Kifo cha Hayati Dkt. Magufuli kimeipasua CCM. Je, huu ndio wakati wa wapinzani kutusua kisiasa?

Alitabiri Remy Ongala kuwa Ccm ilishakufa sasa yametimia.

Kuna wanaCcm waliokuwa upande wa hayati JPM wanaona sasa nchi imekamatwa mikononi mwa mafisadi na wezi.

Kuna wanaCcm kumbe walifurahia kifo cha hayati JPM na hii inaonekana alikuwa kikwazo kwao.

Ccm ya sasa imepasuka maana kuna mpasuko mkubwa sana.

Je, sasa ndio wakati muafaka wa sisi wapinzani kuaminiwa na wananchi na kupaa kisiasa?
Hakuna wa kuipasua CCM yote unayoyaona ni mkakati ambao mlio nje hamuwezi kuelewa
 
Nachojiuliza misaada yote kwa HANGAYA alafu tozo zpo pale pale plus kupanda kwa bidhaa ZOTE...walisema bia zmepunguziwa kodi cha ajabu zpo pale pale....mm sjawahi kumkubali Magu but mwanamke hawez kuongoza taifa
Kwa kutokuwepo vyama vya upinzani, vyenye viongozi walio na mtazamo wa kitaifa, badala ya maslahi na agenda binafsi, kushika madara ya Dola ni ndoto ya mchana kweupe.

Kwa CCM, Chama Tawala, matokeo ya hiyo misaada na tozo, kwa maendeleo ya watu na nchi kwa ujumla ndiyo kitakuwa kipimo katika Uchaguzi Mkuu, 2025.

Kuhusu mwanamke kuongoza nchi ni mtihani kwa sababu ya jinsi ya maumbile na majukumu yao. Maamuzi yote huwa siyo yao ni tegemezi ambayo hutegemea aliye karibu naye.
 
Mkuu Kamanda Asiyechoka , hakuna kitu kama hicho!, CCM haina mpasuko wowote!.

Wapinzani wepi hao wa kuaminiwa na wananchi?.
P

This is below your usual standards!! Unasema wapinzani wepi wanaoaminiwa na wananchi, unasemaje kuhusu CCM wasioaminiwa na wananchi?? Au unamaanisha anayeshinda anakuwa ameaminiwa na kila mpiga kura??

Unanishangaza kusema neno “wowote” katika tungo moja na mpasuko! Ni kweli akina kiroboto na wahuni hawana tofauti zozote? Au unamaanisha mgogoro wao haujafikia kuitwa mpasuko??
 
Ni kwel haijapasuka ina ila dereva na konda hawaelewani, na hapa Kati kaongezeka fundi, hakuna anaeonge lugha 1 dereva anawasha gari linawaka ila Moshi mweupe na Kisha gari linatembea kidg linazima, konda yy anasema twende tu, Sasa fundi kaja anatoa solution kuwa Ni lazima tuifumue injini yote tuisuke au kununua mpya, hapo Sasa shida inaanzia,

Abiria wapo tu wanatoa hata hawajui, Kama halitavutwa hli gari kwa kutumia gari lingene,hakuna namna nyingine zaidi ya kufumliwa injini, na Ikiwa hayawezekani yote hayo abilia wengi watakufa kabla ya kufika mwisho kwa kukosa mahitaji, maana wengi wa abilia hawana uwezo wa kumdu ghalama za njiani na hawakuwa na akiba ya kutosha,

Hapo vip PASKALI
Na hapo ndipo mabadiliko ya lazima yatafanyika.
 
This is below your usual standards!! Unasema wapinzani wepi wanaoaminiwa na wananchi, unasemaje kuhusu CCM wasioaminiwa na wananchi?? Au unamaanisha anayeshinda anakuwa ameaminiwa na kila mpiga kura??

Unanishangaza kusema neno “wowote” katika tungo moja na mpasuko! Ni kweli akina kiroboto na wahuni hawana tofauti zozote? Au unamaanisha mgogoro wao haujafikia kuitwa mpasuko??
Good point
 
Tatizo la wapinzani wameendelea kumuongelea mwendazake instead wanatafute namna ya kupambana na Samia itafika Muda 2025 wataendelea kumu attack magufuli ambaye hayupo duniani . Wangeangalia namna ya kudeal na rais aliyepo madarakani . Angekuepo mtikila kwa ishu za muungano ndio angetusua sahizi Kwa kuangalia madhaifu ya muungano ambapo Marais wote ni wazanzibar . Mtu wa bara Hana haki na Znz. Hivi ndio vitu vingemmaliza mama 2025
Good point, tunafeli sana wapinzani.
 
Alitabiri Remy Ongala kuwa Ccm ilishakufa sasa yametimia.

Kuna wanaCcm waliokuwa upande wa hayati JPM wanaona sasa nchi imekamatwa mikononi mwa mafisadi na wezi.

Kuna wanaCcm kumbe walifurahia kifo cha hayati JPM na hii inaonekana alikuwa kikwazo kwao.

Ccm ya sasa imepasuka maana kuna mpasuko mkubwa sana.

Je, sasa ndio wakati muafaka wa sisi wapinzani kuaminiwa na wananchi na kupaa kisiasa?
Kamanda,
CCM ni ile ile.
Kwenye maslahi ya pamoja wanaungana .
 
Tatizo la wapinzani wameendelea kumuongelea mwendazake instead wanatafute namna ya kupambana na Samia itafika Muda 2025 wataendelea kumu attack magufuli ambaye hayupo duniani . Wangeangalia namna ya kudeal na rais aliyepo madarakani . Angekuepo mtikila kwa ishu za muungano ndio angetusua sahizi Kwa kuangalia madhaifu ya muungano ambapo Marais wote ni wazanzibar . Mtu wa bara Hana haki na Znz. Hivi ndio vitu vingemmaliza mama 2025
Pumba
 
Inawezekana ccm ineshakufa tayar ila wapinzani wameshajiozea zaman. Kwahiyo bora tuendelee kuwa na mfu kuliko huyu aliyeoza..

Tanzania bado hatuna chama cha upinzani. Kipindi cha Dr slaa upinzani ulikuwa unajielewa unataka nini ila tangu kipindi kile wapo wapo tu ni wala ruzuku walio oza.
 
Kwa kutokuwepo vyama vya upinzani, vyenye viongozi walio na mtazamo wa kitaifa, badala ya maslahi na agenda binafsi, kushika madara ya Dola ni ndoto ya mchana kweupe.

Kwa CCM, Chama Tawala, matokeo ya hiyo misaada na tozo, kwa maendeleo ya watu na nchi kwa ujumla ndiyo kitakuwa kipimo katika Uchaguzi Mkuu, 2025.

Kuhusu mwanamke kuongoza nchi ni mtihani kwa sababu ya jinsi ya maumbile na majukumu yao. Maamuzi yote huwa siyo yao ni tegemezi ambayo hutegemea aliye karibu naye.
Kuandika rahisi sana. Hebu anzisha hicho chama chako chenye agenda unazoziita za kitaifa tuone. Watu kama wewe walikuwepo enzi za ubaguzi Africa kusini. Kazi yao ilikuwa nikubeza wapigania uhuru kuwa hawana ajenda kama ufanyavyo wewe. Lakini Afrika kusini ileee, ni nchi huru sasa.
 
Alitabiri Remy Ongala kuwa Ccm ilishakufa sasa yametimia.

Kuna wanaCcm waliokuwa upande wa hayati JPM wanaona sasa nchi imekamatwa mikononi mwa mafisadi na wezi.

Kuna wanaCcm kumbe walifurahia kifo cha hayati JPM na hii inaonekana alikuwa kikwazo kwao.

Ccm ya sasa imepasuka maana kuna mpasuko mkubwa sana.

Je, sasa ndio wakati muafaka wa sisi wapinzani kuaminiwa na wananchi na kupaa kisiasa?
Kama Kungekuwa na CHADEMA ya mwaka 2008 had 2013, CCM hii ingepeta tabu sana kipindi hiki. Ila ssa hamna chma cha kuitikisa CCM pamoja na madhaifu yake yanayookena waziwazi.
 
Back
Top Bottom