Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 6,376
- 6,709
Tukio la kuchomwa visu na kufa kwa mbunge mmoja wa Uingereza Sr David Amess kimefichua ubaguzi wa wazi wa kimfumo wa wazungu. Pamoja na muuaji kukamatwa, bado wanasema kitendo hiki si cha kigaidi. Kama muuaji angekuwa siyo mzungu polisi wangemmaliza kwa risasi. Wala wasingeendelea kushikilia kuwa hawajajua kama tukio hili ni la kigaidi ama la. Zaidi, wasingeficha jina la mhusika kama angekuwa siyo mzungu. Kwa wanaowaona wazungu kama watu wasio wabaguzi na watenda haki, hapa kuna somo kubwa tu. Kwa waliowahi kuishi au wanaoishi Ulaya na Marekani hata nchi nyingine kama vile za Asia au Amerika ya kusini hata Australia, watakubaliana na ukweli kuwa wazungu ni wabaguzi na wenye upendeleo wa wazi hata kufikia kulinda uhalifu kama huu aliofanyiwa huyu mbunge. Tukio jingine la la kijana mmoja nchini Norway ambapo kijana mmoja wa kizungu ametumia mishale kuwaua watu watano na kujeruhi wawili. Hakuuawa na polisi na bado wanasema eti alikuwa radicalized na siyo gaidi. Haki iko wapi hapa?