Kifo cha Mfanyakazi kiwanda cha A to Z Arusha chaibua taharuki kubwa.

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Hali ya taharuki imeibuka katika kiwanda cha kutengeneza vyandarua cha A to Z kilichopo kisongo jijini Arusha mara baada ya kuibuka kwa taarifa za kifo cha mmoja ya Wafanyakazi katika kiwanda hicho.

Taarifa zimedai kuwa baadhi ya Wafanyakazi kiwandani hapo wamezimia kwa kukosa Hewa na mmoja wapo Amepoteza maisha, jambo ambalo uongozi wa a to z umekanusha na kudai si kweli na hakuna tukio kama hilo.

Mmoja ya viongozi wa A to Z, Aberd Edwin ameezeza Kuwa kuna mfanyakazi wao aitwaye Charles Magimbi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kulazwa katika kituo cha afya cha Levolosi jijini hapa.

Aberd amedai kuwa Magimbi ambaye alikuwa kiongozi katika idara ya kushona tisheti (Gametic )alifikwa na mauti baada yakuwa amelazwa katika Hospital hiyo akisumbuliwa na maradhi ya tumbo , ndipo usiku wa leo akawa amefariki dunia.

Amesema baada ya taarifa hiyo ya kifo cha kiongozi wao kuwafikia ,Wafanyakazi waliopo katika idara hiyo waliangua kilio huku wakipiga kelele kwa nguvu jambo ambalo limesababisha taharuki hiyo.

"Ni kweli kuna mfanyakazi wetu amefariki dunia ila si Kwa kukosa hewa taarifa hizo si za kweli ila Mfanyakazi huyo alikuwa naumwa akawa ameenda kutibiwa na baadae kulazwa katika Hospital ya Levolosi na asubuhi ya leo Wafanyakazi wamepata taarifa za kifo chake na kupata kiwewe"Amesema Aberd.
 
Mbona kiongozi(Bashite)wa Dar es Salam yeye bado yupo.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Viwanda vingi Sana Tanzania havijaajiri watu wa mazingira na usalama mahali pa kazi, watu wengi Sana wanaumia na kupata matatizo makubwa Sana viwandani bila kupewa stahiki zao
 
Back
Top Bottom