Kifo Cha Kanumba: Wengi Kupandishwa Kizimbani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifo Cha Kanumba: Wengi Kupandishwa Kizimbani

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Allien, Apr 14, 2012.

 1. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2012
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145


  Source: Gazeti la Mwanaspoti

  [​IMG]

  Kanumba's body being escorted to the Leaders grounds  MSANII wa muziki wa Bongo Flava, Ali Kiba, anadaiwa kuhojiwa na polisi kwa maelezo ndiye aliyempa Elizabeth Michael Lulu msaada wa usafiri (lifti) baada ya kutoka kwa Steven Kanumba.

  [​IMG]

  Lulu ndiye anayetuhumiwa kuhusika na kifo cha Kanumba kilichotokea usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita.

  Kachelo aliyemhoji Lulu Jumatatu wiki hii, amedai kuwa msanii huyo alihojiwa katika kituo cha Polisi cha Oysterbay kutokana na kutajwa na mtuhumiwa kuwa ndiye aliyempatia lifti baada ya kutoka kwa Kanumba.

  Mwandishi wa habari hizi alimtafuta Ali Kiba ili azungumzie taarifa hizo, alipopatikana kwa njia ya simu, msanii huyo alisema: Samahani kaka siwezi kuzungumzia chochote kuhusu mambo hayo. Kisha akakata simu.

  Lulu alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jumatano wiki hii na kutotakiwa kujibu chochote kwa vile mahakama hiyo haina uwezo wa kisheria wa kusikiliza kesi za mauaji.

  Lulu alitoa maelezo yake polisi Jumatatu ikiwa ni saa 65 tangu kutokea kwa kifo cha Kanumba., ambapo alizungumza na kachero wa Makao Makuu ya Polisi ambaye pia ana taaluma ya saikolojia.

  Taarifa za uhakika ambazo zimepatana kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinaonyesha kuwa kachero huyo (jina tunalo) aliyetoka makao makuu alifanikiwa kufanya mahojiano na binti huyo ambaye awali aligoma.

  Imeelezwa kuwa, alitumia takribani sasa tatu kumlainisha Lulu azungumze.

  Katika mahojiano na gazeti la The Citizen Jumanne, kachero huyo ambaye alitoka katika Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Jinai alisema tayari amemhoji mtuhumiwa namba moja Lulu pamoja na msanii huyo maarufu wa muziki wa kizazi kipya kufuatia kifo cha Kanumba, aliyefariki usiku wa kuamkia Jumamosi.

  Akimnukuu Lulu katika mazungumzo yake, kachero huyo alisema Lulu aliitwa na marehemu Kanumba ili waweze kutoka (out) kwenda kwenye bendi ya Mashujaa ambayo ilikuwa inapiga kwenye kiwanja chao cha nyumbani, Vingunguti.

  Mtuhumiwa alionekana kutokuwa tayari, lakini marehemu akamlazimisha.

  Kachero huyo alisema: Lulu anadai alifika nyumbani kwa marehemu saa tano usiku, lakini akiwa ameweka msimamo wa kutokwenda sehemu yoyote usiku ule, lakini Kanumba alikuwa akilazimisha ndipo yakatokea mabishano na marehemu akafunga mlango kwa funguo.

  "Hata hivyo, baada ya ugomvi wa kama nusu saa hivi, Lulu alifanikiwa kuondoka chumbani humo na alifungua mlango kwa taharuki na kuondoka bila kujua kilichotokea nyuma, huku akimweleza ndugu wa marehemu kwamba Kanumba ameanguka."

  Mpashaji habari wetu huyo alisema, kumekuwa na jumbe fupi za maneno kutoka kwa wanasiasa ambazo zimekuwa zinaingia kwenye simu ya kiganjani ya Lulu, zikiahidi kumsaidia.

  Alionya kuwa kama wanasiasa wataanza kuingilia uchunguzi wa Polisi katika kesi hiyo ambayo imevuta hisia za watu wengi, wanaweza kuharibu mambo. Lakini yeye mwenyewe akionyesha kwamba yuko imara na anafahamu anachokifanya.

  Kuhusu msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba, kachero huyo alisema kwamba alihojiwa kutokana na kutajwa na mtuhumiwa kama mtu aliyempatia msaada wa usafiri (lifti) baada ya kutoka kwa Kanumba.

  Kachero huyo alisema kutokana na taarifa ambazo wanaendelea kuzipata, kuna uwezekano watu wengi zaidi wakahojiwa ili kujiridhisha kabla ya watuhumiwa kuanza kupandishwa kizimbani baada ya upelelezi

  Source: Gazeti la Mwanaspoti
   
 2. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2012
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  RIP The Great Kanumba!
   
 3. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hapo cjaona jipya
   
 4. serio

  serio JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 5,925
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  Ali k denied that shit,
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hapa sielewi. Kwamba katoka bila kujua kilicho tokea nyuma lakini bado alijua Kanumba kadondoka?
   
 6. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  hivi makachero wanaruhusiwa kutoa taarifa kama hizi kwa waandishi wa habari wakati uchunguzi ukiendelea?
   
 7. roby2006

  roby2006 JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 399
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Tutasikia mengi sana kuhusu hili
   
 8. Mangimeli

  Mangimeli JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  uzushi mwingine nao, lulu ni mtuumiwa na yupo mahabusu iweje awe na simu mahabusu?
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Yale yaleeeeeeeeee!
   
 10. T

  Teko JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2012
  Joined: Jul 3, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Hata mimi hapo sijaelewa,inawezekanaje?
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  Apr 15, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Tuachie police wafanye kazi yao..ni mapema mno kuanza kuunganisha dot
   
 12. Crucial Man

  Crucial Man JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 3,276
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  mbona ni yale yale ya siku zote.sijaona jipya.
   
 13. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #13
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Mpashaji habari wetu huyo alisema, kumekuwa na jumbe fupi za maneno kutoka kwa wanasiasa ambazo zimekuwa zinaingia kwenye simu ya kiganjani ya Lulu, zikiahidi kumsaidia.


  Mangimeli, kwamba sms zinaingia katika simu ya Lulu haimaanishi lazima awenayo mahabusu
   
 14. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #14
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280

  cartura huna habari JF inamakachero wakali zaidi ya siri-kali, au unataka kuwadharau? Tehe tehe tehee!
   
 15. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #15
  Apr 15, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  nilidhani ni wale wa serikali, kumbe ni wa JF?
   
Loading...