Kifo Cha Kanumba: Ni Uzembe Tuu? Sio Lulu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifo Cha Kanumba: Ni Uzembe Tuu? Sio Lulu!

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Pascal Mayalla, Apr 8, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Kwanza tuendelee kupeana pole kwa msiba wa mpendwa wetu Stephen Kanumba "The Great".

  Leo nimeisikia taarifa ya awali ya polisi ikielezea mwili wa marehemu umekutwa na jeraha kichwani na kushikiliwa kwa binti msanii Lulu Michael mwenye umri wa chini ya miaka 18 kuisaidia polisi katika uchunguzi huo!. Taarifa rasmi ya daktari kuhusu chanzo kilichosababisha kifo bado haijatolewa!.

  Hili ni jukwaa la jamii inteligence likijikita zaidi kwenye facts na sio hisia na hoja hapa sio kupeana pole za msiba wala kumtetea huyu binti Lulu ambaye anataka kibebeshwa msalaba wa kifo cha Kanumba kama mhusika mkuu wakati ukweli halisi ni japo kifo hupangwa na Mungu, lakini kuna kila dalili zinazoonyesha kifo cha Kanumba japo kimesababishwa na ajali ya kuanguka na kujigonga, kinaweza kuwa kimechangiwa na uzembe wa watu fulani fulani ambao kama wangefanya the right thing at the right time, labda saa hizi tungekuwa tunazungumza mengine na sio huyu binti wa watu Lulu who is under 18 kutaka kubebeshwa msalaba kwa kunyooshewa vidole. (Hii mada kwanza nilipost kule jamii inteligence ikagoma)

  Hoja hii inafuatia maswali mengi bila majibu ya ni nini haswa kilichotokea hiyo jana!.

  Wewe kama uu mmoja wa mashabiki wa Kanumba na mpaka sasa una uchungu mkubwa na kifo hiki, nakushauri usichangie uzi huu maana utakosa objectivity na impartiatility kutokana na huzuni.

  Hoja za msingi ni hizi.
  1. Ugomvi ulitokea saa 6 usiku na mpaka majirani walisikia kelele za watu wanaogombana. Mwili umefikishwa hospitali ya Muhimbili saa 11 Alfajiri, nini kilitokea hapo kati?.

  2. Mdogo wa marehemu aliyejitambulisha kama Bosco aliyekuwa nyumbani ikiishi na Kanumba, na wakati wa ugomvi alikuwepo nyumbani, ameongea kwenye TV kuwa aliposikia ugomvi chumbani, akaenda kutaka kuingilia mlango ukafungwa kwa ndani, akaendelea kusikia vishindo vya wagombanao ambavyo hata majirani walivisikia, what did he do?, au mlango ukishafungwa kwa ndani huku unajua kabisa kuna ugomvi, basi ni kujiachia tuu liwalo na liwe?. Hapa sio kuna uzembe fulani?!.

  3. Baadae Lulu akaufungua mlango na kutoka kama alivyozaliwa na kumweleza Bosco kuwa Kanumba ameanguka hiyo ilikuwa ni around saa 6 usiku, huyo Bosco ulikwenda chumbani na kumkuta Kanumba kama alivyozaliwa anagalagala chini huku povu likimtoka mdomoni, what did he do first?.

  4. Anasema alimpigia simu daktari wake!. Hivi kweli unaitwa chumbani na kumuona mtu ameanguka anavuja damu anatapatapa, wewe utamtafuta kwanza daktari wake au kazi ya kwanza ni kuita msaada wa kumbeba na kumkimbiza mgonjwa hospitali ya karibu?. Pale kwa Kanumba mpaka hospitali ya Sinza Palestina ambayo ni 24/7 ni only 5 minites away!. Tukio limetokea saa 6 usiku mwili unapelekwa Muhimbili 11 alfajiri!. Kulitokea nini hapo?!. Hapo sio kuna uzembe fulani?!.

  5. Hivi ni kweli Kanumba alikuwa na daktari wake?. Jee alikuwa ana tatizo fulani linalomtokea mara kwa mara kiasi kwamba kuna daktari maalum ndio huwa anaitwa anamhudumia hali iliyolazimisha lazima kwanza huyo dakitari atafutwe kokote aliko, asubiriwe yeye tuu ndipo Kanumba apate huduma ya kwanza?!. Kama tukio ni saa 6, daktari alipigiwa simu saa ngapi?, na alifika saa ngapi?, kumbukeni muda wote huo Kanumba anagalagala na kuvuja damu nyingi kumsubiria daktari wake afike?!. Huu sio uzembe fulani?.

  6. Tunaelezwa daktari alipofika ndipo juhudi za kumkimbiza Muhimbili zikafuatia, huku kukipatikana tarifa za baadhi ya wasanii kufika hapo kwa Kanumba within minutes na wengine kukiri walimkuta mwili umeshaanza kuwa baridi, jee muda gani ulishapita toka tukio la kuanguka mpaka hao wasanii/majirani waliofika mwanzo and what did they do?!. Hapa kweli hakuna uzembe fulani?.

  7. Tumeonyeshwa picha na TBC zikionyesha umati mkubwa wa wasanii ukiandamana kuupeleka mwili wa Kanumba Muhimbili, huku wakishindana kuupiga picha!, ikumbukwe wakati tukio linatokea, Kanumba alikuwa kama alivyozaliwa ila mwili ulionekana kwenye TV ukibebwa ni umevishwa nguo maridadi, hivyo ni emergence ya aina ile ambayo mwili umekutwa ni wa baridi, unavishwa nguo ndipo mgonjwa anakimbizwa hospitali?! Kikawaida mgonjw mwenye emergence huwa anawahishwa hospirali hivyo hivyo alivyo, kama alikuwa hajavaa anafunikwa tuu shuka ili kuwahishwa hospitali, kupatikana muda mpaka kumvisha na kuita wasanii na waandishi kwanza, huu sio uzembe fulani?!.

  8. Kama tukio ni la dharura tulitegemea watu wa kwanza ni majirani iweje wasanii wajazane kivile usiku huo mpaka na waandishi wa TBC?. Haiwezekani baada ya kutokea ajali hiyo ya kuanguka, badala ya kumpatia mgonjwa huduma ya kwanza ya kujaribu kuokoa maisha ya Kanumba kwa kumuwahisha hospitali, watu walikuwa bize kuwatafuta masuper star na waandishi wa habari wawahi tukio lile huku wengine wakiendelea kuhangaikia kuupiga picha mwili wa Kanumba licha ya kujua tayari ni dead body?!. Huu ni utu?!.

  9. Kama hao waliofika wakamshika na kuona mwili umeanza kuwa baridi, ni muda gani daktari alifika?. Ni muda gani walijua Kanumba ameshafariki?, kama alifia nyumbani hawakujua hiyo sasa at that point ni police case badala ya kuitana makundi ya wasanii na kuidramatise scene ya kifo cha Kanumba?!.

  10. Mwisho kwa sababu ripoti ya daktari kutaja chanzo cha kifo haijatoka, naombeni tusimbebeshe mtoto watu Lulu msalaba wa kifo cha Kanumba!. Inawezekana ni Kanumba mwenyewe aliteleza, na hata kama ni kweli alimsukuma, kama alimsukuma in self defence, Lulu hana hatia yoyote kwa sababu kifo kitakuwa kimetokea kwa bahati mbaya bila kusudio la kutenda jinai ya mauaji na kifo hupangwa na Mungu tangu ile siku Kanumba anazaliwa, Mungu aliishampagia siku yake ya kifo na atakufaje! .

  RIP SK The Great

  Paskali
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Good analysis!!
   
 3. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 499
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Pasco,

  Asante kwa tafakuri ya kina. I think namba moja hapo juu, kuna maelezo mengine kuwa kutoka hapo nyumbani marehemu alipelekwa hospitali ya Mwananyamala ambako nafikiri ndiyo alikuwa declared dead. MNH ilikuwa kuhifadhi mwili wa marehemu.....
   
 4. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nalo hilo neno!
   
 5. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2012
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Mkuu wangu huwa una pupa sana wakati mwingine. Kuwa na subira report kamili za dakatari na uchunguzi zitoke na some facts zi-unfold. Huwa unapenda sana kuhukumu na kutabiri lakini mara nyingi hoja zako zinaangukia pua.

  Wape watu nafasi ya kuomboleza na kukumbuka mazuri na mengine baada ya kuzikwa. Kuwa Binadamu.

  Wewe si ndo ulikuwa unapiga kelele kipindi cha marehemu Regia kuwa apumzishwe kwanza kabla ya mengine?

  Stop double standards.
   
 6. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  yap, kifo kimetokana na ukosefu mkubwa maarifa ya kuelewa priorities.
   
 7. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe kwamba Lulu asibebeshwe lawama kwenye hiki kifo.

  Pia nakubaliana na wewe kuwa kuna uzembe uliotokea mahali ndiyo maana huyu Bwana akafariki, ukweli ni kwamba watanzania wengi hatuna ufahamu juu ya kutoa Huduma ya Kwanza. Kuna uwezekano mkubwa sana kama angepatiwa huduma ya kwanza mapema basi angeweza kuishi au la, basi ingesaidia kupunguza baadhi ya maswali ambayo tunajiuliza wakati huu..

  Aidha ni kwamba Daktari alipaswa kuwapa muongozo wa nini wafanye wakati yeye yuko njiani anakuja.
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  nimeipendz analysis yako......

  Ambacho mpaka sielewi dakika hii ni kwa nini wamsubiri daktari ambaye hakuwa na usafiri wakati wangeweza kumwahisha hospitali ya karibu? Ni uzembe uliofanywa na kaka mtu na majirani kwa ujumla.....
   
 9. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Mkuu you sound like Sherlock Holmes.The point is she is not guilty until proven otherwise.
   
 10. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,410
  Likes Received: 1,968
  Trophy Points: 280
  Kweli wewe una pupa haya uliyoeleza ni mapya kabisa . Tutasikia mengi.
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Kutoka hapo Sinza mpaka M'nyamala, wameacha hospitali ngapi za huduma 24/7 hapo kati?. Jee juhudi hizi za kumuwahisha hospitali was it the first priority au kuwaita kwanza daktari na wasanii?.
   
 12. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Unapopigana tegemea kufa au kuumia...biblia inasema"mshahara wa dhambi ni mauti"ukweli lulu ana kesi ya kujibu.
   
 13. B

  Blac kid JF-Expert Member

  #13
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 3,366
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  kwa nini lulu na mdogo'ake kanumba wasingesaidiana kumpa huduma ya kwanza? Lulu hakwepeki kwenye hizo lawama, iweje atoe tu taarifa na kukimbia asitoe ushirikiano kumpatia msaada kanumba! Mimi nasema lulu hawezi kujinusuru ktk hzo lawama.
   
 14. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #14
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Suala la kuchelewesha Kanumba kwenda hospitalini au kumpa huduma ya kwanza linajulikana kwa Kanumba tu kwa sababu tulikuwa tunamjua. Ukweli ni kwamba Watanzania tuna tatizo hili. hata zinapotokea ajali mara nyingi huwa tunawachelewesha majeruhi kwenda hospitali mwisho wake ni kilio.

  Mimi sio daktari wala polisi ila siamini kama Lulu anahusika kwenye kifo cha KN,hapa najiuliza Lulu ana nguvu gani mpaka amsukumize Kanumba adondikee Kisogo, nakumbuka KN alihojiwa na mikasi siku moja na akaulizwa anacheza karate/judo akasema ameshacheza sana na akasema mtu asije kichwa kichwa. Hapa nitaamini kama KN alikuwa amelewa na aliteleza au kuna nguvu ya ziada ambayo Lulu aliipata bila kujua. Lakini mpaka sasa naamini Lulu ana bahati mbaya ambayo huwezi kuilinganisha hata iliyowahi kumpata marehemu Ditoplie. Ingawa sisemi kama Ditopile naye alifanya makusudi, najua kwamba kuna wakati sisi wanadamu tunakumbwa na hali ambayo baadaye inakufanya ujute kwa nini tulifanya vile.Hapa ndipo nasema Dunia ni pana kuliko tunavyoichukulia. Hata mim,wewe na yule yanaweza kutukuta, ndio maana nasema ni bora tuzidi kumuomba Mungu ili Yeye atuepushe na Kikombe hicho. Ni vizuri pia wakati tukimuomba Mungu tuache pia starehe za dunia kama Ulevi, uzinzi na kwenda kwenye starehe najua ni gumu lakini ndio ukweli wenyewe.

  Binafsi naamini Lulu kakibeba Kikombe hicho bila kukusudia,kutegemea au kujua na hii ndio mitihani ya Dunia hii, hii husababushwa na mengi sana aidha kama ni fundisho baada ya kuonywa sana na wanadamu au Upana wa Dunia yetu.
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Allien, nakubalia na wewe, kunapotokea msiba, tuwaache waombolezaji wamlilie marehemu wao na wazike ndipo tuje kujadili nini kilitokea!. Kwa Regia ni ajali ya gari, lakini kwa Kanumba japo pia ni ajali, kuna mkono wa mtu, kilichopelekea hii hoja kuletwa hata kabla ya maziko ni finger pointing kwa haka kabinti Lulu as if she is the cause!.

  Hapa zijahukumu, wala sijatabiri kama kule Arumeru, hapa nimetoa angalizo, there is more to it than finger poiting towards one direction , one person Lulu!. Kwa mwendo huu, kufika hiyo J.4, haka kabinti kanaweza kuwa tayari kameishahukumiwa hukuma ya umma!.

  Poleni wafiwa, vidole tusinyoosheane!.

  Pasco.
   
 16. Catch-22

  Catch-22 Member

  #16
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naomba kuuliza mtu akipata majeraha anatibiwa hospitali au mpaka ende na fomu ya polisi? (PF3?)
   
 17. D

  Dedii Member

  #17
  Apr 8, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 76
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  kifo cha kanumba kinauhusiano na freemason, soon itakuwa wazi.
   
 18. bht

  bht JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Mpaka PF3 form, sijui kama kuna exceptions Ila kwa uelewa wangu ni hivyo.
   
 19. COURTESY

  COURTESY JF-Expert Member

  #19
  Apr 8, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 2,018
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Masikini lulu,nahisi she has a curse,namuonea huruma sana huyu mtoto,ana bahati mbaya sana
   
 20. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #20
  Apr 8, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Mkuu Pasco,
  Katika hili mie sina haja ya kutafuna maneno!! Hata kama nimehuzunishwa na kifo, bado napinga kwa nguvu zote huyu binti kuhusishwa na hiki kifo! Ikumbukwe kwamba, Kanumba kwa Lulu ni Kama Daud kwa Golliath…..!! Sina shaka yoyote kwamba, kutokana na wivu wa kimapenzi, Marehemu alianza kumshushia kisago Lulu! Bila shaka, kwa jinsi wanaume tulivyo, asilimia kubwa ya wengi wetu tungechukua uamuzi wa marehemu wa kuanza kumshushia binti kipigo!
  Kwa upande mwingine, Lulu alikuwa na haki ya kujitetea! Kama nilivyosema hapo awali, Lulu kwa Kanumba ni sawa na Daud kwa Golliath! Ninachomaanisha, asingeweza kuchapana nae hivyo suluhisho pekee kwake ilikuwa ni kujinasua toka mikononi mwa marehemu! Kama chumba kisingekuwa kimefungwa (may be kilifungwa ili kichapo kitolewe sawasawa na asiwepo wa kukimbia) basi suluhisho la Lulu lingekuwa kutimua mbio! Lakini kwavile mlango ulikuwa umefungwa, Lulu alilazimika kwanza ,kumsukuma marehemu ili apate nafasi ya kutimua mbio na kufungua mlango! Jambo hili, lingefanywa na yeyote yule with exception of very few! Hata ningekuwa mimi, nisingekuwa na njia mbadala zaidi ya hiyo ya kumsukuma Kanumbe ili nipate uchochoro wa kutimua mbio! Hivyo, vyovyote iwavyo, Lulu hakuwa na namna zaidi ya hiyo ingawaje ni bahati mbaya hatua yake ya kujiokoa imezaa mauti kwa mwenzake!

  Tukija kwa mdogo wake Kanumba, huyo ndie mpuuzi kuliko wote….!!! Nazani ujinga kama sio upumbavu aliofanya ni kutaka kujaribu kuifunika hii issue kwavile aliona ingekuwa skendo kwa kaka yake!! Bila shaka, wakati akichelea kuchukua hatua ya kumpeleka hospitali au kuita majirani (ili kuficha skendo) kumbe ndo alikuwa anakaribisha kifo kwa kaka yake! Na hata hiyo hatua yake ya kuanza kwanza kumuita "daktari" wa Kanumba ilikuwa na lengo lile lile la kuficha skendo!
  WASWAHILI WANASEMA, MFICHA MARADHI KIFO UMUUMBUA……hiki ndicho kilichotokea kwa Mpendwa wetu Kanumba!!

   
Loading...