Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Kasheshe unataka watu waanze kuhoji mazingira ya kifo baada ya mtu kuzikwa? sasa ikibidi kufukua mwili si ndo itakuwa kasheshe? (pun intended.. lol)

Mzee Mwanakijiji,

kwi kwi kwi

In short taifa lenu limepranganyika... kila siku watu wanakwepa issue muhimu kwenye taifa letu... nalo ni KUFANYAKAZI KWA BIDII na Maarifa... na KUKUZA UCHUMI.

Hizi siasa na spinning zisizoisha hazilisaidii taifa hata kidogo!!!

Anyway muda si muda hata hili mtasahau pia... kwani la Balali, Amina Chifupa, Mama Mbatia... si mumeshasahau?
 
Huu ndiyo undumilakuwili wa SIRI KALI ambao Watanzania wengi tunauchukia!!! Iko wapi autopsy report kuhusiana na vifo vya Ballali, Amina Chifupa, Mama Mbatia ambao wote vifo vyao vilikuwa vimegubikwa na utata mkubwa? Au autopsy inafanywa pale tu aliyefariki ni kutoka chama cha upinzani? :confused::confused::confused:[/B]

[COLOR="DarkRed"]Hapa alarm ya hatari inalia, kuna uwezekano kuwa wamekimbilia kufanya autopsy ili kutoa taarifa ya kuzima mjadala baadae. This is a possible new tactic ya mafisadi kunyamazisha watu, kweli sasa ni wakati wa kumpa mchawi akulindie mwanao, Polisi lazima wawape ulinzi wabunge wanaoonekana ni mwiba kwa mafisadi bila kujali wanatoka chama gani[/COLOR]
 
Re: BREAKING NEWS: Chadema wataka Maelezo; Wabunge wake watishiwa!

--------------------------------------------------------------------------------

Haya sasa,

Jambo limezua jambo. Yanayosemwa Tarime ni mengi sana kuhusiana na kifo cha mbunge wetu Chacha Wangwe. Tetesi zimekuwa nyingi na washukiwa ni wengi hadi inatia simanzi zaidi kuliko faraja.

Wengine wanasema:

1. Serikali imehusika
2. Rostam Azizi amehusika
3. Chadema wamehusika
4. CCM wanataka jimbo la Tarime.
5. Makampuni ya kuchimba madini
6. Wakereketwa wasiompenda Wangwe
7. Kifo ni cha kawaida kama vifo vingine

Ombi kwa wakazi wa Tarime, tusikubali kugawanywa na vyombo vya habari - TBC hadi vile vya habari corporation ambao wanataka kuleta mgawanyiko wa kikabila na kikoo Tarime.

Tuwe na nguvu na tumalize maombolezo kwa amani na turudi kujenga taifa na jimbo letu ambalo liko nyuma sana kimaendeleo.
Maneno mazito sana haya, ubarikiwe mkuu, na tupo ukurasa mmoja hapa!
 
Maneno mazito sana haya, ubarikiwe mkuu, na tupo ukurasa mmoja hapa!

Mkuu...naona Mnyika amei-quote TBC1 hivi TBC1 imekuwa na tatizo gani tena?

By the way sidhani hapa nchini hivi sasa kuna taarifa ya habari ambayo ina quality ya hali ya juu kama ya TBC1, guys wanahakikisha pande zote zinawekwa hewani.... by the way fanya research majority are now tuning to TBC1...

Tupende tusipende Tido... ameweka changamoto kubwa kwa mambo ya news nchini....
 
MJJ,
Nakubaliana na wewe. Alipokufa Sokoine nilijua kuwa watasema ni nani alimuuwa Pm wetu. Niliamini kuwa ALIFIA Dodoma na kupelekwa Kongwa huko huko na huko jamaa wakaset ajali. Niliamini kuwa wamemuulia Dodoma kwa sababu moja tu. Siku hiyo nilikuwa Dodoma na niliiona kwa macho yangu ndege ya Rais imekuja kumchukua Sokoine. Nilishangaa na ukali wake wote Sokoine kuruhusu ndege ije hadi Dodoma na halafu ikifika aseme "Sitaki ndege na nitarudi kwa gari na wenzangu..". Kwa ndege angelisafiri na rafiki wengi tu zaidi ya kusafiri kwa gari ambalo anakuwa peke yake, safari ni ndefu na wastage of FUEL and time which is equal to money, tena hela za walipa kodi ambazo huyu jamaa alikuwa na uchungu nazo saana.
Hili nalo naliona liko hivihivi. Nilitaka kuandika kwenye makala ya kifo cha Wangwe ila nikasita. Nilitaka kuandika sentesi moja tu kuwa KAMPENI ZA UCHAGUZI ZIMEANZA. Safari hii naona mambo yatakuwa na uzito wa Marcury.

tanzania yetu, unajua dereva wa sokoine wa kila siku ndiye aliyesafiri pamoja na hiyo ndege, hakuweza kumuendesha mkuu sababu kichwa kilikuwa kinamuuma,ikabidi sokoine apatiwe dereva mwingine ambaye alinusurika ajali na sijui yu wapi. wanafikiri hatuji kumbe tunajuwa.tunakubali tu kuzugwa,sababu hatuna jinsi.

nilishasema na narudia kusema tena,kulikuwa hamna ajali wala nini.

halafu mh. zitto nilishawahi kukwambia kuwa macho, hapa hapa JF! tusiwage tunazarau wengine wanavyosema.

tuwe macho,tutasikia huyo malya kajiuwa na hicho kibastora chake kwa kusingiziwe yeye ni muhuaji.
 
Ka nzi ka KLH Kamepeperuka...

Nimepatiwa majibu yafuatayo. Bado mengine tunaweza kusahihisha kwa kadiri nzi anavyoruka ruka. So, right now I'll give the following info 80% ya usahihi.

3.Huyu kijana yeye ndio alikuwa wa kwanza kuipigia polisi simu na kuwataarifu kuhusiana na msiba huo. Sasa hapa panaleta utata mkubwa sana ;

a) Alipata wapi number za simu za polisi?Tena hapo hapo?
b)Ni kwanini awapigie polisi wa kwanza ,na je?yeye kama alikuwa na simu za Wangwe aliwezaje kuzipata kwa hali gari lilivyokuwa?
c)Huyu kijana aliwapigia simu watu wa Tarime na kuwafahamisha kuwa Wangwe amefariki ,na mmoja wapo ni aliyekuwa rafiki wa karibu wa Chacha ambaye alikuwa katibu wa CHADEMA wilaya ya Tarime aliyehamia CCM.
D) Alimpigia simu mke wa Marehemu pamoja na ndugu zake marehemu, ila hakupiga simu kwa kiongozi yeyote wa CHADEMA ,ile hali kama alikuwa anatumia simu za Wangwe basi number za simu za viongozi wa CHADEMA zilikuwepo.
e) Mkuu wa wilaya ya Kogwa alienda eneo la ajali in 30 minutes time ,baada ya ajali na ndio alimfahamisha Mkuu wa Mkoa ,then Waziri wa mambo ya ndani na then Spika.....
f) Zitto alipigiwa simu na waziri Masha, na baada ya simu kukatika alimpigia spika na spika akasema hata yeye kayasikia hayo .

4.Huyu kijana Mallya ,kwa taarifa za leo ni kuwa amekubali kuwa yeye ndio alikuwa anaendesha gari ,na hilo kalisema polisi .

5.Huyu Mallya kuna taarifa kuwa ameiharibu simu yake na ameondoa simu card yake pamoja na kingine kikubwa na cha kustaajabisha ni kuwa ameondoa memory card ya simu yake .

Sasa hili la memory card linatupa wasiwasi zaidi na hatujui ni kwanini hilo limefanywa hivyo na hii inaonyesha kuwa aliyefanya hivyo lazima atakuwa ni expert mzuri sana .

