Kifua Kikuu - TB

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,113



TB au Kifua Kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza ambao husababishwa na viini viitavyo ‘tubercle bacilli’.
Wengi wetu tuna viini vya TB mapafuni mwetu lakini hii sikumaanisha kwamba tutauguza huu ugonjwa. TB hushika wale ambao wana ukosefu wa kinga mwilini unao sababishwa na kutokula chakula kizuri, matumizi ya madawa ya kulevya au wanaouguza magonjwa mengine.

TB ya mapafu ndio imeenea zaidi. Hata hivyo, viini vya TB vinaweza kusafirishwa kutoka mapafuni kupitia kwa damu hadi sehemu zingine za mwili na kusababisha hivyo viungo viathiriwe na TB.

Viini vya TB hupatikana kwa mate ya muuguzi. Wakati mgonjwa anakohoa, kupiga chafya au kutema mate kiholela, viini vya TB husambazwa kwa hewa. Mwenye afya akiipumuwa hewa hiyo anaambukizwa na mapafu yake inaanza kuwa na vijidonda.

Dalili za TB

  • Kikihozi kisichoisha
  • Uchovu na kuishiwa kwa nguvu mwilini
  • Kupoteza uzito
  • Kupoteza hamu ya kula
  • Kutokwa na jasho hata wakati kuna baridi
  • Maumivu ndani ya kifua
  • Kuishiwa na pumzi
  • Mate yaliyo na damu au kukohoa damu
Tiba ya TB
Kuna tembe tofauti zinazotumiwa kutibu TB. Dawa hizi hutumika kwa kipindi cha miezi sita au hata zaidi.

Dalili za TB zikingunduliwa mapema, sio lazima mgonjwa alazwe hospitalini.
Hata hivyo,ikiwa ugonjwa umezidi sana, mgonjwa wa TB atakuwa mdhaifu sana na itabidi alazwe hospitalini.

Chini ya Kanuni mpya za utibabu wa TB ulimwenguni, inapendekezwa, wagonjwa wa TB ya kawaida wanapaswa kulazwa hospitalini kwa miezi miwili pekee halafu miezi minne iliyobaki watibiwe wakiwa na jamii zao.

MDRTB ni neno linalotumika wakati viini vya TB vinashinda nguvu dawa moja au mbili zinazotumiwa kutibu TB. Shida kama hii hutokea ikiwa mgonjwa ametumia madawa kwa njia isiotakikana au alianza matibabu akakosa kumalizia ile miezi sita inayohitajika. Kawaida, inachukua miezi sita au zaidi kutibu TB kabisa. Hata hivyo, mgonjwa akianza matibabu, baada ya muda kidogo hujihisi yuko sawa. Ijapo atakatiza matibabu, kuna hatari kwamba viini vilivyo mwilini mwake hujiunda kipya na kujiongezea nguvu hivi kwamba madawa aliyokuwa akitumia hapo mbeleni hayawezi kumtibu tena. TB ya aina ya MDR wakati mwingi haitibiki na mtu ambaye anaugua aina hii ya MDR anaweza kuisambaza vile vile kama TB ya kawaida.

Matibabu ya mgonjwa aliye na MDRTB inagharimu mara ishirini zaidi ya yule aliye na TB ya kawaida. Matibabu ya mgonjwa wa MDRTB yanaweza kuchukua muda wa miezi kumi na nane.

TB ni mojawapo ya magonjwa ambayo huathiri watu walio na virusi vya Ukimwi. Kama una Ukimwi, jihadhari sana usishikwe na TB. Iwapo unajishuku una TB, hakikisha umepimwa na kutibiwa vilivyo.
 
Back
Top Bottom