Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Unaweza kusikilia mahojiano ya KLHN na Mtikila jana usiku na uamue wewe mwenyewe maana haya ya kuambia na kuripotiwa na watu wengine....
Ile SMS uliyopata Mwanakijiji kuhusu Zitto huko Kenya unaunganisha vipi na mahojiano yako na Mtikila kuhusu safari ya Zitto huko Kenya..?
 
Kuna watu wamepania kulisambaratisha taifa. Cha kushangaza ni kuwa wakubwa, pamoja na madaraka makubwa waliyonayo ikiwa ni pamoja na kumweka mtu kizuizini, hawajui wafanye nini.
 
Kazi kweli kweli...sijui hapo nini ni nini...maana anachosema Mtikila hatuwezi kuthibitisha labda yeye ataweza...lets wait
 
Dah jameni sijui sasa hizi siasa zinaenda wapi maana kila pahala ni utata tu. Mtikila naona siku hizi amekua PI, uchunguzi wake ungekuwa wa manufaa zaidi kama angetoa taarifa hii wakati tukio lilipotokea na si wakati ambapo Kampeni za Uchaguzi Mdogo Zimeanza.
 
Du hii nchi inakoelekea siko kabisa. ni kama kichwa cha mwendawazimu. Ila kwa mtaji huu na mtikila kwenda kuropoka haya huko tarime kwenye kampeni jimbo la tarime chadema walisahau, hii inatisha sana, yani imekaa vibaya.
 
Mtikila anasema Mbowe, Dr. Slaa na Tundu Lisu ndio wauaji wa Wangwe .......na hili tumuamini au? Lakini nadhani watu tulitegemea atupe ushahidi wake na sio kutamka tu kwa maneno.

Bofya hapa
Global Publishers - Picha


Kama ana ushahidi kuwa ni hao waliotajwa ndio waliohusika basi ashitaki mahakamani. Kama hatafanya hivyo, hatakuwa tofauti na waganga wa kienyeji wanaochochea vitina miongoni mwa ndugu na jamaa.

Na kama kwa hili hatathibitisha vizuri, atakuwa amejisusha kwa kiwango cha hali ya juu sana, hasa kwa kuzingatia kuwa yeye ni mchungaji na mchungaji hawezi kuwa na sifa ya kuleta mafarakano kwenye kundi analolichunga. Nadhani inabidi aseme vizuri kwa hili la sivyo hatakuwa ametenda haki kwa ndugu na jamaa na Watanzania wote.
 
Asante Mwanakijiji kwa mahojiano!

Huyu bwana anashangaza kweli! Kimsingi hana jipya ile nadhani anaihujuma chadema! What a timing! Kama hawa ndio wapinzani tulionao kweli wanakatisha tamaa!
 
Kweli isije ikawa wamemuua halafu mwili ukakalishwa kwenye gari, gari ikawashwa accelerator jiwe ikajibamiza huku na kule hadi likawa nyang'a nyang'a. Yule kijana Deus Malya anastori za kutusimulia.

Mtikila kasoma Jamiiforums? Maana hii tayari ilishazungumzwa hapa JF.
 
Hivi huyu kisharudisha pesa za Rostum? Na vipi mbona amekuwa kimya sana katika mapambano na ufisadi?
JF,
Siyo fedha za Rostam tu. Taarifa zinazotufikia ni kuwa ana 50 za Makamba pia. Amepewa kwa jukumu pekee la kuimaliza Chadema kama prelude ya Kampeni za Tarime. Amechelewa tu kwenda kule baada ya kuona kuna mvua ya mawe kwa wanaoichafua Chadema. Logic ya kuomba Scotland Yard ieleweke kwa msingi huo. Haitaitwa,na ataendelea kwa kisingizio hicho kukataa kutoa ushahidi. Hata hivyo, sina sababu ya kujibizana na Mtikila, mwisho umma hautajua kichaa ni nani.
 
JF,
Siyo fedha za Rostam tu. Taarifa zinazotufikia ni kuwa ana 50 za Makamba pia. Amepewa kwa jukumu pekee la kuimaliza Chadema kama prelude ya Kampeni za Tarime. Amechelewa tu kwenda kule baada ya kuona kuna mvua ya mawe kwa wanaoichafua Chadema. Logic ya kuomba Scotland Yard ieleweke kwa msingi huo. Haitaitwa,na ataendelea kwa kisingizio hicho kukataa kutoa ushahidi. Hata hivyo, sina sababu ya kujibizana na Mtikila, mwisho umma hautajua kichaa ni nani.

Dr Slaa una ushahidi kuwa Makamba kampa 50m? Mh tunakuheshimu sana mambo ya kuokoteza udaku kwa mtu calibre yako sio mazuri kabisa
 
Asante Mwanakijiji kwa mahojiano!

Huyu bwana anashangaza kweli! Kimsingi hana jipya ile nadhani anaihujuma chadema! What a timing! Kama hawa ndio wapinzani tulionao kweli wanakatisha tamaa!
JF,
Nashukuru kuwa angalau sasa somo linaanza kueleweka. Tuliposema, Chadema tuko tayari kwenda peke yetu wengi walitulaumu wakadhani tumefanya makosa makubwa kukataa ushirikiano. Tuliweka wazi kuwa hatuhitaji kufanya siasa ya unafiki, na wala kushirikiana na watu ambao mchana tunacheka usiku wanatuhujumu. Nadhani somo linaanza kueleweka, na tunakaribia wakati ambapo Watanzania sasa tunaweza kuwaambia, kuwa viko ni vyama vichache sana vilivyo serious ambavyo mtu anaweza kushirikiana navyo.Watanzania nadhani sasa mnaanza kutuelewa.

Viko vyama vina njaa haviwezi kujizuia kupokea "vijesenti", viko vyama vinatumika na dola na CCM, viko vyama vipo tu, alimradi vinapata heshima pale vinapoalikwa kwenye sherehe au shughuli za kitaifa. Nasikitika sana hii ndiyo hali halisi lakini ukweli umma lakini ni vema tukausema ili tujue tuendako. Ukombozi hautaki kudanganyana tena. Hata ndani ya Chadema, sisemi njaa haipo, na kwa bahati sasa tuna ushahidi kamili, tena wa viongozi wazito, japo tumewastukia mapema na kuthibiti.

Wakati utakapofika tutauweka hadharani ili mfahamu mazingira tunakofanyia kazi na jinsi vita hivi vilivyo vigumu iwapo hatutakuwa makini au tukimeza tu kila kinachosemwa na yeyote bila kufanya utafiti na tathmini ya kina ya kila tukio. We promise wa-Tanzania kwa kadiri ya uwezo wetu tutafanya kila linalowezekana tusingizwe mkenge na mafisadi ambao wanatafuta kila njia kutuvuruga.
 
Dr Slaa una ushahidi kuwa Makamba kampa 50m? Mh tunakuheshimu sana mambo ya kuokoteza udaku kwa mtu calibre yako sio mazuri kabisa
Masatu,
Unajua kabisa sina tabia ya kuropoka na wala kutamka kitu sina uhakika nacho. Kipindi chote tulichosemwa wakati wa msiba wa Wangwe tulikaa kimya kwa sababu hatukuwa na kitu mikononi mwetu. Sasa tunacho na hatuna wasiwasi. Mwulizeni Makamba akanushe na aone tutakavyomwumbua. Kwa taarifa yenu wala siyo huyo tu.
 
Jamani kwani Mtikila ile milioni 3 ya Rostam Azizi amesha rudisha??
Isije ikawa ndo wanalipana kinamna kwa kuwashafua watu......tuwe makini.
Na tumwulize vita yake dhidi ya fisadi Rostam imeeishia wapi???Mbona kimyaaaa?
 
na hao wanachadema wakienda kukampeni huko tarime wajiangalie sana!maana hayo maneno ya mtikila yakifikishwa kwa wananchi wa tarime ni balaa!viongozi wa chadema muwe makini sana maana mnahusishwa moja kwa moja na kifo hiki!kama ni kweli hii damu haitaenda bure!
First Lady,
Asante kwa tahadhari. Kwa bahati nzuri, Tarime siyo mnayosoma kwenye magezeti yanayomilikiwa na mafisadi wala yaliyokuwa simulated. Wanatarime wanajua ukweli, wanaiamini Chadema, wanaipenda Chadema usidanganyike na unayoyasoma.

Maneno hayo, tulijua Mtikila ataenda kusema, hatukujua content lakini tulifahamu alipo "ajiriwa na Makamba" na tukawajulisha. Hivyo, wapenzi wetu mtulie tu mfuatilie mambo kwa kusoma magezeti na kufanya uchambuzi wa kina. Ushuhuda wa wazi ni Kampeni yetu ya Ufunguzi ilivyoenda kwa amani na ufanisi mkubwa jana.

Wapenzi wetu mlioko mbali mtutakie heri na kutuombea kila mmoja kwa imani yake.Tuweke mapenzi kwa Wanatarime mbele kuliko mapenzi ya Vyama vyetu nina hakika tukifanya hivyo, Mungu, kwa wale wanaomwamini, atawapa watu wake aliyowapingia.
 
Dr Slaa una ushahidi kuwa Makamba kampa 50m? Mh tunakuheshimu sana mambo ya kuokoteza udaku kwa mtu calibre yako sio mazuri kabisa
Ushahidi gani unaodai wakati Rostam alishaweka mambo hadharani?Huyo jamaa is for a price he can dance any tune provided is given something.Naomba mrudi kwenye ile posting ya jana ya breaking news ya huyu jamaa.Nilitoa angalizo kuwa inawezekana huyu mtu ameshinda kesi ya uchochezi ya Mkapa kuwa ni raia wa msumbiji at a price ya kuchafua wapinzani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom