Kifo cha Regia na harakati za mageuzi Tanzania.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifo cha Regia na harakati za mageuzi Tanzania..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAGEUZI KWELI, Jan 18, 2012.

 1. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Watanzania tumeumia na tumelia sana kwa kifo cha dada yetu Mpambanaji wa kweli Regia Mtema.Haina shaka kwamba alikuwa ni kipenzi cha wengi hasa kwa kipindi hiki kifupi alichokuwa Bungeni.
  Amefariki na Mungu ndiye mpanga yote..Tunamshukuru Mungu kwa kila Jambo.

  Nini alichoacha kwa watanzania wa sasa?? Ukiangalia waliopokea taarifa za kifo chake na waliokusanyika kuanzia nyumbani kwake Tabata Chang'ombe mpaka Karimjee na hatimaye waliompokea Ifakara, Tukubali tusikubali kila mtanzania amesikia Vijana na wanaotaka mageuzi walivyosikitika kwa msiba huo.
  Chadema kimekuja juu sana hasa kitaifa ni Gumzo juu ya Chadema na Kifo cha Mbunge wake.

  Regia amekutanisha Serikali na wapinzani, Regia alikuwa na Kura zaidi ya alfu 30 jimboni kwake kama mgombea Ubunge, Regia ameacha Changamoto kwa Chadema na namna ya kutumia hekima katika kuziba pengo lake ndani ya Bunge.

  Maoni yako kwa Chadema hapa ni nini?? Kama si mshabiki wa Mageuzi tupe nafasi kidogo..
   
Loading...