Miwatamu
JF-Expert Member
- Oct 2, 2012
- 1,450
- 487
Yawezekana kwa mawazo mepesi kutokana na kichwa cha habari hapo juu mtu akahisi kuwa msiba wa kuondokewa na kipenzi chetu katika tasnia ya sanaa Ndugu yetu; Sharo Millionea hautuhusu sisi sote. Ukweli ni kuwa unatuhusu tena kwa karibu zaidi kutokana na jinsi kijana alivyokuwa anajitahidi kubuni bila kuiga mambo mengi katika fani yake hiyo. Sharo amevuma sana kila kona na kufanya hata watoto wetu kumweka mbele zaidi katika maongezi yao na hata kutumia baadhi ya misemo yake.
Lakini nasema kuwa ni msiba wa Mzee Majuto kutokana na ukweli kuwa katika wasanii tulionao hapa nchini ambao wameweza kupatana na kufanya vitu ambavyo vinaonekana kama vinafanywa na mtu mmoja, basi ni hawa watu wawili. Nasema hivyo kutokana na ukweli kuwa Sharo na Majuto ni wasanii pekee ambao wameweza kubuni mitindo mbalimbali ambayo haina athari zaidi ya faida kwa jamii, lakini vilevile ni watu ambao hawakuwa na habari za kuchefua katika jamii kama tunavyowaona baadhi yao wale walio katika tasnia hii.
Nina hakika majuto kama hatostaafu kazi hii ya sanaa baada ya kifo hiki, basi itamchukua muda sana kupata mbadala wa Sharo ili kumrudisha ulingoni.
R.I.P Sharo.