Kifo cha Swetu Fundikira

Tatizo bongo hatuna wanaharakati wa kweli. Hiki kipondo cha jamaa kingetokea Marekani kwa mfano, ungeona tayari watu washaandamana na kubeba mabango Pentagon. Na wish tungekuwa na kina Al Sharpton wetu....

nasubiri maandamano ya yule mjeshi aliyeua wenzake zaidi ya 10... na ya yule mbongo aliyechomwa kisu pale london... na ya brian mazula, na ya kupaza, na ya kapalata
 
nasubiri maandamano ya yule mjeshi aliyeua wenzake zaidi ya 10... na ya yule mbongo aliyechomwa kisu pale london... na ya brian mazula, na ya kupaza, na ya kapalata

Huyo mwarabu wa Fort Hood kwishnee. Kwanza hakuua raia. Aliua wajeshi wenzake.

Mbongo yupi huyo aliyechomwa kisu London?

Na get your facts straight. Brian Mazula anaingiaje hapa? Kupaza who? Wa Wisconsin? Kapalata muuaji wake anajulikana na hakuwa mwanajeshi (ambaye amekula kiapo kulinda wananchi na si kuwaua)....
 
Hawa askari wakipatikana na hatia ni wapewe adhabu kama invyo stahili .Ila kinanishangaza hata huyu mama aliiweza kumpiga marehemu pia?.
Hili tukio haliko wazi nadhani kuna kitu kinafichwa , sidhani kama ina husiana na Marehemu kuchukua bibi, haswa ukimwangalia huyo jimama hapo sidhani kama ndio chanzo.
kama nilivyo sema mwanzo, hapo kwa Manyanya wakati wa usiku mara nyingi police wenye magari huwa wanakula hapo.Ktu ambacho kina weza kua kilitokea ni Marehemu kuendeSHA gari vibaya na labd akutaka kuwagonga hao police na kupelekea kuwaudhi hawa askari kiasi cha kuanza kumfuatilia.
Swali pale pale kuhusu gari gani huwa anaendesa huyu marehemu,(kama nilivyo jibiwa na mdau sitopewa jibu) , nahisi hiyo Nissan patrol ina husika , ina wezekana ndio ya huyu marehemu.
 
Huyo mwarabu wa Fort Hood kwishnee. Kwanza hakuua raia. Aliua wajeshi wenzake.

Mbongo yupi huyo aliyechomwa kisu London?

Na get your facts straight. Brian Mazula anaingiaje hapa? Kupaza who? Wa Wisconsin? Kapalata muuaji wake anajulikana na hakuwa mwanajeshi (ambaye amekula kiapo kulinda wananchi na si kuwaua)....

Wazee... hata mubishane au muiweke vipi... muuaji ni muuaji... awe padri, mjeshi, mwanamuziki etc. hatuwzi kuandamana kwa kuwa aliyeua yuko hivi au vile... a murder cant be anything else....

wale ni walevi wamegombana wakapigana wakauana hata tuiweke vipi!!! wht if kesho ukiambiwa swetu alikua usalama wa taifa?? tutasema sawa tu wamemalizana wenyewe??

the bottom line ni kwamba tunajiweka katika mazingira hatarishi

  • kwanza kwa excessive drinking
  • then we drive
  • then we provoke each other
  • then we fight
  • and forget who we are

WE CANT PAINT ANY OTHER PICTURE THAN BLAMING BOTH PARTIES... BAHATI MBAYA MMOJA KATANGULIA MBELE YA HAKI RIP

kv
 
SI KWELI HATA KIDOGO.....!

JWTZ litabaki ni jeshi imara na lenye nidhamu ya hali ya juu! mapungufu yetu wananchi ya KUWACHOKONOA wapiganaji hawa ndo huwa yanaleteleza haya yanayowafika.....!

Ndio pia pale dhana tajwa kuwa AKUANZAYE MMALIZE.....! Inapofanya kazi sawia....!

Askari wetu ni wapole wakati wa amani.....na hiyo ndiyo sifa yao kuu.....na pia ni wakali pale choko choko za aina yeyote zinapoelekezwa kwao.

pindi wanapochokozwa wananchi na vyombo vya habari huwa kimya.....ila pale wanapotoa majibu ya yale yaliyoelekezwa kwao kelele na vilio hutawala juu yao....! Na pia hapa tunaona KATI YA VYOMBO VYA USALAMA (polisi, jwtz, jkt, magereza, takukuru, mgambo, sungusungu, uhamiaji, jku & valantia) vinapokuwa katika mikwaruzo.... AIDHA WAO NA WANANCHI au WAO NA POLISI.....

POLISI HUHESABIWA HAKI NA VYOMBO VILVYOBAKI HUTWISHWA MZIGO WA LAWAMA....!

JWTZ msirudi nyuma kwa kelele za chura.....!
Nakubaliana na wewe kwa kulisifu jeshi letu,lakini mwanajeshi mwenye nidhamu ya kweli aliyepitia heavy training ya kijeshi hawezi kufanya aliyoyafanya hao walioua.Nakumbuka nikiwa jeshini,nafanya kozi ya gojyu-ryu.siku zote lazima uambiwe hii inatumika kwa self-defence na ukiwa kazini(tena purposely).Sababu mwanajeshi yeyote hata kama hana silaha,tayari yeye mwenyewe ni silaha.So hao walioamua kulipaka jeshi matope hawastahili kuwa jeshini wala uraiani sababu wameshindwa kujitambua wenyewe ni wakina nani na kuruhusu pombe iwatawale na kufanya waliyoyafanya.Ndo maana ya kufundishwa uvumilivu jeshini,yale manyanyaso yote unayopata kutoka kwa walimu ni kukufanya uwe mvumilivu.Kumbuka raia hakutambui na wala hajui skills ulizo nazo.Nilishashuhudia raia akimtukana askari matusi ya nguoni aliyevaa gwanda pamoja na SMG-full magazine,na jamaa akacheka tu.Itakuwa hao ambao walikuwa kiraia.
 
SI KWELI HATA KIDOGO.....!

JWTZ litabaki ni jeshi imara na lenye nidhamu ya hali ya juu! mapungufu yetu wananchi ya KUWACHOKONOA wapiganaji hawa ndo huwa yanaleteleza haya yanayowafika.....!

Ndio pia pale dhana tajwa kuwa AKUANZAYE MMALIZE.....! Inapofanya kazi sawia....!

Askari wetu ni wapole wakati wa amani.....na hiyo ndiyo sifa yao kuu.....na pia ni wakali pale choko choko za aina yeyote zinapoelekezwa kwao.

pindi wanapochokozwa wananchi na vyombo vya habari huwa kimya.....ila pale wanapotoa majibu ya yale yaliyoelekezwa kwao kelele na vilio hutawala juu yao....! Na pia hapa tunaona KATI YA VYOMBO VYA USALAMA (polisi, jwtz, jkt, magereza, takukuru, mgambo, sungusungu, uhamiaji, jku & valantia) vinapokuwa katika mikwaruzo.... AIDHA WAO NA WANANCHI au WAO NA POLISI.....

POLISI HUHESABIWA HAKI NA VYOMBO VILVYOBAKI HUTWISHWA MZIGO WA LAWAMA....!

JWTZ msirudi nyuma kwa kelele za chura.....!
Duuh, kwahiyo wakikasirika wao ni kupiga tuu kwa kwenda mbele? Kwanini wasihusishe vyombo vingine vya sheria?
Tunapata nini sasa kama askari wanaua na wako mahakamani wakitakiwa kujibu mashitaka? Mi sikubaliani na hilo. Kwa training zao, askari hawawezi wakakabiliana na raia kwa mabavu halafu raia wakaweza kusimama. Lazima wajue kuwa training zao ni kwa specific use. Siyo kwenda kupigana na kila dereva wa daladala na kila mlevi barabarani. Kama wataendelea kufanya hivyo watajaa magerezani kama watuhumiwa.
Nidhamu bado ni kitu muhimu sana.Kama mimi nisiye askari silewi nikapoteza mawasiliano, kwanini askari walewe hivyo?
 
eti huku majuu, as if its something new, name a state and we share experience wewe senene

hayo ya thanks kwa ****... Sihitaji senksi yako kwani siishi utakavyo wewe!!! It doesnt matter unavyoichukulia ila utambue kwamba walipofanya mauaji hayo hawakuwa kazini bali walikuwa kama cohort ya buddies wakiwa kwenye starehe, tuache kuchanganya madesa, narudia tena!!!

Case ya askari ni kama ile ya mwanajeshi aliyempiga polisi ubungo, hayo mengine hayafanani

hivi yule askari wa marekani mwenye asili ya kiarabu aliyeua wenzake zaidi ya kumi case yake imechkuliwaje?

Matusi tunaweza tena bila mauzauza, ila kwa ****** kama wewe tunaamua kukaa kimya kwani wewe hujui ufanyalo na hiyo laana imetoka kwa ndugu zako kima wewe

hiyari yashinda utumwa, na kwa wote walio majuu kwa ajili ya kutafuta nawapa heshima kubwa, ila kama wewe uko majuu kukimbia wanajeshi ambao wengine ni ndugu zako, nakupa pole sana maana hata tumbili alikimbia mnazi akalala kwenye mwembe

#$%^&*(_)(*&^

sasa ni lunch time

safi hiiiiiiiiiiii!!!!!!!!
 
Ukosefu wa nidhamu tu hapo. Kwani ukiwa askari au mwanajeshi mtu akikutukana adhabu yake ni kipigo mpaka kuuwa? Siku hili haya majeshi wanaingiza wahuni tu. Mara polisi wanashiriki kwenye ujambazi mara wanaeshi kupiga raia mpaka kuuwa. Sijui nini maana yake?
 
Chukulia scenario hii: uko baa unakula ze laga. Jamaa flani anakukorofisha kinamna halafu mnajibizana mbovu, yanaisha. Mda wa kurudi home unaendesha gari yako, mgomvi wako yule yule anakuja na gari yake anakupita kimanjonjo halafu gari yake inakwaruza ya kwako, halafu anaendelea na safari kama vile anafurahia alichokufanyia. Unaamua kumfukuzia, na yeye anaongeza mwendo, hadi mnafika mahali unafanikiwa kumpita na kum-block kwa mbele. Unashuka na mihasira kuuliza kulikoni. Unajibiwa 'Gari lipi nimegonga? Hili nalo gari? Kama umezoea kufi*wa na babako usilete us*nge wako hapa, **** nini. Kafi*we huko, kum********!' Na ngumi unaziweza. Kitafuata nini?

NALAANI MAUAJI HAYA, SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, ILA KILICHOPO CHA KUJIFUNZA PIA TUJIFUNZE. ELIMU HAINA MWISHO, NA ELIMU NYINGINE GHARAMA YAKE NI KUBWA SANA.
 
thanks saaana kwa kuona hili... wauwaji hawakuua kwasababu ni wanajeshi, waliua kwasababu ya ugomvi ulichangiwa na pombe ya muda mrefu na huyo mjeshi na mkewe walishakuwa na bifu na marehemu kabla ya gari kuondoka

tumesahau kwamba wanajeshi ni watu tunahukumu kwa kazi zao, sijui wangekua walimu tungesema walimu wauaji au vipi... TAHADHARI, WAUWAJI WALIUA KWA SBABU YA UGOMVI NA SI KAZI YAO TUSIPOTOSHE UKWELI

ufupi wa kutafakari unatufikisha hapa tulipo

Matukio kama haya yawezekana kuwa yanatokea mara kwa mara lakini hili kwa kuwa limemhusu mtumishi wa JWTZ na mtoto wa Fundikira ndiyo maana limekuwa reported.

Si vyema kulipaka matope Jeshi letu wakati mtumishi huyu alikuwa katika starehe zake binafsi na kama inavyosemekana walikuwa wakitokea katika ULEVI.
 
Chukulia scenario hii: uko baa unakula ze laga. Jamaa flani anakukorofisha kinamna halafu mnajibizana mbovu, yanaisha. Mda wa kurudi home unaendesha gari yako, mgomvi wako yule yule anakuja na gari yake anakupita kimanjonjo halafu gari yake inakwaruza ya kwako, halafu anaendelea na safari kama vile anafurahia alichokufanyia. Unaamua kumfukuzia, na yeye anaongeza mwendo, hadi mnafika mahali unafanikiwa kumpita na kum-block kwa mbele. Unashuka na mihasira kuuliza kulikoni. Unajibiwa 'Gari lipi nimegonga? Hili nalo gari? Kama umezoea kufi*wa na babako usilete us*nge wako hapa, **** nini. Kafi*we huko, kum********!' Na ngumi unaziweza. Kitafuata nini?

NALAANI MAUAJI HAYA, SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, ILA KILICHOPO CHA KUJIFUNZA PIA TUJIFUNZE. ELIMU HAINA MWISHO, NA ELIMU NYINGINE GHARAMA YAKE NI KUBWA SANA.

Hapo lazima ujifunze ku-control temper yako - ukishidwa basi inakuwa tatizo kubwa kama hilo lililotokea.

Wote walijibizana kwa jazba ndipo kukapelekea mambo haya, ndiyo maana wanasema usitumie mingumi watu wanatembea barabarani washakufa siku nyingi tu, kofi moja tu chali - umeuwa duh. hapo si chini ya miaka 30 jela.

Harafu mzee umeandika sawa sawa as if ulikuwepo kwenye eneo la tukio - au we ndo yule jamaa wa tatu aliyekimbia nini?
 
Chukulia scenario hii: uko baa unakula ze laga. Jamaa flani anakukorofisha kinamna halafu mnajibizana mbovu, yanaisha. Mda wa kurudi home unaendesha gari yako, mgomvi wako yule yule anakuja na gari yake anakupita kimanjonjo halafu gari yake inakwaruza ya kwako, halafu anaendelea na safari kama vile anafurahia alichokufanyia. Unaamua kumfukuzia, na yeye anaongeza mwendo, hadi mnafika mahali unafanikiwa kumpita na kum-block kwa mbele. Unashuka na mihasira kuuliza kulikoni. Unajibiwa 'Gari lipi nimegonga? Hili nalo gari? Kama umezoea kufi*wa na babako usilete us*nge wako hapa, **** nini. Kafi*we huko, kum********!' Na ngumi unaziweza. Kitafuata nini?

NALAANI MAUAJI HAYA, SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, ILA KILICHOPO CHA KUJIFUNZA PIA TUJIFUNZE. ELIMU HAINA MWISHO, NA ELIMU NYINGINE GHARAMA YAKE NI KUBWA SANA.

unachosema kinafanana na taarifa nilizozipata ..jana...wanasema kuwa jamaa walikuwa na majibishano tangia maeneo ya mango ...pamoja na jamaa akawatukana ..jamaa wakakasirika wakaingia garini...wakaondoka..marehemu na wenzake wakaendelea kuwafuuata na kuwapita kwa kasi.......ikaishia askari hao kuwapita tena na ndipo vurugu zikaanza.....nashauri ...yule aliyekuwa na marehemu kwenye gari naye akamatwe kama shahidi .....ili kuweka sawa taarifa kwa polisi....

si vema kumchokoza yeyote sembuse askari....ila kosa kubwa walilofanya askari ambalo litawasababishia kunyongwa ni kumpigga na kuondoka naye na kuendelea kumpiga.......wangeweza kumpiga pale pale na kumuacha...tungesema ni hasira......na wangeweza kujiokoa na adhabu ya kifo....ikawa wameuwa bila kukusudia...lakkini sasa hii ni manslaughter live!!

labda sasa wapate wakili atakayeweza kujenga hoja yao kuwa walitaka kuporwa gari...amabayo hata hivyo haionekani kuwa significant.....haina uzito...[hakuwa na silaha]
 
Hii ndio niliokua naitaka isemwe... lets be fair in every judgement!!! umenena neno safi

Matatizo yalikuwapo pande zote mbili na for this matter to be dealt appropriately ni lazima waliokua na marehemu wapatikane na watoe ushahidi, gari zilizokua involved zifanyiwe forensic na ikibidi hata waliokua mango garden wahojiwe

ULEVI UNATUPONZA VIJANA WENGI SWETU SI WA KWANZA KUFA KWA KIPIGO NA HATAKUA WA MWISHO --- ITS ANOTHER INDICATION OF A FRUSTRATED SOCIETY WE LIVE IN
 
Nimewapata vema kabisa sasa kuwa inawezekana kabisa jamaa walichikozwa sana na huyu bwana. na kuna watu wana maudhi maana wanatalalila nyingi maneno ya hovyo kibao ambayo yanapandisha munkari wa mtu bila sababu.
Lakini turudi palepale kwamba kuna watu wanatembea lakini ni wagonjwa mahututi. Kama askari wataendelea kutoa toa vipigo ndiyo mwanzo wa kuwa wauaji bila mpango.Moja ya vigezo vya kufanya kazi jeshini ni afya njema. Sasa ukituona tumevimbiana mtaani ukahisi tuna afya njema na tunaweza kuhimili vishindo vya askari jeshi ni makosa makubwa. Ni sababu ya ugali rosti zisizo na idadi tunazokula.
Kama wangelimu arrest na kumpeleka huyu jamaa polisi,pamoja na uwezekano kwamba alikuwa na mdomo mchafu leo tungekuwa na mambo tofauti.
 
