Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,500
Nimejiuliza na kufikiria sana sana kuhusu kifo cha Rais Magufuli kilichosababishwa na mfumo wa umeme wa moyo uliokuwa unaratibiwa na pacemaker/defibrillator.

Kujiuliza na kufikilia kwangu kumetokana onyo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Marekani (Department of Homeland Security-DHS) lililotolewa mwaka 2019 linaloonya makampuni yanayotengeneza pacemaker/defibrillator kuhusu hatari ya kifaa hicho kudukuliwa na wataalam wa udukuzi na kupelekea hata kifo kwa watu waliopandikizwa kifaa hicho.

Ukitaka kusoma onyo hilo unaweza kugonga hapa;
Link>>> Pacemakers and Hacker Dangers

Wizara hiyo ilibainisha kuwa wadukuzi wanaweza kuingilia mifumo ya pacemaker/defibrillator na kuweza kubadilisha mawasiliano yake ambapo inaweza kupelekea mtu aliyewekewa kifaa kufariki.

Wizara hiyo ilienda mbali zaidi na kusema hata wadukuzi ''mwenye uwezo mdogo'' wanaweza kudukua pacemaker/defibrillator na kufanikiwa kuleta madhara makubwa kwa watu waliopandikizwa vifaa hivyo kwa sababu vifaa hivyo havina mfumo wa uhakiki au idhini (authentication or authorization) ambao ni kinga ya mwanzo dhidi ya udukuzi.

Onyo hili lilipelekea watoa huduma ya afya nchini Marekani kuwaita wananchi wa Marekani zaidi ya nusu milioni waliopandikizwa vifaa hivyo na kuwaeleza ukweli wake.

Kama kifaa hiki kinaweza kudukuliwa hata na wadukuzi wenye uwezo mdogo na kuleta madhara au kifo, inafikirisha sana kusikia kifo cha Rais Magufuli kimesababishwa na mfumo wa umeme wa moyo uliokuwa unaratibiwa na pacemaker/defibrillator. Bear in mind, Rais Magufuli amekuwa na hii pacemaker/defibrillator kwa zaidi ya miaka 10. Why now?

Inafikirisha zaidi baada ya kusoma makala iliyoandikwa na Tundu Lissu kupitia gazeti la Afrika ya Kusini liitwalo Maverick akidai alidokezwa kuhusu hali ya Rais Magufuli na chanzo cha ''uhakika'' kutoka Marekani tarehe 6 Machi.

Ukitaka kusoma makala hiyo gonga hapa;
Link>>> OP-ED: Tanzania’s five years of devastation under the presidency of John Pombe Magufuli

Ukiyachanganua maelezo ya Tundu Lissu utagundua kuwa chanzo cha ''uhakika'' walijua wamefanikiwa ''mission'' ya kudukua hasa baada ya Rais Magufuli kwenda katika hospitali ya Muhimbili tarehe 6 Machi kutibiwa ambapo inaonekana daktari/madaktari walitoa siri hiyo nje lakini baada ya kutoka Muhimbili siku ya pili hawakujua yuko wapi kutokana na usiri wa hali ya juu wa ulinzi wa Rais Magufuli.

Hata gazeti ya Kijasusi liitwalo Africaintelligence halikuweza kujua aliko na likadai habari zinazosema yuko Kenya au India sio za kweli kwa sababu limefanya uchunguzi na kugundua sio kweli.

Kama chanzo cha kifo cha Rais Magufuli kitakuwa ni kudukuliwa kwa pacemaker/defibrillator, hii itakuwa ni aibu na udhaifu mkubwa kwa vyombo vilivyopewa mamlaka ya ulinzi na usalama wa taasisi ya Urais nchini Tanzania. Taasisi ya Ulinzi na Usalama inawezekana ilikuwa imejikita katika ulinzi wa mwili(Physical security ) pekee bila kujiandaa kwenye ulinzi wa saibenetiki(cybersecurity).

Kuna baadhi ya watu watajiuliza, kwa nini pacemaker/defibrillator ya Rais Magufuli idukuliwa kwa sasa?

Mtu mwenye upeo mkubwa atajua muda huu ndio ulikuwa ni muda mwafaka kiujasusi baada ya uchaguzi mkuu 2020 kwa sababu nguvu zilizokuwa zimewekezwa katika Uchaguzi Mkuu 2020 ili kumuondoa Rais Magufuli madarakani kwa njia ya sanduku la kura au maandamano kupitia kwa Tundu Lissu kutofanikiwa.

Ukisikiliza sauti ya tatu utagundua kuwa Tundu Lissu aliwaaminisha ''majasusi'' ana uwezo wa kumtoa Rais Magufuli madarakani kwa kura au maandamano.

Ieleweke kuwa, katika baadhi ya misheni hasa za kijasusi zenye changamano na tata huwa kuna mpango(plan) zaidi ya mmoja. Baada ya mpango wa kwanza kushindwa, mpango wa pili ulichukua nafasi yake na kufanikiwa!

Nadhani hoja za kinadharia kutoka kwa baadhi ya wanasiasa hasa wabunge za kutaka kubadilisha katiba ya Tanzania ili kumuongezea Rais Magufuli muda wa Urais pia zimeharakisha sana ''mission'' hii kabla hawajaanza kuandika ''miswaada binafsi'' na kupeleka bungeni kwa sababu ungepitishwa bila kikwazo chochote!

Mission accomplished, the rest is history!

NOTA BENE.
Kwa wasiojua, pacemaker/defibrillatorni ni kifaa kidogo cha umeme chenye ukubwa kama kiberiti ambacho hufuatilia na kudhibiti wimbo wa moyo ambacho huingizwa kwenye kifua ili kufuatilia na kudhibiti sauti ya moyo isiyo ya kawaida ili kusukuma damu kwa kiwango kinachotakiwa.
Screenshot (67).png
 
Hiyo makala niliisoma vizuri.

lakini kuna point moja umeruka sehem. kifaa hicho mawimbi yake ni mafupi mno kiasi kwamba mtu lazima awe so close kuweza ku access hiko kifaa.

Nut in real sense. the way rais alifichwa. ilikuwa ni ngumu sana. kama PM na mawaziri hawakujua, nani angemsogelea rais zaid ya walinzi wake na madkatari wa usalama?

Plus Tanzania hatufikia uwezo wa hacking kiasi hiko. bado tuna safari ndefu.

All in all our late president aliondoka kwa tatizo la moyo. hizi theory sijui ilikuwa hivi ilkkuwa vile hazimrudushia uhai.

Wanausalama walishatoa sababu. Apumzike kwa amani
 
Hakuna sehemu nimesema Lissu kamuua Magu!

Conspiracy? YES!
So you admit ni conspiracy? okay so its not real.

Lissu yeye alipata formal information kuwa rais ana hali mbaya.. baadae akiwa ameondoka. sio eti kama hacked. ameondoka na nn na nn sababu hapo hakujua.

So badala ya ku stick kutunga empty theories na whitch hunt hapa..
tumuenzi kwa mazuri aliyotenda our late president.
 
Kwa hiyo hata W. Kijazi aliyekuwa KMK alikuwa na pacemaker? Kama KMK alikufa kwa ugonjwa wa moyo na hakudukuliwa basi hata jemadari angeweza kufa kwa ugonjwa wa moyo na ndicho tulichoambiwa.

Na hata hii homa kali kuna watu wa INSIDE CABINET ya JPM wamepata. Mfano ni Mpango. Mpango ni inside cabinet wa JPM. Aliugua homa. Kweli unaweza kupata corona halafu marafiki wako wa karibu wakakosa?
 
Back
Top Bottom