Kifo cha mama mjamzito Lindi (kwa gari ya wagonjwa kuishiwa mafuta) serikali inachukua hatua gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifo cha mama mjamzito Lindi (kwa gari ya wagonjwa kuishiwa mafuta) serikali inachukua hatua gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchaichai, May 24, 2012.

 1. m

  mchaichai JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 650
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [Mnamo tarehe 23/05/2012 katika kijiji cha Rutamba mama mjamzito alifariki kwa gari ya kituo uishiwa mafuta njiani ili hali wizara ya afya inatengewa fedha za kutosha na wadau wengi tu wa maendeleo wanachangia mfuko wa afya ili kupunguza vifo vya akina mama wajawazito hasa maeneo ya vijijini kwa nchi nzima je hii ni haki? na Je katika hili wizara na serikali ya mkoa ichuke hatua gani za kitaaluma na kisiasa dhiki wa wahusika wakuu katika idara ya Afya?
   
 2. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hebu elezea ilikuaje ili tujue tatizo ni wizara,halmashauri,DMO,dereva,wahudumu wa afya au mama mjazito aliyefariki?
   
 3. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Vyovyote iwavyo, wizara ndiyo msimamizi wa masuala yote ya afya; watoe majibu
   
 4. mzalendokweli

  mzalendokweli JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii ni kutuonyesha kua maisha yetu yako hatarini kila mahali. Km kwenye Afya kuko hivi kwenye Elimu kukoje?
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  wazira ajiuzuru kama vipi tukusanye sahihi 70 dr mwinyi apige nyama chini kutokana na kifo hiki
   
 6. N

  Nabwada Senior Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nadhani kuna tatizo upande wa Transport Office,budget ya mafuta imechakachuliwa au Dereva kaiba Mafuta kwenye Gari.Nahisi moja kati ya hayo.Pia haya Magari ya Wagonjwa mara nyingi wanaoyatumia huwa ni wazima hawaumwi,wanamaliza mafuta hao.POLE KWA WOTE WALIOFIKWA NA MSIBA HUU ukiosababishwa na uzembe.
   
 7. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,309
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Chonde chonde wanandugu. Asilimia 99 mwenye tatizo hapo ni Dereva. I am sorry to say this. Madereva wa serikali wanaiba mafuta ni noma. Hakuna udhibiti hata kidogo. Hata kumaliza wizi serikalini ni pamoja na serikali kujuwa hili. Wana majumba mazuri na huwezi amini. Wizi wa mafuta wa kupindukia. Mungu amlaze mahala pema Mama mjamzito na Mtoto wake.
   
 8. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Mkuu neno wizard ya Afya inatengewa fungu la kutosha nadhani sio sahihi kabisa! Jaribu kufatilia swala hili kwa ukaribu ujue kosa limeokea wapi! Kwa budget ya Afya bado ni ndogo na haitoshi ukizingatia tumeongeza wanaotakiwa kupata huduma bure, watoto chini ya miaka 5, wajawazito, wazee na wenye magonjwa sugu. Mara ngapi tumesikia dawa hakuna hospitali? Let us think loudly
   
 9. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  huku ni kuvuka mipaka. waziri awajibishwe kwa makosa ya kituo cha afya? kwanza vituo viko chini ya halmashauri na si wizara ya afya.
   
Loading...