Kifo cha Mustafa Kamal Ataturk(Laana za Allah zimshukie)


S

said Nundu JR

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2016
Messages
306
Likes
155
Points
60
S

said Nundu JR

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2016
306 155 60
*KIFO CHA MUSTAFA KAMAL ATATURK (Laana za Allah Zimshukie)*

Mustafa Kamal ataturk ni raisi wa kwanza wa Uturuki, atakumbukwa kuungana na dola za kikafiri Uengereza na Ufaransa kuivunja dola ya kiislamu ya Khilafah tarehe 3 Machi 1924 , na kuigawanya dola hiyo vijinchi vidogo vidogo na kuweka vibaraka wao katika uongozi ili kuongoza kwa maslahi yao. Mmoja wa vibaraka wao akawa ni huyu Mustafa kamal aliyenzisha taifa jipya na kuliita Turkey.

Baada ya Kuivunja dola ya kiislamu, Mustafa Kamal akapiga marufuku dini ya kiislamu nchini humo kama dini ya taifa hilo na kusema dini itenganishwe na maisha ya kawaida, na kupiga marufuku Lugha ya kiiarabu, kuadhiniwa kuadhiniwe kituruki, Quran ichapishwe kituruki, kalenda ya kiislamu ikatupiliwa mbali, wanaume wasivae kofia za kiislamu wavae za kimagharibi na tembo kuwa halali na baadhi ya misikiti kufungwa kama msikiti mkubwa wa Aya Sophia kufanywa makavazi.

Mwaka 1938, Mustafa kamal alianza kuuguwa ugonjwa wa maini uliyosababishwa na kunywa tembo kwa wingi, akawa anaugua akiwa kitandani katika kasri lake, Allah SWT Akamzidishia magonjwa ya kila aina hadi mwili wake mzima ukawa unawashwa kila mahali na kuhisi joto la ajabu mwilini.

Alikuwa akihisi mwili kushika moto hadi kupiga makelele mpaka kasri nzima inasikika kelele zake, Siku moja aliamrisha apelekwe katikati ya bahari ili apiwe na upepo wa bahari lakini haikuwa dawa joto likawa linazidi, mara yengine akaamrisha nyumba yake kumiminiwa maji na wazimamoto masaa 24 kupunguza joto analosikia lakini joto haliku tulia. Mara yengine anaamrisha wafanyikazi wake wamueke madonge ya barafu karibu na mwili wake pia haikumfaa.

Tarehe 26 Septemba 1938, alizidiwa hadi kupoteza fahamu kwa masaa 48 na kupelekea kupoteza akili, tarehe 9 Novemba, 1938 alipoteza fahamu tena kwa masaa 38 siku ya pili yake tarehe 10 Novemba akafariki dunia.

Mwili wake uliketi siku tisa bila ya kuoshwa baada ya mashekhe wote kukataa kuosha maiti yake hadi siku ya tisa alipokuja dadake kuwahimiza mashekhe kumkafini

Mwili wake ulipokuwa unaenda kuzikwa kaburini, MWILI WAKE UKAKATAA KUINGIA KABURINI NA ARDHI IKAMKATAA kila anapopelekwa hadi ikaamuliwa mwili wake kuhifadhiwa katikati ya majiwe ya aina ya Mar-mar na kuwekwa katika Makavazi ya kitaifa ya Etnagrafi katika mji mkuu wa Ankara, kwa muda wa miaka 15 hadi ilipofika mwaka 1953 mwili wake ukagurishwa na kupelekwa kuhifadhiwa katika Jumba moja juu ya mlima katika mji mkuu wa Ankara hadi leo hii viongozi mbali mbali pamoja na Raisi wa sasa wa Uturuki Erdogan wanakwenda kumzuru katika siku za makumbusho ya kifo chake.

Wanazuoni wa wakati huo walisikiwa wakisema, "Si ardhi tu ya Uturuki iloyomkataa mwili wake, bali hata ardhi ya ulimwengu mzima ingemkataa".

*Chanzo:*
 
mederii

mederii

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Messages
690
Likes
292
Points
80
mederii

mederii

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2015
690 292 80
Mwili wake ulipokuwa unaenda kuzikwa kaburini, MWILI WAKE UKAKATAA KUINGIA KABURINI NA ARDHI IKAMKATAA kila anapopelekwa hadi ikaamuliwa mwili wake kuhifadhiwa katikati ya majiwe ya aina ya Mar-mar na kuwekwa katika Makavazi ya kitaifa ya Etnagrafi katika mji mkuu wa Ankara, kwa muda wa miaka 15 hadi ilipofika mwaka 1953 mwili wake ukagurishwa na kupelekwa kuhifadhiwa katika Jumba moja juu ya mlima katika mji mkuu wa Ankara hadi leo hii viongozi mbali mbali pamoja na Raisi wa sasa wa Uturuki Erdogan wanakwenda kumzuru katika siku za makumbusho ya kifo chake.

OK kumbe hata leo viongozi mbali mbali wanakwenda kumzuru atakua amelifanyia taifa la Uturuki maendeleo kiasi anakumbukwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
relis

relis

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2015
Messages
2,051
Likes
1,770
Points
280
relis

relis

JF-Expert Member
Joined May 24, 2015
2,051 1,770 280
Unamuombea laana mtu aliyefariki? Dini nyingine za ajab khaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mi nnachowapendea ndugu zetu hawana unafiki ktk dini yao anayeenda kinyume na maamlisho yao na akiwa ni miongoni mwao watamuombea laana bora akina sie watakuacha lkn pia hawapendi kugeana faraja ktk ukweli kutokana na mafundisho ukienda kinyume makazi ni motoni kwetu tunajifariji fulani atapokelewa na bwana hekaluni na faraja nyingine kibao ndio maana hatuna hofu dhambi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MASAMILA

MASAMILA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2014
Messages
2,282
Likes
1,807
Points
280
Age
32
MASAMILA

MASAMILA

JF-Expert Member
Joined Jun 22, 2014
2,282 1,807 280
YESU Kafundisha wapi kuua kama allah alivyofundisha? View attachment 1018981

Sent using Jamii Forums mobile app

Kila kitu kina utaalamu wake

Kwa mujibu wa uislamu kila binadamu ana haki ya kuishi kimsingi asiue wengine akitegemea kuachwa aishi ilihali ameua

Uislam unasema "Mana Qatala Qutil"

Sheria inakataza waislamu kupigana na wasiowapiga
 
busha

busha

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2019
Messages
231
Likes
190
Points
60
busha

busha

JF-Expert Member
Joined Jan 21, 2019
231 190 60
kashindwa vibaya sana mustafa,,,,kwisha habari yake,,,
 
ofisa

ofisa

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2011
Messages
2,024
Likes
958
Points
280
ofisa

ofisa

JF-Expert Member
Joined May 15, 2011
2,024 958 280
Watu hawataki kukubali ukweli kuwa ukiasi baadhi ya vitu vya mwenyezi Mungu hukukataa,
Kuna msiba nishawahi hudhuria jeneza halikupita mlangoni mpaka mashekh wakamuomba marehemu asamehe aliyowahi tendewa kwenye nyumba aliyokuwa akiingizwa.
 

Forum statistics

Threads 1,262,093
Members 485,449
Posts 30,112,813