Kifo cha SHARO, Ni msiba wa Mzee Majuto

Miwatamu

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
1,450
487
Yawezekana kwa mawazo mepesi kutokana na kichwa cha habari hapo juu mtu akahisi kuwa msiba wa kuondokewa na kipenzi chetu katika tasnia ya sanaa Ndugu yetu; Sharo Millionea hautuhusu sisi sote. Ukweli ni kuwa unatuhusu tena kwa karibu zaidi kutokana na jinsi kijana alivyokuwa anajitahidi kubuni bila kuiga mambo mengi katika fani yake hiyo. Sharo amevuma sana kila kona na kufanya hata watoto wetu kumweka mbele zaidi katika maongezi yao na hata kutumia baadhi ya misemo yake.
Lakini nasema kuwa ni msiba wa Mzee Majuto kutokana na ukweli kuwa katika wasanii tulionao hapa nchini ambao wameweza kupatana na kufanya vitu ambavyo vinaonekana kama vinafanywa na mtu mmoja, basi ni hawa watu wawili. Nasema hivyo kutokana na ukweli kuwa Sharo na Majuto ni wasanii pekee ambao wameweza kubuni mitindo mbalimbali ambayo haina athari zaidi ya faida kwa jamii, lakini vilevile ni watu ambao hawakuwa na habari za kuchefua katika jamii kama tunavyowaona baadhi yao wale walio katika tasnia hii.
Nina hakika majuto kama hatostaafu kazi hii ya sanaa baada ya kifo hiki, basi itamchukua muda sana kupata mbadala wa Sharo ili kumrudisha ulingoni.

R.I.P Sharo.
 
Ni kweli meeeen,sharo kachangia sana kung'arisha nyota ya majuto iliyokuwa imeanza kufifia, ooooh mamaaaa!?
 
Kweli Duniani tunapita tu. Ndo kwanza alianza kuvuma na kila siku nilikua nikisubiri nimuone atatoka na kipi mara eti hatunae tena! !!!!

Pumzika kwa amani kaka cse no way out.
 
Ni kweli tutamisi nilikuwa nayapenda yale matangazo yake ya airtel na hili jipya lilianza kurushwa hivi karibuni la "kule hakusomeki meen, nimehamia............." nashagaa kwa nini wameyatoa mbiombio au ndio mkataba tena maana mwenyewe hayupo? Kweli uhai hausomeki, tuhamie kwa Mwenyezi Mungu na ni vema kutenga Kutenga muda wa kumshukuru Mungu kwa kuwa Uhai wetu u mikononi mwake.................. panga yote mabaya kwa mema, ukaloge, ukaibe, na yote yachukizayo lakini mwisho wa siku maisha ni kama mshumaa uwakao kama si upepo kuuzima unayeyuka na kwisha.......... ya nini kusumbuka na dunia, ya nini kutendeana vibaya, ya nini kuchukiana na kugombania madaraka ya nini ....................... na ya nini yote haya sina jibu.

Mungu turehemu..............

Pumzika kwa amani Sharo.
 
Yawezekana kwa mawazo mepesi kutokana na kichwa cha habari hapo juu mtu akahisi kuwa msiba wa kuondokewa na kipenzi chetu katika tasnia ya sanaa Ndugu yetu; Sharo Millionea hautuhusu sisi sote. Ukweli ni kuwa unatuhusu tena kwa karibu zaidi kutokana na jinsi kijana alivyokuwa anajitahidi kubuni bila kuiga mambo mengi katika fani yake hiyo. Sharo amevuma sana kila kona na kufanya hata watoto wetu kumweka mbele zaidi katika maongezi yao na hata kutumia baadhi ya misemo yake.
Lakini nasema kuwa ni msiba wa Mzee Majuto kutokana na ukweli kuwa katika wasanii tulionao hapa nchini ambao wameweza kupatana na kufanya vitu ambavyo vinaonekana kama vinafanywa na mtu mmoja, basi ni hawa watu wawili. Nasema hivyo kutokana na ukweli kuwa Sharo na Majuto ni wasanii pekee ambao wameweza kubuni mitindo mbalimbali ambayo haina athari zaidi ya faida kwa jamii, lakini vilevile ni watu ambao hawakuwa na habari za kuchefua katika jamii kama tunavyowaona baadhi yao wale walio katika tasnia hii.
Nina hakika majuto kama hatostaafu kazi hii ya sanaa baada ya kifo hiki, basi itamchukua muda sana kupata mbadala wa Sharo ili kumrudisha ulingoni.

R.I.P Sharo.

Its true...R.I.P SHARO!!!!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom