Kifo Cha Mbatia Chaibua Mapya:inadaiwa Alilengwa Zitto

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,503
1,225
kama mtu anataka kuficha identity kwa tz sio kazi ngumu.. sim cards zinauzwa kama peremende na mtu anaweza kuwa na line ya simu akaitumia kwa kazi flani then akaitelekeza. ishu ya PRIVATE NUMBER inafanya kutilia mashaka ukweli wa hii habari

najua watanzania bado sana,evrythin is possible,nipe namba yako nikutumie Sms ikiwa na private.kwa mfano unapata message ya kutoka Mobipawa,na inaandika sender mobipawa.

piga huduma kwa wateja tigo namba 100,na uulize,basi kwa taarifa yako na ujumbe ulitumwa kwa waandishi tutawaleta,
haogopwi mtu hapa JF
 

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,503
1,225
Wapendwa,
huwezi kutuma sms ikatokea private namba, never ever.Jaribu kutunga kitu kingine.

baba paroko karibu katika uwanja wa Mapambano,hilo jambo linawezeana,na nitaomba nikupe ushauri,siku zote fanya utafiti kabla ya kutoa kauli,Kwa msaada zaidi piga huduma kwa wateja tigo,voda au celtel na uulize jambo hili..

sasa unataka kumtete naibu waziri kwamba hakutuma ujumbe huu???
 

Saharavoice

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,198
2,000
Technologia za kisasa kila siku zinakuja na mpya, sms with hiding number might be possible!!!

Njia nyingine kama niko right, unatuma sms kupitia mtandao wa internate (kuna web zinatoa hiyo huduma like Wadja.com n.k)
 

Rwabugiri

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
2,776
1,195
Jamani jamani mbona inatisha na kuvuta usikivu?

Kweli siasa mchezo mchafu! lakini huyu muuaji mpaka lini? Ee Mungu tunusuru!
 

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,747
0
Unajua Uzuri Ni Kwamba Mwanakijiji Anazo Contacts Za Zitto Na Itakuwa Vizuri Akimuita Kijijini Kwake Na Amuhoji Hayo Maswali Ili Tumsikie Mwenyewe Zitto Akisema Otherwise Wengine Itatuwia Vigumu Sana Kuamini Maana Wapishi Wa Habari Jf Wapo Wengi !!

Kitu Simpo, Mwanakijiji Muite Zitto Na Umuulize !
 

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,747
0
Hapa kuna haja ya kufanya mambo matatu ama manne ili kujua nini kinaendelea.

1.kama ni kweli kuwaw kuna kiongozi aliwapigia simu waandishi wa habari asubuhi saa nne na kuwaambia kuwa kuna habari kubwa siku hiyo, na pia kama kiongozi huyo aliyepiga simu ni huyu huyu aliyempigia zitto basi kuna haja ya huyo kiongozi kujieleza alikuwa anamaanisha kitu gani.

2. inawezekana asiwe mlengwa ni zitto ila alikuwa sumaye kwani naye pia alikuwepo kwenye msafara ,kuna haja ya polisi kuchunguza jambo hili kwa kina na kulipatia majibu ya haraka kwaqni hii itakuwa ni hatari klwa viongozi wetu.

3.lazima mwanahalisi wawe tayari kuwataja waandishi husika ili kuweza kuupata ukweli wa mambo na kujua nini kilimuua waziri wetu ,huenda naye alikuwa ni mlengwa huyo naye alikuwa big news.

Ni lazima kuujua ukweli kwani habari hii ikiachwa inaweza kuleta hisia mbaya na pia kuwajenga watu kisaikolojia kuwa zitto anataka kuuwawa na hii ni hatari kwa taifa haswa ukizingatia hali halisi ya kisiasa kwa sasa.

Dereva ni lazima atafutwe akiwa hai ili kuweza kuieleza ,mahakama kiini cha ajali na pia ni lazima uongozi wa juu wa jeshi la polisi uwajibike kama unashindwa kumtafuta dereva aliyesababisha kifo cha waziri wa serikali , je?akisababisha kifo cha mlalahoi kama mimi atapatikana?

Usalama wa taifa lazima uingizwe matatani kwani kama habari hizi zina ukweli kuna kila sababu kuwa wanajua kinachoendelea kwenye taifa hili lazima wawajibike kueleza nini kinaendelea kimya kimya kwenye nchi hii.

Nami nitaanza uchunguzi wangu ili kujua nini kilitokea na hata kama ni kwenda hadi kwa familia ya dereva na kujua kama kabla ya siku ya ajali alikuwa amesafiri kwenda wapi na kama hali za maisha ya familia zilikuwa tofauti na siku nyingine ,na hapo nitauweka uchunguzi wangu wazi japo unaweza ukachukua muda mrefu kwani mimi sio mtaalamu wa masuala ya kiuchunguzi.

vizuri saaaana, lakini pia nadhani FULL DETAILS anazo zitto mwenyewe na si mwingine, hivyo itakuwa vizuri kama zitto akija hapa na kutueleza ukizingatia yeye pia ni mwanachama JF !!
 

Atanaye

Senior Member
Oct 31, 2007
153
195
Atanaye,
Zitto alishakuwa maarufu toka kipindi kile tunasoma Mlimani,sasa kusema anatafuta umaarufu sasa ni kumkosea heshima.wewe unataka asiseme kwa sababu itamuongezea umaarufu??

the truth should be told..
Apparently sikuwa nataka kumkosea heshima Mh Zitto vievile nataka aseme tu kwani domocracy is prevailing-na 'umaurufu'was not in my text!
"The original meaning of the word "glamour" was the act of casting a spell over someone, particularly to change how things appeared to them." -na tunajua wanasiasa wanatumia strategies kama hizi! According Webster's dictionary "seemingly mysterious allure" na labda hii ndio alitaka apate focus ya magazeti na television ili apate forum ya wakuwataja mafisadi, au?;) na vilevile and I quote "The primary modern meaning of the word relates to fascination, charisma, beauty, or sexual attraction." Sidhani Zitto anweza kumpita J.K by this definition!!!;) Therefore in contextGlammer remains ambiguos!
.Source:Webster+Answers.com
 

Kweku

Member
Nov 3, 2007
14
0
Hii kali. Tatizo ni je kuna ushahidi? au zitto kuchelewa kidogo ilkuwa ni coincidence tu
 

Mwanagenzi

JF-Expert Member
Sep 11, 2006
690
1,250
Je, haiwezekani kuwa aliyempigia Zitto ni David, ambaye pia alikuwa karibu na eneo la tukio?
 

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,553
2,000
Wana JF,
Nilizungumza na mwandishi wa MwanaHalisi na kumweleza ya kwamba siamini kama ajali ile ilipangwa. Ninaamini ni ajali kama ajali nyingine tu. Kuendekeza habari hizi ni hatari sana kwa utulivu wa nchi. Nilimwambia hivyo mwandishi. Ajali ikitokea na nikapoteza maisha, ni mipango ya mungu. Wala sitembei nikiogopa kuwa nitauwawa. Siogopi hata kidogo.
Ni kweli nilipigiwa simu na naibu waziri. Lakini haihusiani hata kidogo na ajali. Mimi kama kiongozi ninawasiliana na viongozi mbalimbali. Sasa kama kiongozi akinipigia simu halafu ikatokea ajali na nikasema yeye ndio kapanga, basi sitakuwa ninawasiliana na viongozi.
MwanaHalisi limekwenda out of the way. Na nimewasialiana na Mhariri wake juu ya hili.
 

Rwabugiri

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
2,776
1,195
Wana JF,
Nilizungumza na mwandishi wa MwanaHalisi na kumweleza ya kwamba siamini kama ajali ile ilipangwa. Ninaamini ni ajali kama ajali nyingine tu. Kuendekeza habari hizi ni hatari sana kwa utulivu wa nchi. Nilimwambia hivyo mwandishi. Ajali ikitokea na nikapoteza maisha, ni mipango ya mungu. Wala sitembei nikiogopa kuwa nitauwawa. Siogopi hata kidogo.
Ni kweli nilipigiwa simu na naibu waziri. Lakini haihusiani hata kidogo na ajali. Mimi kama kiongozi ninawasiliana na viongozi mbalimbali. Sasa kama kiongozi akinipigia simu halafu ikatokea ajali na nikasema yeye ndio kapanga, basi sitakuwa ninawasiliana na viongozi.
MwanaHalisi limekwenda out of the way. Na nimewasialiana na Mhariri wake juu ya hili.

Asante Mh Zitto kuliweka wazi hili na kutuondolea hofu iliyo anza jengeka. Hata hivo lisemwalo lipo kama halipo li njiani ni vyema ukawa makini tu ndugu, kwani siku zote 'Kinga ni bora kuliko tiba'

Japo bado husemwa 'ajali haina Kinga' ila ukiwa mwangalifu zaidi katika mawasiliano yako na kupunguza kujieleza zaidi ya wapi ulipo uwapo safarini hasa kwa watu usio na uhakika nao, utajifunza mengi na kuepusha mengi pia.

Mungu wetu akutangulie siku zote.
 

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,727
2,000
Wana JF,
Nilizungumza na mwandishi wa MwanaHalisi na kumweleza ya kwamba siamini kama ajali ile ilipangwa. Ninaamini ni ajali kama ajali nyingine tu. Kuendekeza habari hizi ni hatari sana kwa utulivu wa nchi. Nilimwambia hivyo mwandishi. Ajali ikitokea na nikapoteza maisha, ni mipango ya mungu. Wala sitembei nikiogopa kuwa nitauwawa. Siogopi hata kidogo.
Ni kweli nilipigiwa simu na naibu waziri. Lakini haihusiani hata kidogo na ajali. Mimi kama kiongozi ninawasiliana na viongozi mbalimbali. Sasa kama kiongozi akinipigia simu halafu ikatokea ajali na nikasema yeye ndio kapanga, basi sitakuwa ninawasiliana na viongozi.
MwanaHalisi limekwenda out of the way. Na nimewasialiana na Mhariri wake juu ya hili.

Asante sana Zitto, comments zako zimetoa majibu ambayo bila shaka yamefunga mjadala; kwa hili inaonekana Mwanahalisi wameipika story ili kuuza gazeti kwa kutumia jina lako. Kama Mhariri wa Mwanahalisi ni muungwana inampasa aombe radhi otherwise credibility ya gazeti lake iko ukingoni.
 

Mkereketwa

JF-Expert Member
May 19, 2007
202
0
Hoja ni kwamba Mh Zitto mwenyewe aje atoe hiyo issue. Vile vile mkuu hapo juu mimi najua kwambaunaweza kutuma SMS na ikatokea unknown kwa kutumia internet kama MSN, SKYPE, FREECALL, VOIB etc.
 

mambo

JF-Expert Member
Jun 11, 2007
2,374
2,000
Mheshimiwa wangu,mkereketwa tumeambiwa tuwe tunasoma kabla ya kujibu hapa forum na wazee wazima,zitto ameshajibu hapo juu.pls soma.
 

Domo Kaya

JF-Expert Member
May 29, 2007
531
0
ndio hiki kitu kinawezeakana,wewe ndio haufahamu nini cha kufanya..nenda karibu na huduma kwa wateja ya kampuni yoyote ya simu..

Jamani msitufanye sisi wana JF ni washamba sana. Hakuna system inayoweza kutumika mtumaji message akaifanya message anayotuma isisome number na ionyeshe private number, nadhani mwandishi au mtoa habari amejichanganya.

Wana JF mnapotoa habari hakikisheni hiyo habari inaweza kuwashawishi watu waiamini... sio unasikia watu wakijadili na wewe unaileta hapa bila ya kuwa na uhakika na unachokiandika.

Sielewi mleta habari huyu alikuwa namaanisha nini:

Je dereva wa FUSO alilipwa ili atengeneze ajali?
- na kama kweli alilipwa je ni shillingi ngapi mpk auze maisha yake.

Je ni imani za kishirikina?
- na kama ni imani za kishirikina je waganga ndio waliitengeneza ajali?????
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom