Kifo cha Kanumba: Ni uzembe tu? Sio Lulu!

There you are!

Kanumba kama kioo cha jamii anajua kabisa , HAJATOA POSA, HAJATOA MAHARI, HAJAJITAMBULISHA KWA WAZAZI WA LULU, na hajaweka wazi kwa jamii......anakaa na kitoto kidogo na kulala nacho....( ameanza naye urafiki huu tangu ka binti kakiwa na miaka 14) just imagine.....

muda huo saa sita usiku, still walikuwa wanataka watoke kwenda club?????????

oh...no wait... a minute...The guy was stupidy!! Lulu is little ***** its known

kuwalaumu watu wengine kama unavyosema is not fair.....

wazazi wanapaswa kulaumiwa wakianzia na mama wa Kanumba......28 yrs bado anahitaji sana malezi hata kama tutasea amekua!!! he neded strong hand to lead him...mama Lulu aliishajichokea na mtoto wake...ulimwengu sasa umechukua nafasi
Maaaan! JF ya miaka mitano nyuma...
 
Na huyo ni Waberoya wa miaka mitano nyuma, Waberoya wa leo usimshangae akiandika Makonda oyeeee!!
Hahahaa Matola wakati napitia huu uzi kuna mtu enzi hizo alikuwa timamu ila siku hizi nikijaaliwa kuingia humu huwa naruka mabandiko yake, kafyatuka mazima! Sijui watu zile akili nani kawashikia aisee! Kajisemea Paskali nchi hii uking'ang'ana na ukweli utaonekana an 'enemy of the people'
 
NazDaz, kinachofuata ni mimi kufanya petition niwe registered nitoe msaada wa kisheria nisaidie watu kama hawa!. Kama brother Ditto (rip) aliyafanya aliyoyafanya na akapewa dhamana, wako mamia kwa maelfu wanaoozea jela kwa kukosa huduma hizi. Ukiimagine haka kabinti kalivyo na akili za ki 'wema sepetu", halafu ukawafikiria wana jela wetu!, kanahitaji serious rescue efforts soonest!.

Bado tunakuhitaji uwasaidie “ mamia kwa maelfu wanaokosa huduma’hizo’ “!

Sio wote waliopo jela wana hatia ! Tuwasaidie Chief!

Keep your Word!!
 
Wanabodi,

Kwanza tuendelee kupeana pole kwa msiba wa mpendwa wetu Stephen Kanumba "The Great".

Leo nimeisikia taarifa ya awali ya polisi ikielezea mwili wa marehemu umekutwa na jeraha kichwani na kushikiliwa kwa binti msanii Lulu Michael mwenye umri wa chini ya miaka 18 kuisaidia polisi katika uchunguzi huo!. Taarifa rasmi ya daktari kuhusu chanzo kilichosababisha kifo bado haijatolewa!.

Hili ni jukwaa la jamii inteligence likijikita zaidi kwenye facts na sio hisia na hoja hapa sio kupeana pole za msiba wala kumtetea huyu binti Lulu ambaye anataka kibebeshwa msalaba wa kifo cha Kanumba kama mhusika mkuu wakati ukweli halisi ni japo kifo hupangwa na Mungu, lakini kuna kila dalili zinazoonyesha kifo cha Kanumba japo kimesababishwa na ajali ya kuanguka na kujigonga, kinaweza kuwa kimechangiwa na uzembe wa watu fulani fulani ambao kama wangefanya the right thing at the right time, labda saa hizi tungekuwa tunazungumza mengine na sio huyu binti wa watu Lulu who is under 18 kutaka kubebeshwa msalaba kwa kunyooshewa vidole. (Hii mada kwanza nilipost kule jamii inteligence ikagoma)

Hoja hii inafuatia maswali mengi bila majibu ya ni nini haswa kilichotokea hiyo jana!.

Wewe kama uu mmoja wa mashabiki wa Kanumba na mpaka sasa una uchungu mkubwa na kifo hiki, nakushauri usichangie uzi huu maana utakosa objectivity na impartiatility kutokana na huzuni.

Hoja za msingi ni hizi.
1. Ugomvi ulitokea saa 6 usiku na mpaka majirani walisikia kelele za watu wanaogombana. Mwili umefikishwa hospitali ya Muhimbili saa 11 Alfajiri, nini kilitokea hapo kati?.

2. Mdogo wa marehemu aliyejitambulisha kama Bosco aliyekuwa nyumbani ikiishi na Kanumba, na wakati wa ugomvi alikuwepo nyumbani, ameongea kwenye TV kuwa aliposikia ugomvi chumbani, akaenda kutaka kuingilia mlango ukafungwa kwa ndani, akaendelea kusikia vishindo vya wagombanao ambavyo hata majirani walivisikia, what did he do?, au mlango ukishafungwa kwa ndani huku unajua kabisa kuna ugomvi, basi ni kujiachia tuu liwalo na liwe?. Hapa sio kuna uzembe fulani?!.

3. Baadae Lulu akaufungua mlango na kutoka kama alivyozaliwa na kumweleza Bosco kuwa Kanumba ameanguka hiyo ilikuwa ni around saa 6 usiku, huyo Bosco ulikwenda chumbani na kumkuta Kanumba kama alivyozaliwa anagalagala chini huku povu likimtoka mdomoni, what did he do first?.

4. Anasema alimpigia simu daktari wake!. Hivi kweli unaitwa chumbani na kumuona mtu ameanguka anavuja damu anatapatapa, wewe utamtafuta kwanza daktari wake au kazi ya kwanza ni kuita msaada wa kumbeba na kumkimbiza mgonjwa hospitali ya karibu?. Pale kwa Kanumba mpaka hospitali ya Sinza Palestina ambayo ni 24/7 ni only 5 minites away!. Tukio limetokea saa 6 usiku mwili unapelekwa Muhimbili 11 alfajiri!. Kulitokea nini hapo?!. Hapo sio kuna uzembe fulani?!.

5. Hivi ni kweli Kanumba alikuwa na daktari wake?. Jee alikuwa ana tatizo fulani linalomtokea mara kwa mara kiasi kwamba kuna daktari maalum ndio huwa anaitwa anamhudumia hali iliyolazimisha lazima kwanza huyo dakitari atafutwe kokote aliko, asubiriwe yeye tuu ndipo Kanumba apate huduma ya kwanza?!. Kama tukio ni saa 6, daktari alipigiwa simu saa ngapi?, na alifika saa ngapi?, kumbukeni muda wote huo Kanumba anagalagala na kuvuja damu nyingi kumsubiria daktari wake afike?!. Huu sio uzembe fulani?.

6. Tunaelezwa daktari alipofika ndipo juhudi za kumkimbiza Muhimbili zikafuatia, huku kukipatikana tarifa za baadhi ya wasanii kufika hapo kwa Kanumba within minutes na wengine kukiri walimkuta mwili umeshaanza kuwa baridi, jee muda gani ulishapita toka tukio la kuanguka mpaka hao wasanii/majirani waliofika mwanzo and what did they do?!. Hapa kweli hakuna uzembe fulani?.

7. Tumeonyeshwa picha na TBC zikionyesha umati mkubwa wa wasanii ukiandamana kuupeleka mwili wa Kanumba Muhimbili, huku wakishindana kuupiga picha!, ikumbukwe wakati tukio linatokea, Kanumba alikuwa kama alivyozaliwa ila mwili ulionekana kwenye TV ukibebwa ni umevishwa nguo maridadi, hivyo ni emergence ya aina ile ambayo mwili umekutwa ni wa baridi, unavishwa nguo ndipo mgonjwa anakimbizwa hospitali?! Kikawaida mgonjw mwenye emergence huwa anawahishwa hospirali hivyo hivyo alivyo, kama alikuwa hajavaa anafunikwa tuu shuka ili kuwahishwa hospitali, kupatikana muda mpaka kumvisha na kuita wasanii na waandishi kwanza, huu sio uzembe fulani?!.

8. Kama tukio ni la dharura tulitegemea watu wa kwanza ni majirani iweje wasanii wajazane kivile usiku huo mpaka na waandishi wa TBC?. Haiwezekani baada ya kutokea ajali hiyo ya kuanguka, badala ya kumpatia mgonjwa huduma ya kwanza ya kujaribu kuokoa maisha ya Kanumba kwa kumuwahisha hospitali, watu walikuwa bize kuwatafuta masuper star na waandishi wa habari wawahi tukio lile huku wengine wakiendelea kuhangaikia kuupiga picha mwili wa Kanumba licha ya kujua tayari ni dead body?!. Huu ni utu?!.

9. Kama hao waliofika wakamshika na kuona mwili umeanza kuwa baridi, ni muda gani daktari alifika?. Ni muda gani walijua Kanumba ameshafariki?, kama alifia nyumbani hawakujua hiyo sasa at that point ni police case badala ya kuitana makundi ya wasanii na kuidramatise scene ya kifo cha Kanumba?!.

10. Mwisho kwa sababu ripoti ya daktari kutaja chanzo cha kifo haijatoka, naombeni tusimbebeshe mtoto watu Lulu msalaba wa kifo cha Kanumba!. Inawezekana ni Kanumba mwenyewe aliteleza, na hata kama ni kweli alimsukuma, kama alimsukuma in self defence, Lulu hana hatia yoyote kwa sababu kifo kitakuwa kimetokea kwa bahati mbaya bila kusudio la kutenda jinai ya mauaji na kifo hupangwa na Mungu tangu ile siku Kanumba anazaliwa, Mungu aliishampagia siku yake ya kifo na atakufaje! .

RIP SK The Great

Paskali
Leo ni imetimia miaka 10, toka kifo cha nyota huyu wa Bongo Movies, Steven Kanumba, na mpaka Leo, sio tuu pengo lake halijazibika, bali hajapatikana star mwingine yoyote wa kuvaa viatu vyake vikamfiti.

RIP Steven Kanumba, tutakukumbuka milele!.
Paskali
 
Back
Top Bottom