumbua wafanyabiashara wakubwa walipokuwa wakikwepa kodi, kwa sababu wao walikuwa wanafaidika na hali hiyo.

Kifo cha Rais Magufuli kimewapa fursa watu hawa, si wengi lakini wana nguvu, haraka sana hata kabla hatujamzika shujaa wetu, wameshaanza kufuta nyazo zake. Wameanza vita mitandaoni kushambulia na kuwachafua watu wenye mitazamo inayofanana na Hayati Magufuli, kwa hofu kwamba kuendelea kwa uwepo wao kutaendelea kuwanyima fursa ya kupora rasilimali za nchi hii kama alivyowanyima nafasi hiyo Rais Magufuli.

Wahanga wa kwanza katika vita hii ni wale walioaminiwa kwa dhati na Hayati Magufuli, ambao kwa uadilifu, uchapa kazi wao, wameanza kushambuliwa ili wachafuke waonekane hawafai mbele ya jamii ili kuwapa nafasi waliozoea vya kunyonga, waje kupora tena rasilimali zetu.

Uwezo wa watu hawa kubeba maono ya Rais ya Magufuli na kuyatafsiri kwa vitendo ndicho kinachowaogopesha wale wanaotamani wafute historia na ushawishi wa Magufuli katika serikali ya Rais Samia, ndiyo maana wameanza mapema kurusha mawe na kuwachafua wasaidizi wake muhimu kwa malengo ya kutimiza dhamira yao hii ovu.

Ni vyema tumuombee Rais Samia asimame imara katika kuamua dira na mwelekeo wa Tanzania chini ya uongozi wake. Tunaambiwa tayari ziko juhudi za kutaka kuweka watu ambao kazi yao ya kwanza itakuwa ni kuanza kufuta kila aina ya urithi wa Magufuli na kuturudisha tuliko toka, kama kikundi hiki cha watu wenye nguvu wakifanikiwa kupenyeza ‘watu wao’ kwa sababu zozote zile, itakuwa ni msiba mwingine kwa Taifa.

Matumaini yetu ni kwamba Rais atasimama imara kuepuka ushawishi mbaya wa aina hii kwa ajili ya maslahi ya chama, Taifa na mamilioni ya watanzania ambao maisha yao yaliguswa na kipenzi chao, Rais Hayati John Magufuli.

ASANTE SANA JOHN
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom