Kifo cha TRC :Wahujumu Uchumi na Mafisadi wamehusika na kuneemeka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifo cha TRC :Wahujumu Uchumi na Mafisadi wamehusika na kuneemeka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Oct 7, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kifo cha TRC :Wahujumu Uchumi na Mafisadi wamehusika na kuneemeka

  Waswahili husema temba ujionee. Enzi za enzi, malori yalikuwa ni Mwanamboka na Superdoll, Kugis na Wachaga wachache.
  Leo hii mtiririko wa Malori ni mkubwa mno na unatisha. Nimeona malori mengi sijapata ona katiba vijibarabara vyetu. Katika umbali wa kilometa 60, pale Saranda mpaka Isuna Singida ambako hakuna lami, nimekutana na malori 300+ katika kipindi cha dakika 90! Barabara mbovu, bado ya kokoto na mchanga, malori ni makubwa mno na mazito.
  Nikakum buka foleni ya maloriniliyoiona KIbamba, Mlandizi, Chalinze, Morogogoro na Gairo. Nikajiuliza imekuaje Tanzania kuna malori mengi kiasi hiki?
  Nikajiuliza, kwani hatuna reli kusafirisha mizigo, iwe ni makontena, mafuta hata marobota ya pamba?
  Jibu lake ni kuwa TRC imekufa baada ya Serikali kuamua kuwaleta Rites waiendeshe na wala si wale Wajerumani.
  La zaidi baada yakuongea na wafanyabiashara wengi, nikaambiwa zaidi ya asilimia 50 (50%) ya malori ya mizigo, ni mali za viongozi wa Serikali, Polisi na watumishi wa Umma!
  Wale wadudu wa Mukichwa wakaunganisha moja jumlisha moja ni Uhujumu!
  Sasa siku nyingi nilikuwa nikidhamiria kuwalaumu Rites, ambao hawakwepi lawama kwa kutuhukulia mabehewa yetu na kutuletea vihiyo kuongoza kampuni yetu. Lakini wao walikuwa ni wepesi kuhongeka na si Mjerumani na ndio maana Serikali ikakimbilia kuileta Rites na si ajabu kama Richmond, walikuwa na bei Poa!
  Kilivhotokea ni kujihujumu wenyewe na wala tusielekeze vidole kwa Rites, wao lawama kwao na kuwajibika kwa ni matokeo ya nia na vitendo vyetu.
  Ama kweli Tanzania itajengwa na wenye Meno! Ikiwa wakubwa wanadiriki kulihujumu Taifa kwa kuzamisha utendaji wa Shirika la Reli ili wao wapate pesa kutokana na malori yao, swali linakuja, kwanini basi tusiwaongezee makosa ya kuharibu barabara zetu, kuharibu mazingira, kuongeza uagizaji wa vipuli vya magari na ongezeko la ununuzi wa mafuta?
  Mnakumbuka ule mkasa wa Elisante Muro kutaka kujenga bomba la mafuta ambalo alipewa Richmond, na sasa mtu mwingine? Kama Muro alikuwa na pesa na kila kitu kujenga bomba kama la Tazama kutoka Dar mpaka Mwanza, hatuoni kuwa tusingekuwa na haja ya kuwa na matenka ya mafuta ya mita kumi yakiongozana barrabarani huku yakididimiza lami yetu na kuleta msongamano?
  Hivi hawa wahujumu, ni wajinga kiasi gani kuwa hawaoni dhamira zao kwa kuhujumu kimoja jinsi kinavyohujumu vingi , mengi na wengi?
  Wengine wao wamediriki hata kutafuta watu wakangÂ’oe mataruma ya Reli kwa makusudi kabisa ili Reli isipite, sasa siku Reli ya Rwanda ikianza kazi sijui itakuweje!
  Labda tuwape semina hawa viongozi wetu tuwafundishe nja za ujasirimali na uzalishaji mali ambazo hazitaleta hujuma!
  Poleni Wahindi wa Rites, mnabeba msalaba mzito kwa kuwa mliingizwa mkenge!
   
 2. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hawa wenye malori siyo wajimga kama unavodai Rev,wanapata maslahi makubwa na ndio haja yao.
  kwani wanajali nini hata hizo barabara zikiharibika au kuleta msongamano??
  Wao wakitaka kupita si watu wanaondolewa barabarani wao wapite?na tumbo mbele na ubinafsi uliokithiri ilhali wengi wa watanzania wakiishi katika mazingira magumu ya umaskini uliokithiri.
  Am sympathetic with Tanzanians ila hoping kila kilicho na mwanzo kina wisho!
   
 3. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Kaka, walichota hapo, na wakaenda kununua Reli ya Kenya /Uganda (RVR). Si unajua Kampuni ya RA ndo ilipata ile tenda ya kununua Reli ya Uganda? Walichota hapo....Lakini bahati wakenya walistuka na kusitisha lile zoezi. Nakwambia bila RA, Chande, EL nk kupunguzwa nguvu zao za maamuzi serikalini, ni bure. Come 2015, watachukua hii nchi...na hapo ndipo mtaimba.....
   
 4. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Kuna vitu vingine ni ngumu kuvielewa. Maamuzi mengine ya serikali sijui nani anayapa baraka. Yamejaa watu wasiojari consequences zake hata kama siku moja inawezekana wakadaiwa zaidi tokana nayo.
  Mungu ibariki Tanzania. Huyu shetani anayetuandama, sasa mpatilizie mbali. Nchi yetu irejee kule inakota kwenda.
   
 5. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nadhani dawa ni kutoa amri au sheria ndogo itungwe kuwa sehemu zote inakopita reli malori ni marufuku kupeleka mizigo tuone watafanya nini. wizara husika iandae bill.
   
 6. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ipo siku watachoka na ulimbukeni wao na kugundua vitegauchumi vinavyolipa zaidi huku vikiinua zaidi ubora wa maisha wa wananchi.
   
 7. s

  shabanimzungu Senior Member

  #7
  Oct 8, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani the whole saga of TRC and now TRL is by one person-self styled and bought out title ''''''''''Sir"""" Andy Chande...he is the biggest fisadi and he was the one who brought these indians to loot the country...he colluded with Mkapa. When wil u all learn.???????????.He must be exposed..if any Journalist is reading this he must investigate this isue and it will be the biggest scoop! But rememebr he is a freemason and Mkapa is also one..so they protect one another...........JUST KICK THESE INDIANS OUT ........WE CAN DO IT..ENOUGH IS ENOUGH ..VISIT ANDY CHANDES WEBSITE AND YOU WILL SEE HE IS WITH MKAPA ALL THE TIME...............
   
 8. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Leo hii barabara msongamano, barabara zinamomonyoka, Reli imelala kifo cha Mende tunasubiri Reli ya Rwanda ifanye kazi!
   
 9. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kulikuwa na kampuni za uchukuzi kila mkoa nazo zimekufa kifo cha mende. Wanaokumbuka kampuni kama MORETCO n.k n.k Yaani inasikitisha. Kuna mtu anayejua shirika la Maendeleo Dar es Salaam linafanya kazi gani zaidi ya kupangisha magofu yake yaliyobaika mjini na akina Kingunge kupata commission? Tuanzie hapa.
   
Loading...