Kifo cha Mchungaji Dkt. Rwakatare: Rais Magufuli atuma salamu za pole. Asema alikuwa Mcha Mungu mwenye kupenda amani

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Wanafamilia, Wabunge na Waumini wa Kanisa la Mlima wa Moto (Mikocheni B Assemblies of God) kufuatia kifo cha Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatare.

Rais ameeleza kusikitishwa na Kifo cha Mchungaji huyo ambaye amesema alikuwa mcha Mungu, mwenye upendo, asiye na majivuni, aliyepigania umoja na amani na aliyeipenda nchi yake kwa dhati.

Amesme “Katika kipindi hiki cha majonzi tumuombee Askofu Rwakatare apumzike mahali pema peponi na nawasihi Waumini wa Kanisa la Mlima wa Moto muendelee kuwa wamoja na muendeleze mazuri yote yaliyofanywa na Askofu Rwakatare wakati wa uhai wake”

EWCYFwuWAAENxoI.jpg
 
Mcha Mungu?!
Tuwe wakweli jamani
'Binadamu umavumbi na mavumbini utarudi......
Huyu Mungu Huyu tuendelee kumtukuza
 
Kuwepo katika ulingo huu WA JF yahitajika kuwa na moyo mvumilivu haswaa, Ujinga na utoto ni mwingi kuliko uhalisia, Kuna watu wanaweza kumpangia hata Mungu nini afanyie kazi na kipi asifanye Duh!!

Kuna mwingine huruma Hana, hata kukitokea jirani yake ama binadamu mwenzake kafa anafanya sherehe ili hali hata yeye Kesho aweza kuzikwa,!!
 
Tatizo CORONA inaatack mwili na kukufanya ushindwe kupambana na magonjwa mengine kama BP, Kisukari, TB, Malaria, Kaswende, Kifaduro, Malaria etc. Yaani watu wengi sasa watasombwa na magonjwa hayo mengine baada ya mdudu COVID19 kufanikiwa kuingia mwilini...
 
Tuache unafiq alikuwa na uchaMungu gani?
Wakati ndio walewale waliotaka na kushabikia mauaji ya Zitto
 
Mbunge viti.maalumu CCM Dr Rwakatare Kafariki akiwa na miaka 70 akiwa na nguvu zake, pesa na biashara kibao kitu ambacho vibibi vingi na vibabu vya chadema vya umri huo rekodi hiyo havifikii vinakuwa vijinga jinga Fulani tu


Hheheh! Ndesamburo alifariki ameacha nini?badala ya kuiga njia alizopita unatupondea chadema...!
 
Back
Top Bottom