Kifo cha ubeberu wa Washington China yasitisha ununuzi wa mafuta ya Marekani

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,887
Hatua ya China ya kusimamisha ununuzi wa mafuta kutoka Marekani
Serikali ya China imesimamisha kabisa ununuzi wa mafuta kutoka Marekani.
Mkuu wa shirika la meli za kibiashara nchini China amesema kuwa, kufuatia kushtadi mgogoro na pia kuongezeka vita vya kibiashara kati ya Marekani na China, Beijing imeamua kusimamisha kikamilifu ununuzi wa mafuta kutoka Marekani. Aidha Sheih-Chun Lin amevitaka vituo vya usafishaji mafuta na wafanyabiashara wa China kuacha kununua mafuta ghafi ya Marekani. Mwezi Agosti mwaka huu, China ilinunua mapipa milioni tisa na laki saba ya mafuta kutoka Marekani, hata hivyo baada ya uhusiano wa nchi mbili kuingia dowa, mwezi Septemba ilipunguza kiwango cha ununuzi huo wa mafuta na kufikia laki sita pekee. Uamuzi wa serikali ya China wa kusimamisha kikamilifu ununuzi wa mafuta kutoka Marekani, ni miongoni mwa hatua za radiamali za China kufuatia vita vya kibiashara vilivyoanzishwa na Washington dhidi ya Beijing. Mvutano wa kibiashara kati ya Marekani na China, ulishtadi kufuatia hatua ya Rais Donald Trump ya kuzipandishia ushuru wa forodha bidhaa za chuma na aluminiamu kutoka China, hapo tarehe nane Machi mwaka huu.
Kupungua kiwango cha ununuzi wa mafuta ya Marekani kwa zaidi ya mapipa milioni tisa kulikofanywa na China tena ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tu, (yaani kuanzia Agosti hadi Septemba), kunaonyesha mipango ya Beijing ya kukabiliana na Washington katika vita vya kibiashara ambavyo lengo la White House lilikuwa ni kupunguza ushindani wa kiuchumi na China katika uga wa biashara za kimataifa. Kuhusiana na suala hilo, Wang Zhiming, mtaalamu wa masuala ya kiuchumi anasema, hatua ya Marekani ilikuwa ni kujaribu kuitisha Beijing katika biashara ya kimataifa, hata hivyo Washington imeshindwa katika vita vyake vyote dhidi ya China. Mpango wa China wa kusimamisha kabisa ununuzi wa mafuta ya Marekani, unaweza kuwa na matokeo mazuri ya kibiashara kwa serikali ya Beijing katika miamala yake ya kibiashara na Washington. Hasa kwa kuzingatia kwamba, ziada ya bidhaa za biashara ya China katika mwezi Agosti uliopita ilikuwa ni ya thamani ya dola bilioni 31, ikilinganishwa na Marekani, kiwango ambacho ni ongezeko la asilimia 18.7 ikilinganishwa na mwezi mmoja kabla ya hapo.
Kinyume na tathmini ya Trump na washauri wake wa kibiashara kuhusiana na radiamali ya China katika vita vya kibiashara vya Washington dhidi ya nchi hiyo ya Asia, uamuzi muhimu wa Beijing wa kusimamisha kikamilifu ununuzi wa mafuta kutoka Marekani, unaonyesha kwamba China inatumia kwa weledi nyenzo zake kwa ajili ya kukabiliana kibiashara na Washington. Baada ya kukosekana faida katika mzungumzo na Marekani kwa ajili ya kuhitimisha vita hivyo vya kibiashara, serikali ya China sambamba na kuchukua misimamo ya kulipiza kisasi dhidi ya Washington katika kuziwekea ushuru bidhaa za Marekani zinazoingizwa China, iliwasilisha pia mashtaka yake kwa Shirika la Biashara Duniani WTO dhidi ya White House kutokana na hatua yake ya kukiuka mikataba ya kibiashara ya kimataifa. Aidha sambamba na serikali ya China kulitaka shirika lake la taifa la mafuta kusimamisha ununuzi mafuta kutoka Marekani, pia imeyawekea ushuru wa asilimia 25 mafuta ghafi ya Marekani, suala ambalo litakuwa na taathira muhimu kwa mashirika ya mafuta ya China na kuyapelekea yafadhilishe kujidhaminia nishati hiyo kutoka eneo la Mashariki ya Kati, hususan Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kuhusiana na suala hilo, Warren Patterson, mtaalamu wa masuala nishati anasema: "China ina nafasi kubwa katika stratijia ya Iran ya kuuza mafuta yake katika masoko ya Asia. Kwa kuzingatia hali mbaya ya uhusiano wa Marekani na China hasa kutokana na mgogoro wa kibiashara kati ya nchi mbili hizo, kuna uwezekano kwamba Beijing itapuuza matakwa mengi ya Marekani." Mwisho wa kunukuu.
Kwa kuzingatia kuwa ununuzi wa China wa mafuta ya Iran utayaepusha mashirika ya nchi hiyo kulipia ushuru wa asilimia 25 kama yangenunua mafuta ya Marekani na wakati huo huo kuwezekana kufanyika miamala ya kifedha kati ya Tehran na Beijing kwa kutumia sarafu ya taifa la China (Yuan), ni mambo ambayo yameyavutia sana mashirika ya China kufanya biashara ya mafuta na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Aidha hatua ya China ya kusimamisha kabisa ununuzi wa mafuta kutoka Marekani imetoa ujumbe kwa Rais Donald Trump kwamba kinyume na alivyokuwa amepanga kufuatilia siasa zake za uhasama za kutaka kusimamisha kabisa uuzaji nje wa mafuta ya Iran katika masoko ya kimataifa, sasa siasa hizo zimemgeukia yeye mwenyewe na kuzua wasiwasi wa uwezekano wa kusimamishwa kabisa uuzaji nje wa mafuta ya Marekani. Uamuzi huo wa China inayotajwa kuwa mnunuzi mkubwa wa pili wa mafuta ya Marekani, unatokana na kufeli kwa Washington katika vita vyake vya kibiashara na China. China imesimamisha ununuzi wa mafuta kutoka Marekani na hivyo kutoa pigo kwa Washington 
Vita vya kibiashara vilivyoanzishwa na Marekani vimepelekea kususiwa mafuta yake 
Trump ambaye ana
 