6.Kwa taarifa za kiuchunguzi ni kuwa huyu Mallya alikutwa na bastola, na alisema kuwa ni ya kwake ,sasa hatujui kama hili polisi watalisema kwani hilo limesemwa na watu ambao walikuwepo wakati polisi walipokuwa wamefika eneo la ajali na kuanza upekuzi.

7.Huyu Mallya ,inasemekana kuwa alikuwa na mtu mwingine kwenye gari ambaye wanakijiji wa pale hawakuweza kumfahjamu mara moja, na haijulikani alipo.

8,kwenye eneo la tukio mzee wa pale kijijini ambaye alisaidia kumtoa Wangwe kwenye gari anasema kuwa huyu wangwe alikuwa amekaa kiti cha abiria mbele ,na alikuwa amefunga mkanda, na huyu mzee ndio alimtoa huop mkanda na kumtoa nje.

My Take:
- The burden of proof, iko kwa Polisi kumuweka kijana huyo kizuizini. My gut tells me something about assassination. It is just my gut and I probably am very wrong.
- Kama kweli Mallya alikuwa na bunduki, was it discharged for any reason even "accidentally"?
- Kuna mtu aliomba lift aidha walipoenda kununua "voucher" kutokana na ushauri wa Mallya. Huyo mtu wa tatu hakuwepo mwanzo wa safari, na kwa hakika hakuwepo mwisho wa safari. Who is he?


Mwanakijiji ,

Thanks alot kwa kuweza kuunganisha vipisi vya hii hadithi , kusema ukweli hii habari hata mimi inabidi niconfess inanichanganya sasa . Kitu ninachojiuliza huyu Kijana Malya alikuwa ni nani ? na jee ni kwa nini marehemu alikuwa akijiuhusisha na hawa watu ? Na inawezekana vipi kumpa mtu lifti saa mbili ya usiku mtu usiyemfahamu, hii aingilii akilini .
 
Kama wewe peasant mimi farmer..Kaa kushoto na uache unafiki kama huna maswali ya msingi usiharibu!

Wewe una mawazo finyu...Ni wale watu waliokuwa wakisapoti vita ya Iraki licha ya wao kuwa waafrika!

Usilete ushambenga kwenye issue nyeti.Huyu mtu aliemtuma kijana mwenye jina la kichagga ana lake jambo.

Kama ni kweli chadema wamehusika...Na wakati huo huo wao wanaambiwa ni chama cha kichagga..Basi wasingemtumia kijana anayeitwa Mallya.

Huyu amepandikizwa na uchunguzi ni muhimu.

Mimi kusema alimwe risasi sikumaanisha hivyo...Na mimi nilishamema before...Inaelekea wewe ni mgeni hapa...LAKINI KILA AMBALO NIMEKUWA NIKITABIRI HUTOKEA...Liwe zuri ama baya..Imekuwa ikionekana kama ninajuwa something..Lakini ukweli mimi sina influence yoyote..Mimi ni mwananchi wa kawaida...Ila mwene uwezo wa kufanya reserach za nguvu na analysis xenye kumake sense...Hilo huitaji kupinga...Hapa jf ni mashahidi wangu...Kila kitu mpaka saa nyingine najiogopa mwenyewe.

Na ndio maana nikasema ni muhimu tujuwe kile kilichotuleta hapa duniani.

Kwakuwa nilisema pia sisi sote ni wasafiri...Hawa chadema na wao bado wana siasa za kinafki zilizolicost taifa letu...Kama this time hawataenda kwenye target yenyewe...Basi hata wao wengine wataendelea kuuwawa tu.

Nawashangaa sana kwani ni wao walikuwa wakisema Mrehemu ana UHUSIANO NA ROSTAM AZIZ...Sasa badala a kuweka ushahidi wa mazungumzo ya watu hao na mambo mengine wao wanaondoa jicho kwenye target na kuwaomba polisi msaada...Polisi hao hao waliomkamata Kubenea kwa kusaidiana na hao wanausalama mafisadi...Ni polisi hao hao mnataka watowe ripoti?

Polisi hao hao waliomwua Kombe kwa kudhani ni JAMBAZI?

Huyo Mallya aliwapigia polisi simu...Nani alimpa namba huyo mtoto na kumwezesha kufanya mambo hayo yote?
Hapo FBI WAITWE.


Talking crap you psycho!
 
Hapo tutajadili nini? Niletee kadi ya chama kama unajua mapenzi yangu kwa chama chochote. Mapenzi yangu ni kwenye ukweli na kuwa tayari kusema hata yale ambayo wengine wangeogopa kwa hofu ya kushambuliwa.

Ulisema Chacha atwangwe risasi, sasa unasema huyo kijana ni nyoka? Una ushahidi gani?

Hakuna hata mtu ambaye anaongelea well-beings za huyo kijana ambaye si ajabu ni victim tu katika mchezo huu unaoitwa siasa.

Mtanzania...ccm wajanja kama nyie...Mnang'ang'ania kuwa ni ajali tu ya kawaida...Hata hivyo ujanja huo una athirika na maswali magumu magumu ya mara kwa mara kwasababu mmeonekana kumtetea huyo Mallya kuliko ilivyo kwa chadema ambao hata hawamjui.

ccm wajinga...Wao wanang'ang'ana na kusema ni chadema TBC wamshaonyesha muelekeao huo.

Haalfu kuna wale wanaojidaia wako above the frey...Wao wanajidai kusema kuna fununu za private corporations zinazohusisha magonvi ya koo nk. kwenye kugombea ardhi.

Hakuna ponti muhimu hata moja ambayo sijaigusia katika thread zote hizi zenye kuhusiana na sakata hili.

All in all...Bottom line kumshughulikia fisadi mara moja ndio solution...Mmeona kuna wana ccm walioko huko uingereza ambao pointi yao kuwa JK apewe muda kwasababu kesi hii ya mafisadi ni kubwa na awe makini ni kauli za kuendeleza muda wa kutowa mauwaji na pengine hata sisi huku maisha yetu yako hatarini na dalili nyingi sana ninaziona hata mimi huku.

Sitaki kusema chochote kwasasa lakini nashangaa sana kwanini nimekuwa mwiba kwa kiasi hiki kwa mafisadi!

Haya yote nitayatolea maelezo baadaye..Mimi najuwa kabisa mjadala huu utaendelea kubadilika kila siku.

Nimeshasema na bado ninaendelea kusisitiza...HUYO NDUGU YETU MOD ANAYEITWA SILENCER NI LAZIMA ANINJIBU...NARUDIA...NI LAZIMA ANIJIBU MARA MOJA!

KWANINI ALISHTUSHWA NA KAULI YANGU?

HALAFU MTU AKAFA KESHO YAKE KWA MAZINGIRA KAMA HAYA?

TENA KWA MTU ANAYEITWA MALLYA?

MALLYA WA WAPI HUYO?

KIBOSHO?AMA WAPI?

HALAFU NA JOHN MNYIKA AKALETA PROPAGANDA KUWA MANGI SINA ALIKUWA MSALITI....NA MIMI KWA ASILI NI MJUKUU WA MANGI SINA...NA HILO WANALIJUWA...KWANINI JOHN MNYIKA HAJASEMA KUWA NI KWANINI ALIMWITA BABU YANGU MSALITI?!

HIZI NI SHUTUMA DHIDI YANGU AMBAZO CHADEMA NATAKA MZIJIBU.

KWASABABU KAMA VIONGOZI WENU WANAAMINI SINA AMBAYE KWA ASILI NI BABU YANGU KABISA NI SAWA NA KUDAI WAKIBOSHO NI WASALITI..SASA KAMA HAMYAJIBU HILI...THEN CHADEMA MMEANZISHA VITA NA WAKIBOSHO....NA MIMI KAMA MJUKUU WA SINA...NITAPAMBANA KWA UDHALILISHAJI HUU...UNLESS MLETE UDHIBITISHO WA USALITI HUO!
PAMOJA NA HUYO MOD ANAYEITWA SILENCER!
 
How interesting and sad. Witherto Tanzania !! The country has surely gone to the dogs - now, what next. My heart cries for a revolution but, alas am but a poor soul with no past or future - for it has all been taken away from me by evil forces that thrive on the plight of the helpless wananchi. How I wait for the new day when the people will rise up and with deafening voices proclaim - enough is enough. No more of this tomfool hardy, no more of this chicanery and no more of this subterfuge. Fellow Tanzanians we are in for a ride and what a ride it must be for with our eyes blindfolded, we can not see leave alone guess where wea are heading. The bitter truth is - we are heading NOWHERE and it is all like a DREAM.

Hey, we need to wake up and throw away the yokes of bondage. We are being led by a band of blood-thirsty individuals that will not rest rest till we are all sucked dry. The fact that at the helm we have a leader (or dont we?) going by the name of Jakaya Mrisho Kikwete, should be enough to motivate and wise us up. It is never too late to do something only the sooner the better.
 
Haya sasa,

Jambo limezua jambo. Yanayosemwa Tarime ni mengi sana kuhusiana na kifo cha mbunge wetu Chacha Wangwe. Tetesi zimekuwa nyingi na washukiwa ni wengi hadi inatia simanzi zaidi kuliko faraja.

Wengine wanasema:

1. Serikali imehusika
2. Rostam Azizi amehusika
3. Chadema wamehusika
4. CCM wanataka jimbo la Tarime.
5. Makampuni ya kuchimba madini
6. Wakereketwa wasiompenda Wangwe
7. Kifo ni cha kawaida kama vifo vingine

Ombi kwa wakazi wa Tarime, tusikubali kugawanywa na vyombo vya habari - TBC hadi vile vya habari corporation ambao wanataka kuleta mgawanyiko wa kikabila na kikoo Tarime.

Tuwe na nguvu na tumalize maombolezo kwa amani na turudi kujenga taifa na jimbo letu ambalo liko nyuma sana kimaendeleo.

Bw. Kibiti,

Bado nimejawa na simanzi kubwa kufuatia kifo cha ghafla cha huyu mbuge, Chacha Wangwe. And yes, I don't know what really happened hadi hiyo mauti kumfika, ila I'm so sick na jinsi watu wanavyojaribu ku-politicise hii issue.

I couldn't agree more with you kwamba whatever happened to "what might have been the motive behind," wana-Tarime wasikubali kamwe kugawa na hizi conspiracy theories zinazorushwa hapa; isipokuwa watulie, waomboleze kwa amani, kisha wajipange upya kujenga jimbo lao la Tarime ambalo lina kila sababu ya kuwa "super-jimbo," ila kwasababu ambazo nyingi zimechangwiwa na serikali kuu, bado liko nyuma [sana] kimaendeleo.

Coz the thing is, hata kama hizo conspiracy theories zitakuwa ni za kweli, still hakuna mtu toka serikali kuu aliyetayari kubeba fate ya Tarime. Fate ya Tarime itabebwa na wana-tarime wenyewe. As the old saying goes, "Each man is the architect of his own fate."
 
I'll tell you one thing. Anayedhania Polisi are willing, able, and determined to find out the truth anaota njozi. Tukubali tu yaishe. Believe me, "mapenzi ya Mungu" yataimbwa kama wimbo wa "Kasuku". You know what, I'm so done, sitoingia zaidi ya nilivyoingia, it is very dangerous.

Anayeamini ajali aendelee asiyeamini lwake!


Mmh! Mkuu inaelekea mambo ni mazito?
 
Kijana Malya ambaye ni mnusurika wa ajali iliyo muua Mbunge wa Tarime Chacha Wangwe karibu miezi miwili hivyo iliyopita alijitambulisha kwa mwandishi mmoja wa gazeti la Mwanahalisi kuwa yeye ndiye "invisible" wa JF na ya kuwa yuko tayari kuwa anampositia material kwenye mtandao huu. Baada ya the real "slim shaddy" kupewa taarifa hiyo, akaunganishwa na simu na "Malya" ambaye baada ya kubanwa na kukemewa aliambiwa aache mara moja kujihusisha na JF na kujifanya ni "Invisible".

Baada ya ajali kutokea, Bw. Malya alikuwa kwa hakika aruhusiwe kuondoka eneo hilo lakini kutokana na hofu ya internal bleeding akapelekwa hospitali. Na mmoja wa maafisa wa ngazi za juu wa Chadema alituma ujumbe usio na utata kuwa kijana huyo aendelee kuwa katika uangalizi wa Polisi ili kuweza kusaidia kupata majibu. Siku ya leo Polisi wamejifunza mengi sana.

Ka nzi kameruka tena! ....
 
Last edited by a moderator:
Maskini, sasa hivi sisi tutaanza lini kupata ukweli wa haya mambo? Tuanze kujiuzulu hawa polisi wetu wapo kwa ajili ya nani hasa? Inawezekana adui wetu hatujamlenga.

Ni vigumu mno kuendelea kuandika chochote...

Mtanzania bado unasema hii ni ajali ya kawaida na hatuhitaji uchunguzi wowote? Umeona sasa kwa nini watu tulikuwa tuna wasiwasi na aliyekuwa dereva, kumbe ni huyu kijana ambaye hajulikani kwa chadema wala familia, na kumbe alikuwa na bastola? Makubwa

Kitila,

Wapi nimesema hatuhitaji uchunguzi wowote? Kifo chochote lazima kichunguzwe mpaka ukweli wote ujulikane. Hiyo ndio kazi ya polisi. Polisi ambao wanafanya chochote tofauti na hicho, wanakiuka maadili ya kazi zao na wanahitaji kulaumiwa na ikiwezekana hata kufukuzwa kazi.

Ninachosema mimi sioni sababu ya hizi pressure za wanasiasa kwenye hili suala. Tuwaachie polisi wafanye kazi yao.

Aidha mimi naamini hii ilikuwa ni ajali na hakuna mkono wa mtu, naweza kuwa wrong kama ambavyo nimewahi kuwa wrong kwenye mambo mengi tu niliyowahi kuyaamini. Lakini mimi siweki mambo ya uchawi au mkono wa mtu mpaka kuwe na ushahidi wa kutosha.

Inasikitisha ninaposikia na kusoma maandishi ya watu juu ya huyo kijana ambaye naamini ni victim pia kwenye hili. Badala ya kupewa pole, anarushiwa maneno yote hayo tena na watu wenye mamlaka. Imagine ungelikuwa wewe au hata mdogo wako?
 
Kijana Malya karibu miezi miwili hivyo iliyopita alijitambulisha kwa mwandishi mmoja wa gazeti la Mwanahalisi kuwa yeye ndiye "invisible" wa JF na ya kuwa yuko tayari kuwa anampositia material kwenye mtandao huu. Baada ya the real "slim shaddy" kupewa taarifa hiyo, akaunganishwa na simu na "Malya" ambaye baada ya kubanwa na kukemewa aliambiwa aache mara moja kujihusisha na JF na kujifanya ni "Invisible".

Ka nzi kameruka tena! ....

Ndo huyu huyu 'rafiki' wa marehemu Wangwe ama mwingine?
 
wangweshuhuda.jpg

Mkazi wa eneo la Pandambili, Mwiguni George, aliyefika dakika chache katika eneo la Pandambili baada ya kutokea ajali iliyosababisha kifo cha Mbune Chacha Wangwe, akieleza hali ilivyokuwa kwa Kamanda wa Polisi, Peter Kivuyo, (kulia).

Date::7/30/2008
Kifo cha Wangwe: Shuhuda atoa taarifa mpya polisi

* Adai Mbunge Wangwe hakuendesha gari lililopata ajali

Na Faraja Jube, Dodoma
Mwananchi

UTATA umejitokeza iwapo marehemu Chacha Wangwe aliyefariki katika ajali ya gari Jumatatu usiku alikuwa akiendesha gari hilo ama la.

