Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,552
Nairobi, Kenya. Kiongozi mkuu wa chama cha National Super Alliance (Nasa), Raila Odinga amesema atakaa mezani kujadiliana na Rais Uhuru Kenyatta kwa sharti kwamba uchaguzi mpya uandaliwe katika muda wa siku 90 na si vinginevyo.
Odinga ameshikilia kwa kuwa Kenyatta alikataa kufanya mazungumzo kabla ya uchaguzi wa marudio wa Alhamisi iliyopita basi kilichosalia ni hicho.
Akizungumza katika mahojiano na shirika la CCN Ijumaa, Odinga alisema hata kama Rais Kenyatta atatangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo wa marudio, kiongozi huyo wa Jubilee hatapata urahisi kuongoza Kenya.
Badala yake amemshauri Kenyatta kujiuzulu kwa sababu ya “idadi ndogo” ya wapigakura waliojitokeza. Alisema uchaguzi ule ilikuwa “kura ya kutokuwa na Imani.”
Alipoulizwa ikiwa mpango wake wa kuanzisha harakati za upinzani kitaifa ilikuwa njia ya kuiswaga serikali ya Kenyatta ijielekeze kumwaga damu, Odinga alisema shughuli ambazo chama hicho kinapanga kutekeleza zimebainishwa ndani ya Katiba.
“Kama unavyojua, Katiba yetu inaruhusu kuweka vigingi, kugoma, maandamano ya amani, kupinga, kususia na mengineyo. Kwa hiyo, tuna njia kadhaa mbadala ambazo ni halali na zipo Kikatiba, ambazo tutazitumia kuongeza shinikizo dhidi ya serikali hii,” alisema.
Maswali:
CNN: Nini kitatokea wiki ijayo matokeo yatakapokuwa yamejumlishwa, matokeo hayo yote yatakapokuwa yametangazwa? Mwelekeo ni kwamba yatampa ushindi wa urais Kenyatta kwa sababu ninyi mmesusa.
Je, wewe na wafuasi wako mtakuwa na nini cha kusema?
Odinga: Huu ni uzandiki kwa sababu, kimsingi umefungua mfuniko kwenye kopo wa kile ambacho Kenyatta amekuwa akidai; kwa sababu ni asilimia 25 tu ya wapigakura ndio walijitokeza Alhamisi.
Hivi sasa wanapika namba ili idadi iongezeke. Lakini kwa mujibu wa mfumo wa KIEMS, uliotumika kutambua wapigakura, waliojitokeza walikuwa 3.5 tu. Idadi hiyo ni asilimia 20 ya waliojiandikisha.
Kimsingi matokeo haya yanathibitisha kwamba watu hawana Imani. Ni kura ya kutokuwa na Imani na serikali ya Rais Kenyatta. Ba endapo ningekuwa mimi, na ninajua demokrasia ilivyo ningejiuzulu au kung’atuka.
CNN: Ikiwa hilo halitatokea na tayari atakuwa ametangazwa rais tena, je wewe na wafuasi wako mtachukua hatua gani? Je, Kenya itaonekana vipi wiki ijayo katika wiki ambayo matokeo yatatangazwa?
Odinga: Tumesema kwamba Katiba yetu, ibara ya kwanza inasema kwamba ikiwa serikali itajitangaza yenyewe kwa watu, basi watu wana haki ya kufanya uamuzi.
Watu watakuwa na haki ya kutotii amri kutoka serikali ya namna hiyo.
CNN: Je, unatarajia kushuhudia maandamano zaidi na machafuko zaidi?
Odinga: Hapana. Hatutaanzisha machafuko kukabiliana na serikali. Tutafanya migomo wala si kwa maandamano bali kwa njia nyingine ambazo tutatangaza Jumatatu.
Tutatangaza mfululizo wa hatua za kuchukua ili kuishinikiza serikali hii kuondoka.