Kifo cha Mwangosi: Sasa uhusiano wa polisi na wananchi ni wa mashaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifo cha Mwangosi: Sasa uhusiano wa polisi na wananchi ni wa mashaka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by tenende, Sep 22, 2012.

 1. t

  tenende JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Jana nilitembelea katika kijiji cha MBOGA, kata ya MSOGA kufuatilia siasa za vijijini zinavyoendeshwa na CHADEMA mkoani Pwani. Mkutano huo ulianza saa 9 alasiri na kuhudhuriwa na watu wapatao 115 hivi waliokuwa wakiongezeka kadri muda ulivyokuwa unaenda. Nikiwa katika eneo la mkutano nilishtuka saana kuona wananchi wakikimbia na kupiga kelele "wababe wa Mwangosi haoo!" .. Tafrani hii ilichochewa na MTENDAJI kata wa MSOGA Bwana MTAMANI alipowapigia polisi simu kuwaeleza kuwa CDM wanafanya mkutano bila kibali. Kimbia kimbia ilitokea baada ya kuona OCS wa Chalinze na ujumbe wa askari 10 (wengine wakiwa na silaha walioongozana naye wakiusogelea mkutano. ........Hali hii ilimpa wakati ngumu Mwenyekiti wa CDM jimbo la CHALINZE Bw. Torongey (alipokuwa anahutubia), kupaaza sauti kwa wananchi kuwa "hawa siyo wa Iringa, njooni tuendelee na mkutano!" Baada ya kuona hivyo OCS akaamua kufanya haraka kazi aliyojia na kuondoka. OCS alieleza kuwa amepigiwa simu na mtendaji kata aitwaye MTAMANI kuwa mkutano wa chadema unafanyika bila kibali. .......Viongozi wa CDM wakatoa nakala yao ya ratiba na barua ya polisi kisha OCS akaondoka na ujumbe wake. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, baada ya tukio hilo hata wale waliokuwa mbali awali wakajaa mkutanoni. Mikutano hii inaendelea kijiji kwa kijiji.
   
 2. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kwa kifupi CDM imeishaingia ndani ya mioyo ya watu
   
 3. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  natamani kuona jeshi hili linavunjwa na kamanda kamhanda anapigwa mvua 30
   
 4. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  dah!!! hizi sio dalili nzuri hata kidogo kwa hiki chombo cha dola ambacho kinahubiri ulinzi shirikishi mchana na usiku. halafu kama jeshi la polisi lingefanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na jinsi inavyoonyeshwa kwenye mission na vision statements hakyanani hali ya usalama wetu raia wa tanzania ingekuwa nzuri sana. kwa kifupi hizi ni dalili za kushindwa kwa jeshi la polisi Tanzania.
   
Loading...