Trade War haijawah muacha mbabe salama! US anashindwa soma alama za nyakati na anashindwa kujua China ni Nchi No 2 Duniani kwa uchumi mkubwa baada ya US na projection inavoonesha by 2030 uenda China ndo ikawa namba 1 duniani kwa uchumi wenye nguvu! US anapoteza nguvu nyingi kwenye uchumi wake na deni kubwa lilisababishwa na vita ya Afghanistan na Irak vita bado inaendelea kule Afghanistan na Irak imechukuliwa na mahasimu wake Iran hivyo anatumia fedha nyingi kuirudisha kitu ambacho hatafanikiwa....Leo Mbwekaji wa Trump kule UN Nick Haley ka resign inaonekana kachoka kumtetea Boss wake ambae amejiingiza kwenye migogoro na kujitoa kwenye mkataba wa kimataifa wa Nuclear wa Iran na Tusishangae mtu atakae mrithi akawa Kanye West.....
 
China atapata tabu sana kwenye gii Vita. Aache uhuni wa kucheza na thamani ya pesa yake. Pia aweke mazingira ya soko huru kama wenzake. Ukitaka kula lazima uliwe.
 
Marekani ni shavu Nene, China aje auze midoli huku afrika
 
Marekani ni shavu Nene, China aje auze midoli huku afrika
Hii ligi bado sana, tuwekeni manano ya akiba jaman, hebu tusubirin hapo washington majib yao yanakujaje,....lakini kadiri nijuavyo ni kwamba anaeanzisha vita alishajiandaa na kujua silaha gani anaitumia, sidhan kwamba akili zoote za hao watu hapo Washington wakati wanaanza hili hawakujua kwamba kuna majib ya namna hii? Kuna kanmsemo kalikua kanasema mmarekan akikohoa dunia hupata mafua....kamebeba uzito mkubwa sana.watu ambao wameongoza dunia hii karibu karne nzima sasa sio wa kuanguka hivyo kipumbavu namna hii, pili mnamwonea Trump.bure tuu, hio ni sera iliokuwepo.mezani some yrs back yeye ni mtekelezaji tuu..kwa akili zoote zilizopo hapo Washington, marais woote wastaaf, mabilionair woote,,marafiki majiran kama UK, Jews, woote hawa wamelala wasiwabonyeze swahiba wao then macho kuvimba aje ashinde hii vita.......hii ni kujitia moyo kama ile kauli yetu kwamba sisi africans ndio wenye akil nyingi
 
Back
Top Bottom