Kifo cha Mh Regia, Kilombero walia na Mteketa!

MUNGU WETU USILALE KAMA TUNAVYOLALA WAJA WAKO!

Nakuomba ukanyanyue mkono wako na waepushe na michafuko yote ile inayonyanyuka.
Naamini ni huyu mwovu shetani ndiyo anayenyanyua kichwa lakini hana mamlaka yoyote mbele yako Mungu wangu!

Mwana Mpotevu hebu fuatilia na tunakutegemea kwa news zaidi!
 
mmm jamani inasikitisha sana,mwenyezi mungu awape faraja yake wazazi,ndugu wapiga kura wake,wabunge wenzake na watanzania wote,bwana alitoa na bwana ametwaa jina la bwana libarikwe,
Dada Regia umetutoka tungali tunakuhitaji, tunamis uwepo wako.
 
na wananchi wanachomaanisha hapa ni ushirikina unaominika kufanywa na Mh Mteketa! Imani yao kubwa ilikuwa kwamba mbunge wa jimbo ni marehemu regia! Inashangaza kwa kweli,ila kwa ujumla msafara mzima umefika salama salmini kwa mengine ni kwamba huku pia naona chadema wanakubalika sana

Hii inanikumbusha kifo cha marehemu chacha wangwe!kwanini wabunge wa chadema hawafi kwa amri ya mungu mpaka wahusishwe wanasiasa wengine?kwa wangwe tuliambiwa ni bwana mbowe ndio alihusika na kile kifo kutokana na tofauti zao za kisiasa na marehemu,hapaa tena tunaambiwa ni mteketa! kuna nini chadema?
 
Nikiwa kwenye msafara wa magari yaliyotoka Dar na viongozi mbalimbali ,wanafamilia wa marehemu mh Regia,na wananchi wengine ingawa na usiku saa 3 kamili tunaingia ifakara kuanzia keepleft mpaka maeneo ya msamaria mwema kituo cha mafuta mji umezizima! Kwa majonzi! Watu ni wengi barabarani akina mama vijana na watoto wanalia kwa kwikwi wengine na wengine wamethubutu kulia na mh mbunge wa jimbo la kilombero ABDUL MTEKETA kuwa amechokoza nyuki!

Jamani msitake kutafuta mchawi kwa hii ajali.

Kwa kuangalia tu kwa macho Gari la Marehemu utaona wazi hakuwa amefunga mkanda (safety belt) wakti anaendesha gari. Vile vile mwendo kasi na hakuwa na uzoefu wa kutosha kuendesha gari kwa mwendo mrefu.

Kifupi hakufata sheria za uslama barabarani.

Asitafutwe mchawi kwa hilo. Kosa lake hakufata sheria za usalama barabarani

Mkuu mimi Regia niliwahi kukutana nae ana kwa ana na aliniambia hiki ninachokisema, Mungu amemwepusha na mengi ila nitakuwa wa mwisho KUTOAMINI kuwa hii ajali Mteketa hajahusika

kwa hiyo unaamini kuwa mtu akikufanyia urogi/uchawi unakupata na unaweza kufa?

Na ulinzi wa Mungu unaemuamini haufui dafu kwa urogi?
 
  • Thanks
Reactions: bht
Hata mimi nilishangaa kwani eneo la ruvu darajani halina kona yoyote iweje asione mbele kama kuna gari wakati ana overtake?pili, kama gari lilipinduka mara saba na kugalagazwa vile why only Regia??ndio kuna mipango ya Mungu lakini hapa napata mashaka kwamba huenda ni mapenzi ya Mungu yaliyotimia kupitia kwa mtu flani kama ambavyo Yesu alikufa lakini kwa kupitia usaliti wa Yuda,

Hata wewe Mrembo by Nature!
 
  • Thanks
Reactions: bht
kwa hiyo unaamini kuwa mtu akikufanyia urogi/uchawi unakupata na unaweza kufa?

Na ulinzi wa Mungu unaemuamini haufui dafu kwa urogi?

kwa yeyote anayemuamini Mungu na bado akaogopa nguvu za uchawi si muumini wa kweli?

Hivi tunayeamini Mungu alimuumba na huyo 'mchawi' tuseme anauwezo mdogo kulinganisha na wa kiumbe chake?
 
kwa yeyote anayemuamini Mungu na bado akaogopa nguvu za uchawi si muumini wa kweli?

Hivi tunayeamini Mungu alimuumba na huyo 'mchawi' tuseme anauwezo mdogo kulinganisha na wa kiumbe chake?

Kama unaamini Mungu ananguvu kuliko kila kitu na wewe ni muumini mzuri, basi sioni kwa vipi utaamini kuwa urogi ushinde nguvu za huyo Mungu unaemuamini

Logically mchawi atakuwa kamzidi nguvu mungu ndo maana urogi unakupata

Hitimisho ni kuwa, umeleta dharau kwa mungu wako kuwa anaweza kuzidiwa nguvu na mchawi mmoja tu

*Idea tu ya kuamini kuwa kuna wachawi inanshangaza sana
 
Jamani msitake kutafuta mchawi kwa hii ajali.

Kwa kuangalia tu kwa macho Gari la Marehemu utaona wazi hakuwa amefunga mkanda (safety belt) wakti anaendesha gari. Vile vile mwendo kasi na hakuwa na uzoefu wa kutosha kuendesha gari kwa mwendo mrefu.

Kifupi hakufata sheria za uslama barabarani.

Asitafutwe mchawi kwa hilo. Kosa lake hakufata sheria za usalama barabarani

barubaru umeongea,maana ishakuwa kazi mara huyu mara yule
 
Kila Mwanasiasa akifa eti kuna Mguu wa mtu, jamani tuacheni Imani za kishirikina, Mungu ametwaa, kama kweli watu wanakufa kwa ushirikina basi tusiwe tunawaombea maana sala hazitafika kwa kuwa sio mapenzi ya Mungu bali mapenzi ya binadamu
 
Jamani msitake kutafuta mchawi kwa hii ajali.

Kwa kuangalia tu kwa macho Gari la Marehemu utaona wazi hakuwa amefunga mkanda (safety belt) wakti anaendesha gari. Vile vile mwendo kasi na hakuwa na uzoefu wa kutosha kuendesha gari kwa mwendo mrefu.

Kifupi hakufata sheria za uslama barabarani.

Asitafutwe mchawi kwa hilo. Kosa lake hakufata sheria za usalama barabarani

kwa mara ya kwanza umeongea point
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom