achengula
JF-Expert Member
- Jul 30, 2009
- 369
- 62
Ugonjwa wa kifua kikuu cha ngombe ni ugonjwa hatari sana wenye madhara makubwa kiafya kwa ngombe, mwanadamu na hata katika biashara ya kimataifa. Ni ugonjwa unaosababishwa vimelea vya bakteria wanaojulikana kwa jina la kitaalamu kama Mycobacterium bovis. Kimsingi ni ugonjwa wa mfumo wa upuuaji unaochukua muda mrefu (kuanzia wiki chache hadi maisha yote) kujijenga ndani ya mwili tangu maambukizi hadi kuanza kujitokeza dalili za ugonjwa na kuanza kuambukiza wanyama wengine. TB yaweza kuwapata wanyama wengi lakini mara nyingi ni ngombe na nyati. Mwanadamu hupata ugonjwa wa kifua kikuu kutoka kwa ngombe au mazao yake, lakini pia mwanadamu anauwezo wa kumuambukiza ngombe. Maambukizi yameonekana pia kwa kondoo, mbuzi, farasi, nguruwe, paa, mbwa na paka. Kwa maelezo zaidi (dalili, utambuzi, tiba na uzuiaji) juu ya ugonjwa huu soma hapa SEKTA YA MIFUGO TANZANIA