Kifo cha Rais Magufuli kitasababisha walioomba ukimbizi nje kurudishwa Tanzania

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,975
Baada ya muda mfupi tutaanza kuwaona wale wote waliomba ''ukimbizi wa kisiasa'' nje ya nchi hasa Ulaya na Marekani kuanza kurudishwa kwa nguvu nchini.

Ukimbizi wa kisiasa una misingi yake na kwa sasa msingi kwa wakimbizi kutoka Tanzania ni madai kuwa wanakimbia nchi kwa sababu maisha yao yako hatarini kutokana na utawala wa Rais Magufuli. Ninajua kuna watanzania wengine wametumia dhana ya ''ukimbizi wa kisiasa'' wakati ukweli ni wakimbizi wa kiuchumi!

Mtu yeyote anapoomba ukimbizi wa kisiasa katika nchi za Ulaya na Marekani, kwanza anapokelewa na kupewa hifadhi ya muda halafu baadaye anatafutiwa sehemu ya kuishi wakati madai yake yakiwa yanafanyiwa kazi kuhakikisha ukweli wa madai yake.

Mchakato wa kupata ukweli huchukua muda mrefu hata miaka kulingana uwingi/mrundikano wa kesi za ukimbizi.

Hatari iliyopo kwa wakimbizi wa kisiasa ni kuwa, kama muda wa kesi yao ukifika na kukuta hali ya kisiasa waliyokuwa wanadai kuikimbia imebadilika basi hawawezi kupewa hifadhi ya kudumu bali huamuliwa kurudi walikotoka kwa sababu ni salama.

Kwa mfano, wale wakimbizi wa kisiasa kutoka Tanzania waliodai wanakimbia utawala wa Rais Magufuli hawawezi kwa sasa kupewa ukimbizi wa kudumu kwa sababu waliyekuwa wanamkimbia ameishaondoka madarakani. Kwa maana nyingine, kesi/madai yao yamekufa automatically.

Tusishangae baada ya muda mfupi tutawaona wale wote waliokimbia nchi kwa madai ya utawala wa Rais Magufuli wakirudishwa nchini kwa hiari yao au kwa nguvu.

Wazungu pia wana kanuni yao ambapo wanaweza kukutumia kwa jambo fulani na wakifanikisha tu wanaachana na wewe (wanakutelekeza). Kama kuna watanzania waliotumiwa kisiasa na wazungu katika kukabiliana na Rais Magufuli nao wajiandae kuachwa bila msaada au kurudishwa nchini kwa sababu malengo ya wazungu yatakuwa ''yametimia''. Ile dhana ya ''toilet paper'' hutumiwa sana na wazungu!

Kwa watu wenye uelewa wanapoona baadhi ya wale walioomba ukimbizi wa kisiasa nje ya nchi bado wanaendelea kupambana na Marehemu Rais Magufuli kwenye mitandao ya kijamii (twitter, facebook na Instagram) wanajua kuwa wanachotafuta ni ushahidi wa kuonyesha kuwa hata baada ya kifo cha Rais Magufuli bado maisha yao yako hatarini kwa sababu kuna baadhi ya watu wanaendelea kutoa vitisho kwenye account zao (twitter, facebook na Instagram).

Bila kuonyesha kuwa maisha yao bado yako hatarini, kesi/madai yao ya kuomba ''ukimbizi wa kisiasa'' yatakuwa yamekufa automatically!

Siasa za ukimbizi zina gharama zake na moja ya gharama ya ''ukimbizi wa kisiasa'' ni kubadilika kwa hali ya kisiasa katika nchi uliyoikimbia!
 
Ngoja nikusaidie unapoomba ukimbizi wa kisiasa hauombi eti sababu awamu fulani au mtu fulani ndio tishio!

Bali tishio la usalama wako likiendelea kuwepo utaendelea kuishi huko hata miaka na miaka na kanuni za kimataifa ziko wazi! Hao jamaa walikimbia kulinda uhai wao Magufuli alikua kama ndio kibwagizo ila waliokua na nia mbaya kwao bado wapo.

Nikuulize tu kwani Iddi Amin aliishi uhamishoni toka 1979 hadi mauti yake 2003 na aliishi nchi tatu tofauti kwa kuhamahama kwanini hujiulizi hawakumwabia sasa utawala mwingine umeingia rudi kwenu?
 
Mtakatifu wenu keshaanza kuumbuliwa kwamba mambo yalikuwa yanaendeshwa kwa maigizo na uongo mtupu.

Time will tell, acha mambo yaendelee kuwekwa hadharani.
Neno ''kuumbuliwa'' ni dhana katika fikra zako ambayo siwezi kukusaidia kuiondoa!

Kuicheza ngoma ya CCM ndio sehemu ya siasa za Tanzania!
 
Mtakatifu wenu keshaanza kuumbuliwa kwamba mambo yalikuwa yanaendeshwa kwa maigizo na uongo mtupu.

Time will tell, acha mambo yaendelee kuwekwa hadharani.
Ameumbuliwa na nani? Kutoka chama kipi?

Mbona mnakuwa wajinga?
 
Belgiji hawezi kurudi maana amsterdam anamnogesha sana kule!

Si umesikia ametoa masharti mapya ya kurudi? Kwamba lazima aruhusiwe kuanika maovu ya JPM? Kana kwamba sasa hivi kuna mtu kamzuia,
.
Hii yote ni janja yabkuendelea kubaki na amsterdam
 
Ujinga ni hilo swali, "kutoka chama kipi"
Kwani kwa akili yako kile kiburi, uongo, ukatili, kukosa hekima alikuwa anawakilisha ccm au ilikuwa hulka yake
Mtajikanyaga sana mwaka huu!

Kwa hiyo Samia anamuumbua Magufuli maana alikuwa anafanya kwa hulka zake?
 
Ngoja nikusaidie unapoomba ukimbizi wa kisiasa hauombi eti sababu awamu fulani au mtu fulani ndio tishio!

Bali tishio la usalama wako likiendelea kuwepo utaendelea kuishi huko hata miaka na miaka na kanuni za kimataifa ziko wazi! Hao jamaa walikimbia kulinda uhai wao Magufuli alikua kama ndio kibwagizo ila waliokua na nia mbaya kwao bado wapo.

Nikuulize tu kwani Iddi Amin aliishi uhamishoni toka 1979 hadi mauti yake 2003 na aliishi nchi tatu tofauti kwa kuhamahama kwanini hujiulizi hawakumwabia sasa utawala mwingine umeingia rudi kwenu?
WAMEKMBIA HALI NGUMU YA MAISHA, NA NDIYO MAANA WANABWABWAJA SANA ILI WAPEWE HURUMA....SIASA WAJINGA NDIYO WALIWAO....
 
Back
Top Bottom