Kifo cha Mkapa: Rais Kenyatta aotoa salamu za pole. Raila Odinga amlilia, asema Kenya itamkumbuka kwa juhudi zake za kuiletea nchi hiyo amani

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Facebook(66).png

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametuma ujumbe wa salamu za pole kwa Rais wa Tanzania, John Magufuli; Watanzania wote pamoja na familia kufuatia kifo cha Rais Mstaafu Benjamin Mkapa

Katika ujumbe wake, Rais Kenyatta amemuomboleza kiongozi huyo kama mtu bora wa Afrika Mashariki aliyefanya kazi kwa bidii kwa ajili ya amani na maendeleo ya Kanda ya Afrika Mashariki

Rais Kenyatta ameitakiwa familia ya Rais huyo Mstaafu na Watanzania wote kwa ujumla faraja kutoka kwa Mungu wakati huu wa kuomboleza kuondokewa na Kiongozi wao

Benjamin William #Mkapa aliyefariki usiku wa kuamkia leo hospitalini alikokuwa amelazwa alikuwa Rais wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2005 kupitia chama cha CCM
=====


photo_2020-07-24_09-02-59.jpg

Kiongozi wa Chama cha Upinzani cha ‘Orange Democratic Movement (ODM)’ cha Kenya, Raia Odinga ameomboleza kifo cha Rais Mstaafu wa Tanzania wa awamu ya 3, Benjamin Mkapa kilichotokea usiku wa kumkia leo

Amesema, “Mkapa alikuwa rafiki mkubwa wa watu wa Kenya, muumini mkubwa wa Pan Africanism na muamini mkubwa wa ushirikiano wa Kusini-Kusini”

Ameongeza, “Kenya tunabakiwa na kumbukumbu kubwa kwa namna alivyohusika pamoja na Dkt. Kofi Annan (Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa) na Graca Machel kusaidia nchi hii kurudi katika amani baada ya vurugu kufuatia Uchaguzi Mkuu wa 2007-2008

PIA SOMA:
= > Breaking News: - TANZIA: Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa afariki dunia
 
Lakini nyumbani sasa ....... kimyaaaa bora siyo yeye.

Mungu ndio anajuwa.
 
Ni kinyume, la Tundu Lissu, hajawahi kuliongelea hata kwa mafumbo tu, chama chake kinanunua uongozi mf ni hapa juzi kwenye kura za maoni jinsi rushwa imetembea alikua kimya, watu wakibambikiwa rushwa yupo tu, na tena alikua ana uwezo mkubwa hata kuliko wenzake, Mungu amempenda!
 
ni kinyume, la tundu lissu, hajawahi kuliongelea hata kwa mafumbo tu, chama chake kinanunua uongozi mf ni hapa juzi kwenye kura za maoni jinsi rushwa imetembea alikua kimya, watu wakibambikiwa rushwa yupo tu, na tena alikua ana uwezo mkubwa hata kuliko wenzake, Mungu amempenda!
Hawezi kufanya mambo yote pekeake, hakuna binadamu mkamilifu. Hata wanaokufahamu wanajua madhaifu yako ya kutosha.
 
Hawezi kufanya mambo yote pekeake, hakuna binadamu mkamilifu. Hata wanaokufahamu wanajua madhaifu yako ya kutosha.
Jamiiforums hasa wafuasi wa siasa za upinzani hawana mapungufu kabisa.

Na siku wakiingia madarakani hakuna pungufu lolote litakaloonekana kwa serekali yao.

Nadharia yao ya maisha ni ya kufikirika na sio halisi.
 
Pole kwa wote waliofikwa na msiba.

Taifa limeondokewa na kiongozi shupavu aliyependa uwazi na ukweli.

Aliyeipa Sekta binafsi uhai, kuimarisha uchumi, na kuweka misingi ya Utandawazi.
 
Back
Top Bottom