X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,344
- 14,117
katika haya maisha hakuna mtu asiejua maumivu ya kumpoteza mtu ambae unamuhitaji iwe baba, mama, dada, mke pengine ata watoto. ndugu zetu wanatutoka tunalia mwisho tunanyamaza japo kumbukumbu za upendo tuliokuwa tunaupata kutoka kwao bado zina baki katika fikra zetu.
mimi wewe na yule wote tutakufa ispokuwa tu vifo vyetu vitatofautiana kama vilivyotofautiana vya walio tutangulia, idadi ya mambo yanayo tusababishia vifo siku izi imeongezeka tofauti na enzi za mababu zetu. vyombo vya usafiri, magonjwa, ajari mbali mbali ikiwemo zile zinazosababisha na uzembe wa mafundi {magorofa kuporomoka}, machafuko ya hali ya hewa na sumu vyote hivyo siku hizi vinamsaidia kazi malaika mtoa ROHO. yani siku hizi IZLAIL {malaika mtoa roho} apati shida ata kidogo na mbaya zaidi vifo asilimia 75 vyote vinavyotokea sisi wenyewe ndio chanzo.
utakuta abiria wanamlazimisha dereva aendeshe gari kwa mwendo wa kasi eti wanataka kuwahi, na muda mwingine abiria wanaona mwendo wa dereva anaoenda nao si mzuri ila hawamwambii kitu mwisho inatokea ajari mbaya wanakufa abilia wote. tunalia, tunasononeka tunapoteza watu muhimu, muhimili wa taifa unatetereka lakini atuwafundishi madereva wetu umuhimu wa safari salama. {tunajitakia}
tutakaa na kulaumu pengine dhambi zimetuzidi sana, ila si kila angamizo ni la dhambi mengine ni ya kujitakia na yana epukika kabisa, si inajurikana ukiumwa unywe dawa lakini kuna watu wanaweza wakaathiriwa na maradhi hadi umauti unawakuta hawata thubutu kutumia dawa. mwengine ameathirika na magonjwa makubwa kama UKIMWI pengine ameanza matibabu lakini kutokana na UROFA na UPUMBAVU eti unakuta mtu huyo huyo tena labda amesoma lakini anakatisha dawa mwisho umauti unamkuta hali ya kuwa angetumia dawa kidogo angeweza kuzisogeza mbele siku za kuishi.{tunajitakia}
mimi nadhani muda ufike sasa tusimrahisishie IZRAIL {malaika mtoa roho} kazi, tusimrahisishie kazi kabisa yani tufanye vitu kwa mpangilio ulio mzuri tusiendeshe vyombo vya usafiri kwa kasi. tuache kutumia madawa yenye kemikali tukumbuke kuwa matunda na mimea ni dawa...tule vyakula bora, tule matunda kwa wingi, tuache ZINAA. ifike kipindi huyu malaika akija apate tabu kidogo ya kuzitoa roho zetu. wazee wetu waliishi muda mrefu kwa sababu hawakutumia madawa yenye kemikali ila leo maendeleo ya sayansi tunajikuta tunatengeneza madawa yanayotuathiri sana na madhara yake ni makubwa na yanamsaidia sana kazi malaika mtoa roho akija apati kazi dakika tu unajifia kwasababu ulishajiua muda mrefu. enzi hizo mzee akitaka kufa malaika anafanya kazi pengine wiki nzima ndo mtu uhai unamtoka ila leo hii ni kiasi kufumba na kufumbua mtu roho ina mtoka.
tujiandaeni na kifo maana kifo hakipigi hodi kama aingiavyo mgeni. kifo huja wakati wowote, mahala popote. muda mwingine unaweza ukawaza hadi ukawa unakiogopa kifo lakini atuwezi kukikimbia kwani ni kama asili ya maisha ya viumbe hai kuwa kila kilicho zaliwa kikawa hai lazima muda ukifika kipoteze uhai. tuishike imani tena imani iliyothabiti, tumrudie mwenyezi MUNGU maana yeye peke yake ndie anayejua sababu za sisi kubaki hadi leo tukiwa hai. mwenyezi Mungu anajua sababu ya sisi kuwepo hapa duniani. utakuwa RAIS, WAZIRI, POLISI utafanya kila ufanyacho lakini mwisho wa yote ni kifo na baada ya kifo kuna maisha mengine huko kaburini
kaburi limebeba historia nyingi sana za thamani, zimekuwa historia na wengine masikini wameingia makaburini kabla vitu vyao vya thamani walivyokuja navyo duniani hawaja vitumia. tumuombe Mungu mimi na wewe tusife kabla ndoto zetu hazijatimia maana tukishaingia kaburini inabaki story kuwa tulikuwepo. tufanye kila liwezekanavyo tukiri makosa yetu tuombe radhi tuliowakosea, tuwasamehe waliotukosea tufate misingi iliyowekwa kwenye vitabu vyetu vya dini. tufanye yote hayo ili tupate kuishi maisha marefu tuweze kutimiza malengo yaliyotuleta duniani kwani naamini kila kilichoumbwa kimekuja duniani kwa kusudio lake. haya ni maneno ya @eddy_mhando