Kwa mujibu wa mtu aliyefika katika eneo la tukio dakika chache baada ya ajali hiyo, Mwiguni George, alimkuta marehemu Wangwe akiwa katika kiti cha mbele cha abiria huku sehemu ya kichwa chaki kikiwa kimebanwa ubavuni mwa kiti hicho na mlango wa nyuma.

Akizungumza juzi mbele ya Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kamishina Msaidizi wa Polisi, Peter Kivuyo, Kamanda wa Usalama Barabarani wa Mkoa wa Dodoma, Vitus Nikata na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kongwa, Ramadhan Kalowa, Georgr alieleza kwamba alikuta mwili wa marehemu Wangwe ukiwa umebanwa ubavuni mwa kiti na mlango wa nyuma huku mkanda wa usalama katika gari hilo ukiwa bado upo mwilini mwake.

''Nilikuwa nyumbani nasikiliza kipindi cha michezo, muda ya saa mbili na nusu usiku, nikasikia kishindo kikubwa, nikakimbilia eneo la ajali. Nilipofika katika eneo la ajali nilimkuta kijana mmoja akiwa analizunguka gari huku akipiga kelele za kuomba msaada,'' alieleza George.

Hata hivyo, mtu huyo alieleza mashaka yake kuwa kulikuwa na watu watatu katika gari hilo na siyo wawili kamba ambavyo ilitangazwa katika vyombo vya habari.

Juzi Deus Francis Mallya alikaririwa mara mwili wa marehemu ulipofikishwa katika hospitali ya Mkoa ya Dodoma, akisema kwamba walikuwapo wawili katika safari hiyo na kwamba marehemu Wangwe ndiye aliyekuwa akiendesha gari.

''Nilisikia katika taarifa ya habari kuwa walikuwa wawili. Marehemu ndiye aliyekuwa akiendesha gari na kwamba mmoja amepona. Mimi nina mashaka, kwani nahisi kuwa na mtu wa tatu na kwamba marehemu hakuwa anaendesha gari wakati wa tukio,'' alisema George na kuongeza.

''Nilipofika katika eneo la ajali kulikuwa na mtu mwingine ambaye alikuwa akiwatawanya watu walioanza kufika kwa ajili ya kutoa msaada wasilikaribie gari. Hata hivyo, tulianza kuutoa mwili wa marehemu uliokuwa katika kiti cha abiria upande wa mbele,'' alieleza George.

''Nilimvua mkanda wa usalama katika gari ambao bado ulikuwapo mwilini mwake, kisha tukamtoa kupitia mlango wa dereva kwani mlango upande aliokuwa amekaa haukuweza kufunguka,'' alisema.

Kwa mujibu wa Goerge, mtu huyo wa tatu alielekeza kutolewa kwa fedha alizokuwa nazo marehemu ndani ya mfuko wa koti, jambo ambalo lilimfanya shuhuda huyo kuhisi kuwa alikuwa pamoja nao.

''Tulianza kutoa vitu vya marehemu na mtu huyo alielekeza kuwa kuna fedha ndani ya mfuko wa koti,'' alieleza na kuhoji: ''Sasa mie nikajiuliza kama hakuwa nao alijuaje kuwa marehemu aliweka fedha ndani ya mfuko wa koti?''

Hata hivyo, shuhuda huyo alieleza kuwa wakati pilikapilika zilipokuwa zikiendelea, hakuweza tena kumuona mtu huyo wa tatu, ambaye alitoweka.

Maelezo hayo ya George yalipelekea Kamanda Kivuyo kuagiza askari waliokuwapo katika eneo hilo kuchukua maeleo ya shuhuda huyo kwa ukamilifu.

''Kwanza nakupongeza sana kwa ujasiri wako na moyo wa kizalendo wa kutoa msaada kwa marehemu,'' Kamanda Kivuyo alimweleza shuhuda huyo.

Maelezo hayo yanaleta mkanganyiko kutokana na taarifa za awali kuwa marehemu Wangwe alikuwa akiendesha gari na kwamba walikuwapo watu wawili katika gari hilo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom