Kifo cha Swetu Fundikira

Mara nyingi nikiwa kwa Manyanya kununua chips chafu, huwa naona sana Nissan Patrol ya rangi ya orange, hii gari huwa kwanza ina kuja kwa fujo ,kupaki kwa fujo na kuondoka kwa fujo, speed yake ikija utadhani iko kwenye rally, Imesha taka kunigonga mara moja na siku iliyo fuata ili mgonga muuza chips na kuondoka bila kujali na si mara moja,

Niliuliza ni ya nani ,nikatajiwa jina la mtu mwenye famous last name ,ila nime sahau ni nani , sasa nilikua naomba kuuliza huyu marehemu Swetu alikua anaendesha gari gani ?

I bet my foot, hautaambiwa alikuwa anendesha gari gani!!!
 
TAARIFA za baadhi ya wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kumpiga hadi kumsababishia kifo, Swetu Fundikra, ni za kusikitisha na haziwezi kupita bila kujadiliwa.

Kwa moyo wa uchungu, tunachukua nafasi hii kuwapa pole ndugu na jamaa waliofikwa na msiba huo na Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.

Kwanza tungependa kuweka bayana kwamba hatuingili kazi za jeshi na kwa hali hiyo hatuhatarishi usalama wa taifa kwani tunaamini hakuna aliye juu ya sheria.

Tunaandika tahariri hii, tukiwa na kumbukumbu ya msururu mrefu wa vitendo vya askari wa JWTZ kujichukulia sheria mkononi na kuwanyanyasa wananchi wenzao kwa kuwashushia vipigo bila sababu za msingi.

Mei, 19 mwaka jana, askari wa JWTZ ambao kimsingi ndio waliokabidhiwa kuhakikisha usalama wa raia wenzao na nchi yao kwa jumla wanakuwa salama, walimvamia na kumpiga kinyama askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Sajenti Thomas Mayapala, kwa madai kwamba aliwachelewesha katika safari yao wakati wa kuyaongoza magari katika makutano ya barabara za Morogoro, Nelson Mandela na Sam Nujoma.

Mwaka jana pia, JWTZ waliripotiwa kufanya ghasia na kuwajeruhi vibaya raia kadhaa ikiwa ni kulipiza kisasi cha raia hao kumwadabisha mwanajeshi aliyenaswa akijihusisha kingono na msichana ambaye ni mwanafunzi wa sekondari.

Tukio hilo lilikuja wakati jijini Dar es Salaam kukiwa na mzozo unaowahusisha askari wa JWTZ ambao waliwapiga na kuwashikilia kwa muda wafanyakazi kadhaa wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco) waliokuwa wakiendesha operesheni ya kukata maji katika makazi na kambi za jeshi kutokana na kulimbikizwa kwa deni la ankara linalofikia sh milioni 276.

Kama hiyo haitoshi, wanajeshi kadhaa walivamia kituo kikuu cha usambazaji maji cha Dawasco kilichopo Ubungo, kuwazuia wafanyakazi waliokuwapo na kupora kamera ya mwandishi.

Mlolongo wa matukio ya askari hao kwa mwaka jana kuwashushia kipigo raia ni mrefu na unahitaji ukurasa mzima kuutaja.

Je, askari hao wa JWTZ wanafahamu kwamba wao ni raia kama Watanzania wengine ambao wanapaswa kufuata sheria za nchi na kwamba sheria haiogopi kazi au wadhifa?

Askari hao wanafahamu pia kwamba wajibu wao mkubwa kwa nchi ni kuhakikisha furaha na usalama wa raia wenzao badala ya kuwaonyesha ubabe na ukatili eti kwa vile tu wamekabidhiwa nguvu za juu zaidi za dola katika nchi hii?

Msimamo wetu ni kwamba vitendo vilivyofanywa na askari hao wa Dar es Salaam na kwingineko havikubaliki kwa kisingizio chochote kile, vimeishushia hadhi JWTZ mbele ya wananchi na kuondoa heshima waliyokuwa wakipewa kutokana na majukumu yao nyeti ya ulinzi wa wananchi, mali na rasilimali zao.

Vitendo hivyo viovu si tu vinakwenda kinyume na maadili ya uaskari, bali pia vinakinzana na dhana nzima ya utawala bora ambayo wanajeshi wanapaswa waiheshimu na kuifuata.

Ni bora wanajeshi hao wangetumia muda na nguvu zao kuihimiza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kutimiza jukumu lao la kulinda usalama wa raia na mali zao badala ya kumshambulia marehemu Fundikira.

Kwa niaba ya wananchi tunakemea ubabe huu unaoanza kuzoeleka wa askari wa JWTZ kuwashambulia raia na tunatarajia kutoka kwa makamanda wa juu kauli na hatua kali za kuwaadabisha waliohusika na ahadi kwamba siku za mbele hakutakuwa na matukio mengine kama haya, vinginevyo tunachelea kusema kwamba imani ya wananchi kwa jeshi itapungua.
 
SI KWELI HATA KIDOGO.....!

JWTZ litabaki ni jeshi imara na lenye nidhamu ya hali ya juu! mapungufu yetu wananchi ya KUWACHOKONOA wapiganaji hawa ndo huwa yanaleteleza haya yanayowafika.....!

Ndio pia pale dhana tajwa kuwa AKUANZAYE MMALIZE.....! Inapofanya kazi sawia....!

Askari wetu ni wapole wakati wa amani.....na hiyo ndiyo sifa yao kuu.....na pia ni wakali pale choko choko za aina yeyote zinapoelekezwa kwao.

pindi wanapochokozwa wananchi na vyombo vya habari huwa kimya.....ila pale wanapotoa majibu ya yale yaliyoelekezwa kwao kelele na vilio hutawala juu yao....! Na pia hapa tunaona KATI YA VYOMBO VYA USALAMA (polisi, jwtz, jkt, magereza, takukuru, mgambo, sungusungu, uhamiaji, jku & valantia) vinapokuwa katika mikwaruzo.... AIDHA WAO NA WANANCHI au WAO NA POLISI.....

POLISI HUHESABIWA HAKI NA VYOMBO VILVYOBAKI HUTWISHWA MZIGO WA LAWAMA....!

JWTZ msirudi nyuma kwa kelele za chura.....!
 
mahesabu

ubungo walipowachapa makofi matrafic walichokozwa
baraabara za baba zao waamue muda gani wa kupita?
 
POLISI HUHESABIWA HAKI NA VYOMBO VILVYOBAKI HUTWISHWA MZIGO WA LAWAMA....!

JWTZ msirudi nyuma kwa kelele za chura.....!


MAHESABU hujapiga vizuri hesabu zako, ina maana mtu akichokozwa kwenye pombe, aende kikosini na kuleta askari wapige na kuumiza watu mtaa mzima? akiibiwa mjeshi mmoja ni haki kikosi kizima kuja kupiga watu mtaa mzima ambao hawana hatia? askari gari lake likikwaruzwa basi aliyemkwaruza ni lazima apigwe?

Kwa nini wasiende polisi? Hawajui sheria? Mimi huwa nawaona hata barabarani wakiwa kwenye magari yao hawataki kufuata sheria za barabarani, watalazimisha kupita hata upande ambao haupitiki.

Nchi hii ina sheria na utawala sasa sidhani kama wao wanahaki ya kujichukulia sheria mkononi kama bwana MAHESABU unavyotaka ihalalishwe.
 
nimewahi kuwa askari ndani ya JWTZ kabla ya kukimbia, kuna ujinga mmoja askari wote wanao kujiona wao ni untouchable, wasioguika ,wasiohojika, kwamba hata rais wa jamuhuri anawaogopa, wanakiburi wajivuni, wanafanya upuuzi mwingi ambao hausemwi , magazeti na vyombo vingi vya habari huogopa kuripoti upuuzi ndani ya JWTZ, angalau siku hizi kunakujiminim kidogo...na hali imekua mbaya zaidi tangu kamanda Waitara aondoke.
 
Waitara alikuwa mwanajeshi wa shoka, nidhamu jeshini iliyoaribiwa na Mboma na wenzie ilikrudi, kwa kweli hio kupiga watu ni ujinga na mob saikoloji tu, hakuna chocghote hapo cha maana
 
nimewahi kuwa askari ndani ya JWTZ kabla ya kukimbia, kuna ujinga mmoja askari wote wanao kujiona wao ni untouchable, wasioguika ,wasiohojika, kwamba hata rais wa jamuhuri anawaogopa, wanakiburi wajivuni, wanafanya upuuzi mwingi ambao hausemwi , magazeti na vyombo vingi vya habari huogopa kuripoti upuuzi ndani ya JWTZ, angalau siku hizi kunakujiminim kidogo...na hali imekua mbaya zaidi tangu kamanda Waitara aondoke.


Nguvumali upo sahihikabisa, wanajeshi wengi wanahiyo dhana, kwamba wao hata rais anawaogopa kwa hiyo wanaweza fanya chochote kile
 
Sikonge, uko deep sana...
kuna siku niliuliza hizi kambi vipi??? nikajibiwa jibu sahihi mno... hivi yupi alianza kambi au watu???

Kama ni kambi basi ni sisi kuson=gea mbali... na kama ni sisi basi kambi zivunjwe

KAZI KWETU

Jeshi siyo WATU/RAIA. Jeshi ni chombo cha serikali. Ndiyo maana utasikia mtu akisema nilikuwa jeshini na nimeacha. Kwa maana hiyo, jeshi kama chombo cha Serikali kinaweza kuhamishwa kwa ridhaa za serikali.

Nakumbuka miaka ya 70 katikati nikiwa mdogo sana tulikwenda kumtembelea rafiki yake sister aliyekuwa mwalimu wa UDSM. Kufika kwake huwezi amini vinyani vilikuwa vinakuja hadi kwenye mlango wa nyumba na kwa sababu ulikuwa wa vioo, tulikuwa tunaviona. Sasa hivi UDSM ni mjini kabisa. Hizo kambo nazo zilikuwa msituni ila sasa ziko mjini. Hapa wangelipabadilisha na kuwaweka Maafisa wa jeshi tu na hawa wenye Vumilia Vumbi Vichakani wapelekwe mbaali kabisa na mji na huko lichukuliwe eneo kubwa sana wapewe huko na watu wasiruhusiwe kujenga ndani ya eneo lao. Hii itasaidia hata mabomu yao yakianza kulipuka, basi miji ya watu inakuwa mbali na misuguano inapungua kwani kwenye miji midogo watu wanafahamiana kiasi hata wanajeshi wenyewe wanafahamiana na raia na hata kuoleana.
 
Waitara alikuwa mwanajeshi wa shoka, nidhamu jeshini iliyoaribiwa na Mboma na wenzie ilikrudi, kwa kweli hio kupiga watu ni ujinga na mob saikoloji tu, hakuna chocghote hapo cha maana

..huyu mwamunyange amewekwa kwa kuwa ni rafiki sana wa JK....lakini ni ana sifa kama za JK..Za kupenda mabibi...anatakiwa kuwa mkali zaidi..pamoja na kuwa si rahisi sana kusema tukio lisiwatokee askari kwani wao ni binadamu na wanachokozwa...mara nyingi sana matukio ya askari kupiga raia ..wao ndio huaza kuchokozwa..sasa tatizo askari jeshi...kipigo chao ni tofauti na polisi..WANAJESHI WAMEFUNDISHWA KUPIGA KWA MINAJILI YA KUUWA....wamefundishwa kupiga maeneo ya mwili ambayo kipigo kimoja tu kinatosha kukuuwa....no second chance ..wanaamini hivyo.....POLISI WANAFUNDISWA KUPIGA MAENEO YA KUJERUHI ..ili kutuliza...so next time you https://jamii.app/JFUserGuide with askari jeshi usikubali kusimama naye ngumi au akuguse anaweza kukusababishia tatizo kubwa...au kifo........

..PIA jeshi ni MNADHIMU ...huyu ndio mkuu wa utawala ..inabidi awe strong na asiwe na utani kabisa...namkumbuka mnadhimu kama SAYORE he was very strict.....inabidi SHIMBO naye awe mkali sana...,mkuu wa utumishi jeshini naye ameletwa pale kirafiki..alikuwa mkuu wa mkoa wa arusha kanali ndomba ..alimpandisha cheo akampa u bregadia jenerali..na kumpeleka jeshini kuwa mkuu wa utumishi...miaka zaidi ya 12 baada ya kuwa nje ya utumishi wa jeshi!!!
 
Dawa sasa ni kutembea tu na 'chamoto', mtu akikuletea za kuleta unampa za uso fastafasta, tuone huo uanajeshi kama utamsaidia kukwepa risasi.
 
..........Hebu waangalie kwanza sura zao, hawana hata haya kumuondolea maisha kijana wa watu. Muangalie kwanza huyo mama, mwanamke mzima kujihusisha kumpiga kaka wa watu.........hana hata uchungu wa kike, wanawake tu watu wa huruma sijui wewe ni mwanamke wa jinsi gani? Na mfungwe maisha nyie msiokuwa na utu wa kibinadamu.
 
Huyo jamaa mbona kama anacheka kwenye hiyo picha? Au anadhani tuhuma dhidi ni mchezo....
 
Tatizo bongo hatuna wanaharakati wa kweli. Hiki kipondo cha jamaa kingetokea Marekani kwa mfano, ungeona tayari watu washaandamana na kubeba mabango Pentagon. Na wish tungekuwa na kina Al Sharpton wetu....
 
Jamani sasa tunamdharau rais ... hii ishu inakuwa handled na KOVA na wenzake ....Watuhumiwa wapo ndani,mmoja anatafutwa..............sasa rais hapo ana sababu gani ya kutoa statement ...wakati watendaji wake wapo?


Sawa watendaji wapo lakini inasaidia nini kwa wafiwa wakati wameisha poteza ndugu yaho? Tunyamaze tuu kwa sababu watendaji wapo? Mimi ninachosema ni kwamba hii tabia haija anza leo, na huyu ndugu is not the first one to die due to this nonsense. Kwa kifupi haya mambo yamezidi, JK kama Raisi akemee hii kitu as it’s obvious that hao watendaji wake are not doing what they are suppose to be doing otherwise huyu ndugu asingepoteza maisha namna hii.
 
halafu watu wenyewe ukiwaona huwezi amini wamemtandika mtu hadi akafa... au alikuwa na matatizo mengine ya kiafya?
 
..........hebu waangalie kwanza sura zao, hawana hata haya kumuondolea maisha kijana wa watu. Muangalie kwanza huyo mama, mwanamke mzima kujihusisha kumpiga kaka wa watu.........hana hata uchungu wa kike, wanawake tu watu wa huruma sijui wewe ni mwanamke wa jinsi gani? Na mfungwe maisha nyie msiokuwa na utu wa kibinadamu.

mambo yanazidi kusanuka. Waliompiga swetu hadi kufa hawakuwa wanandoa. Mwanamke ni mke wa mtu na alimuaga mmeo kwamba anakwenda morogoro kikazi kwa siku 7 kumbe alikuwa dar anajivinjari na hawala yake. Mwanamke anaishi bunju na mme wake. Hii ni adhabu kutoka kwa sir.god. Wanajf, oneni jinsi mambo yalivyo, ungekuwa wewe ndiye mme wa huyo mwanamke katika mazingira kama hayo ungefanyaje?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom