Kifo cha mwenyekiti wa CHADEMA Usa river-Arumeru - Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifo cha mwenyekiti wa CHADEMA Usa river-Arumeru - Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tpmazembe, May 4, 2012.

 1. t

  tpmazembe JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 2,474
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  NIMEJARIBU KUTAFAKARI KIFO HICHI NIMEPITA PICHA HALISI YA SIASA ZA TZ BAADHI NI:-
  • Watanzania tuna siasa za chuki na za kulipana kisasi ,hii ni kutokana na tulivoiweka siasa maana unakuta uchaguzi mdogo mgombea mmoja bajeti anayotumia inakaribia mil 600,ukijiuliza kazitoa wapi?,atazilipaje? hupati jibu,Kutokea yaliyotokea inakuwa kitu cha kawaida maana anayeshindwa anayeruhiwa vibaya sana kiuchumi.
  • VYAMA VYETU TUNAVYOVISHABIKIA VIKO KIMASLAHI ZAIDI HAVIJALI WATU WAKE:-Angalia Mwenyekiti amekufa chadema kama chadema wametuma tu wabunge wawili wamezika hakuna kinachoendelea,hatujasikia kama wameunda timu kuchunguza mauaji au kutoa onyo kwa serikali ,wako kimya,SASA VYAMA VYA SIASA KAMA CDM kuna umuhimu gani kushabikia.wakati viongozi hawa value watu.
   
 2. t

  tpmazembe JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 2,474
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Mimi ni cdm damu,lakini sasa naweza kukaa pembeni kama mambo yatachukuliwa kinyemela namna hii
   
 3. n

  ngaranumbe Senior Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapana, CHADEMA wako makini kabisa na fuatilia vyombo mbalix2 vya habari; Mbowe alisema CHADEMA wako mbioni kutoa tamko. Mtoa mada subiri, hakuna papara wala udhaifu mzee, kifo kinauma hasa katika mazingira yale.
   
 4. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Mi cdm damu,ukisema 2chunguze utakuwa unaingilia kazi ya polisi..2silaumu chama.
   
 5. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwani polisi wangetaka siwangewajumuisha CDM kwenye huo uchunguzi? Nakuhakikishia CDM hawana dola kwa hiyo wanachokijua kuhusu hicho kisa usishangae kukandamizwa na dola. Ila kaa pembeni kama huelewi vitani kuna majeruhi na wahanga.
   
 6. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Nani anae value watu,CCm walioua au CDM iliyopeleka wabunge?
   
 7. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  WEWE HUKUSOMA MAJUZI TU CHADEMA WAMESEMA WANAIPELEKA SERIKALI MAHAKAMANI KWA MAUAJI YA WANACHAMA WAKE? SIKUMBUKI NI MAGAZETI YA LINI LKN KAMA SIYO WIKI HII NI MWISHONI MWA WIKI JANA. Nafikiri siyo vema kulaumu CDM wakati bado Polisi wanaendelea na Uchunuzi.
   
 8. CHIETH

  CHIETH Senior Member

  #8
  May 4, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna maana kujiita CDM damu wakati huwezi kujibu hoja ya mleta mada. Sote tulisikia yaliyosemwa siku ya mazishi ya mwenyekiti sasa unataka nini. Wewe ondoka tu maana CDM inaundwa na wanaojitolea kwa hali na mali hata maisha pia. Kumbuka watu wengi sana wamekufa hapa dunia wakidai haki ambao mimi na wewe tunajivunia. Soma alama na historia ya dunia. Shame on you.
   
 9. m

  mawazohai New Member

  #9
  May 4, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe si mfuatiliaji wa hoja hii. Ni mara ngapi Mwenyekiti kalitolea maneno makali jambo hili? Au kuna cha ziada unataka kukileta.
   
 10. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Mtoa mada hujui mtiririko wa Idara ya John mnyika,juzi alilitolea ufafanuzi..pengine wewe ni gamba.
   
 11. M

  Malipo kwamungu JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 574
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
   
 12. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  kile kifo kinaumiza sana jamani
   
 13. Vato

  Vato JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2012
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33

  hakusema mchunguze, kasema yeye kama raia hajaona ni kwa kiasi gani CHADEMA imelichukulia swala hilo katika uzito unaolipasa...yule jamaa alikufa kwasababu ya CHADEMA, alichangia kwa kiasi kikubwa Nasari kushind katika kata yake, ni mtu muhimu lakini je, kweli msiba ule ulikuwa wa kutuma wabunge wawwili kama mtoa mada anavyosema??????? labda katika kuelimisha na kuutarifu umma ni kwa kiasi gani CHADEMA inawajali wanachama/ makamanda wake wanaopatwa na mambo mabaya katika harakatin za wao kukitumikia chama hebu tuwekeeni mifano CHADEMA imesimama vipi katika kushughuilikia ile kesi nya mauaji ya kamanda aliyetoka Ubungo kwenda Igunga kama wakala...wakati wa uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga baada ya Rostam kung'atuka.
   
 14. Vato

  Vato JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2012
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  1. Sio kila mtu alimsikia Mnyika, so ulichopaswa kusema ni kumwambia mtoa mada Mnyika aliongea nini wakati analitolea jambo ufafanuzi
  2. Ni UJINGA uliokomaa kudhani kila anyetofautiana na wewe kimtazamo au kuhoji baadhi ya mambo ya CHADEMA ni Gamba..ni fikra mgando, njia nzuri moja wapo ya kukijenga chama ni KUKIKOSOA kwa kutoa constructive cricisms...usidhani kukisifia chama siku zote ndio upenzi wa chama, huo sio upenzi ni ushabiki na unafiki..
   
 15. m

  maweni Member

  #15
  May 4, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 96
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Polepole, utakuwa upo kijijini na hujui nini kinaendelea duniani. Ulofa wako usiuexpose kwa jamii erevu. Pole mdau mzembe!
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  May 4, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Nikisema mtoa mada ni Mpumbavu wengine watasema nimemwonea! Basi wacha nisisema hivyo.
  Kwanza kabisa wewe si mwanachadema ndiyo maana hujui nini kiliendelea.
  Pili hujui utaratibu wa uwakilishi wa chama au taasisi kwenye mazishi.
  Tatu hujui taratibu za kutoa tamko. Chama makini lazima itafakari, ifanye uchunguzi wa tukio siyo kukurupuka kama wewe unavyotaka.
  Vile vile nchi hii kuna taratibu za kisheria, ambayo uchunguzi wa tukio unafanywa na idara ya upelelezi. CDM kuingilia uchunguzi wa jeshi la polisi ni kukiuka taratibu za upelelezi, lakini inaweza kufanya uchunguzi wake kimya kimya then inakuja na conclusion.

  Wewe siyo CHADEMA
   
 17. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #17
  May 4, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
   
 18. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,835
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Kazi ya Kukulinda wewe, na mimi na mwingineyo yeyote katika jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kazi ya Serekali iliyopo madarakani, na kama serekali imeshindwa kuwalinda wananchi wake inasubiri Matamko ya wana siasa Ujue Kuna Tatizo Kubwa sana!! Unless ututhibitishie Kuwa Jeshi la polisi Linafanya kazi yake kwa shinikizo la wanasiasa.
  Ila pia Ujue wauwaji wameshafanya Uhalifu wao (Na Mungu awalaani) Kitendo cha CDM kutuma mwakilishi naona ni sawa Kabisa ila Ningeomba lile Wazo la wanachama Kuchangia Hela Kwa Ajili ya Kuwasemesha Watoto Waliobaki Hai Lizingatiwe!! Hata kwa Michango ya wanachama
   
 19. k

  kansiana Member

  #19
  May 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli ni suala la subira, bado wako makini lakini masuala ya jamii/ watu wengi yanahitaji takwimu/ bird watching/ busara/ hekima kuja kwenye mrejesho na hatimaye maamuzi magumu. Lets give ourselves time!:clap2:
   
 20. t

  tpmazembe JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 2,474
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  CCM NI CHAMA KICHAFU NA KISICHOKUWA NA TIJA KWA SASA KWA TAIFA LA TANZANIA,MIMI NI MWANA CDM KWA KUWA NAPENDA MABADILIKO,ccm wanajulikana ni malaika waliofukuzwa mbinguni kwa jeuri na sasa waiihamishia hiyo jeuri dunia na adhabu yao iko wazi ni moto wa milele, lakini cdm ningetegemea wafanye mambo katika hali ya tofauti kidogo LAKINI katika hili CDM wamechukulia juu juu sana,Polisi wahawezi chunguza chochote,ilitakiwa iundwe timu ya cdm viongozi wakuu kama slaa wangeweka kambi arumeru walau kwa wiki moja lakini hilo halijatokea na sasa kila mtu kasahau
   
Loading...