Nimewapa vema kabisa sasa kuwa inawezekana kabisa jamaa walichikozwa sana na huyu bwana. na kuna watu wana maudhi sana maana wanatalalila nyingi maneno ya hovyo kibao ambayo yanapandisha munkari wa mtu bila sababu.
Lakini turudi palepale kwamba kuna watu wanatembea lakini ni wagonjwa mahututi. Kama askari wataendelea kutoa toa vipigo ndiyo mwanzo wa kuwa wauaji bila mpango maana moja ya vigezo vya kufanya kazi jeshini ni afya njema.Sasa ukituona tumevimbiana mtaani ukahisi tuna afya njema na tunaweza kuhimili vishindo vya askari jeshi ni makosa makubwa. Ni sababu ya ugali rosti zisizo na idadi tunazokula.
Wangelimpeleka huyu jamaa hata kama alikuwa na mdomo mchafu polisi leo tungekuwa na mambo tofauti.

Nadhani ili tupate undani wa hili tatizo ni bora tungejua wasifu wa marehemu... alifanya kazi gani, alikua mtu wa namna gani nk.
 
Hii ndio niliokua naitaka isemwe... lets be fair in every judgement!!! umenena neno safi

Matatizo yalikuwapo pande zote mbili na for this matter to be dealt appropriately ni lazima waliokua na marehemu wapatikane na watoe ushahidi, gari zilizokua involved zifanyiwe forensic na ikibidi hata waliokua mango garden wahojiwe

ULEVI UNATUPONZA VIJANA WENGI SWETU SI WA KWANZA KUFA KWA KIPIGO NA HATAKUA WA MWISHO --- ITS ANOTHER INDICATION OF A FRUSTRATED SOCIETY WE LIVE IN

Kwanza kwenye red hapo ni cheap conclusion.

Pili, kwa polisi wapi amabao watafanya forensic investigation?
Issue ni kwamba, watafanya hivyo kwa faida ya nani? they dont know why they became policemen/women at the first place.
 
Shukran tumekusoma yaani wewe umeamua kwamba huyo MTM kusema frustrated society ndio cheap... hebu eleza wewe unadhani ni nini... mimi nimesoma amesema "nadhani" kumbe nadhani ni conclusion... i thought ni speculation
 
PM,
Naona tangu jana unatetea sana Wanajeshi kuuwa mtu.

Sipo hapa kutetea maneno machafu aliyoyasema Swetu (sijui kama ni kweli).

Tanzania maisha ya mtu ni rahisi sana na naona tunakuwa kama Warusi vile.

Dereva kagoma kushuka kwenye gari (daladala), Brother Dito (mjeshi) anatoa cha moto anamlima LIVE. Halafu kama hakijatokea kitu, huyooo anaondoka.

Swetu kakwaruza gari na kurusha meneno machafu (hivi wao hawakurusha? Tena wanajeshi wanatukana utafikiri midomo yao inashinda Ch00ni) basi yeye anapata kichapo cha mbwa. Hebu ona kichwa kilivyovimba. Halafu mnasema kofi moja, wee unaona kichwa kimeharibika halafu unasema wengine wanatembea ni marehemu? Jamaa anaonekana kama Francky Bruno kamaliza kupata kipigo kutoka kwa Tyson halafu mtu unasema Swetu alikuwa "Dead Man Walking?" Hebu acheni mzaha. Hicho kipigo hata angelikuwa ni Badr Hari wa K1, angeliweza hata kufa, sembuse mtu wa kawaida kama Swetu?

Mwisho tuseme ukweli, maugomvi hasa yanayomalizia NGUMI si mazuri kwani unaweza kweli kukutana na dead man, ukamuwahishia tu siku zake chache zilizokuwa zimebaki na yakakukuta.

Hiyo ilishawahi kutokea kwetu kata moja iitwayo Chabutwa. Kijana mmoja wa Kiarabu karudi likizo na kufika nyumbani jioni kakimbilia kwenye uwanja wa mpira wa miguu. Kuingia tu dakika za mwisho, akaanza kucheza rafu si kawaida. Kijana mmoja alirukiwa teke la kifuani na kijana akaanguka. Walipompa huduma ya kwanza kijana akanyenyuka na kuamua kukaa pembeni ya uwanja. Dakika kama kumi baadaye mechi imeisha, yule Mwaarabu na yeye kakaa chini na ghafla akapoteza fahamu. Wakambeba mbio kwenda Sikonge Hospital ila hata kabla hawajafika, kijana akawa amefariki. Yule kijana aliyepigwa teke nasikia ALILIA kwa furaha kuwa 'Kama angelipiza kisasi??!!'. Baadaye ikaja julikana kuwa Mwaarabu alikuwa na Asthma na kifua kilibana baada ya mechi na kikamuuwa.

Wakuu, maugomvi si mazuri bila kujali wewe ni nani na unagombana na nani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom