Kifo cha general Qasem Soleimani ni mpango wa Rais Donald Trump wa kujikinga na mchakato wa kupigiwa kura za kumfukuza kazi (impeachment procedures)

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
NB: PLEASE USIIBE MAKALA YOYOTE YA INFANTRY SOLDIER KATIKA MITANDAO YA FACEBOOK PAMOJA NA WHATSAPP

KIFO CHA GENERAL QASEM SOLEIMAN NI MPANGO WA DONALD JOHN TRUMP KUJIKINGA NA MCHAKATO WA KUPIGIWA KURA ZA KUMFUKUZA KAZI (IMPEACHMENT PROCEDURES)

IMG_20200121_122752_977.jpg

Spin Doctor ni moja kati ya mbinu za kijasusi na propaganda ambazo wanasiasa na watu maarufu hutumia mbinu hiyo kwa lengo la kuwasahaulisha wananchi juu ya kashfa fulani mbaya kwa kuzua tukio jingine.

Hapo wananchi wanasahau tukio la nyuma na kuweka akili zao kwenye jambo jingine ambalo limezuka ghafla. Hapo kiongozi fulani atatumia vyombo vya habari na wanasiasa wa upande wake ili kuwazubaisha wananchi wake.

Kiujumla Spin Doctor hujikita zaidi katika kumpandisha chati kiongozi fulani na kuwafanya wananchi wasahau mabaya yake.

Mwezi December mwaka 2019 vyombo vya ulinzi na usalama nchini Marekani vilitoa ripoti yenye zaidi ya kurasa Mia tatu yenye kueleza uovu wa raisi wa 45 wa Marekani DONALD
JOHN TRUMP.

Ripoti hiyo ilipitishwa kwenye Bunge la wawakilishi (House of Representatives) chini ya mwanamama mtata Bi Nancy Pelosi. Vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama Marekani kama CIA na vyombo vingine nyeti vilifanya uchunguzi huru dhidi ya Raisi Trump na kubaini makosa yafuatayo.

1. Raisi Donald Trump alinaswa akifanya mawasiliano na Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky ili serikali ya Ukraine imchunguze makamu wa Raisi wa zamani wa Marekani enzi za Obama ndugu Joe Biden na mwanae Hunter Biden. Simu hiyo ilipigwa tarehe 25/7/2019 kuanzia saa tatu na dakika tatu asubuhi hadi saa tatu na dakika thelathini na tatu asubuhi.
Joe Biden huenda akagombea Urais kupitia chama cha Democratic hivyo Trump alitaka kujua kashfa zake ili amuangamize mapema.

2. Raisi Trump analizuia Bunge kufanya kazi zake kisheria mfano mwaka 2019 tarehe 4/7 Kwenye maazimisho ya miaka 243 ya uhuru wa Marekani DONALD TRUMP alimtaka spika wa Baraza la wawakilishi Nancy Pelosi kuidhinisha kiasi cha Dola million kumi kwa sherehe za uhuru, Nancy Pelosi aligoma, kitu kingine ni fedha za ujenzi wa ukuta mpakani mwa Marekani na Mexico kwenye jambo la Texas.

3. Matumizi mabaya ya vyombo vya ulinzi na usalama, mfano kuna maafisa wa CIA Trump aliwatuma kwenda Ukraine kuonana na Raisi wa nchi hiyo ndugu Volodymr Zelensky. Maafisa hao Trump aligoma wasihojiwe kwenye tume ya watumishi wa idara za ujasusi na intelijensia.

4. Lugha chafu kwa watumishi wa umma mfano wafanyakazi ofisi mbalimbali ikulu na sehemu nyingine nyeti.

5. Ufisadi ndio maana baadhi ya watu wake wa karibu wako jela akiwemo mwanasheria wake wa zamani Michael Cohen.

6. Raisi Trump ana matatizo ya akili yaani kulingana na jinsi anavyoongea na kutafsiri mambo mbalimbali.

7. Raisi Trump anatoa siri za serikali na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii kama Twitter.

8. Rushwa, Raisi Trump kwenye uchaguzi wa Urais mwaka 2016 alitumia zaidi ya Dola za Marekani Milioni sita kwenye matangazo kupitia Facebook na twitter.

9. Kuhusu uchaguzi wa Marekani kuingiliwa na Urusi bado ni mnyukano wa hoja na upelelezi kati ya CIA na FBI, Kuna ushahidi kwamba huenda serikali ya Urusi ilidukua mfumo wa mawasiliano kwenye uchaguzi lakini hakuna ushahidi wa moja kwa moja kama ndugu Trump alitoa fedha ili hizo njama zifanyike.

Hoja hizo zilitosha kumng'oa Donald Trump madarakani kwa sababu Baraza la wawakilishi lilibariki zoezi hilo na kuwaachia seneti ambalo ni upper Legislature. Yaani seneti lina nguvu kuliko Baraza la wawakilishi chini ya Nancy Pelosi.

Seneti jana usiku limekula kiapo Cha uadilifu, uaminifu na haki ili kuendesha mchakato wa mwisho wa kura dhidi ya Donald Trump, hivyo mpaka tarehe 21/1/2020 itajulikana kama Trump atafukuzwa kazi au atasalia madarakani.

Raisi wa 37 wa Marekani RICHARD NIXON alijiuzuru mwaka 1974 Kutokana na kashfa ya WALTER GATE SCANDAL yaani kutumia vyombo vya ulinzi na usalama kupambana na maadui zake binafsi bila kujali maslahi ya umma.

Baraza la seneti lina jumla ya maseneta 100.
53 wanatoka chama cha Trump yaani Republic huku 45 wakitoka chama cha Democratic na 2 wakiwa hawana vyama.

Kwakuwa Trump anataka kujisahihisha na kujisafisha mbele ya wananchi wa Marekani na seneti ikabidi amuue Generali Qasem Soleiman kamanda mtiifu na msiri wa Kiongozi wa mashia Iran ALI AYATOLLAH KHAMENEI.

Kwakuwa Marekani, uingereza, Ufaransa, Israel na Saudi Arabia walikuwa wanamtafuta Qasem Soleiman wamuue tangu mwaka 1993 ikabidi Trump ashauliane na Mkuu wa vikosi vya anga Marekani Madam Barbara Barrette na mnamo tarehe 3/1/2020 General Qasem Soleiman aliuawa akiwa Iraq na mwenzake ABU MAHD AL_MUHANDIS kiongozi wa kundi la kijasusi nchini Iraq.

Lengo la Trump kumuua General Qasem Soleiman alikuwa anatafuta huruma kwa wananchi wa Marekani kuelekea uchaguzi, pili kuwasahaulisha wananchi wa Marekani Kuhusu mchakato wa kupigiwa kura na seneti ili afukuzwe kazi, tatu kulinda sera za mambo ya nje ya Marekani. Ikumbukwe kwamba nchi ya Marekani linapokuja suala la kitaifa watu wote huwa kitu kimoja ukiachilia mbali tofauti zao kisiasa, itikadi, falsafa na jiografia.

Hivyo Ndugu Donald Trump amechanga karata zake vizuri sana kwa sababu seneti watamuunga mkono na hawawezi kupiga kura za kumfukuza kazi na wananchi wa Marekani watampa kura nyingi sana, kitendo cha Trump kumuua General Qasem Soleiman ni furaha kwa chama cha Republican ambacho maraisi wao waliopita walikuwa makatiri na wahafidhina.

Hii ndio spin Doctor njia ambayo huwaokoa viongozi mbalimbali pale wanapokumbwa na kashfa mbalimbali na huitumia mbinu hii kuwazubaisha wananchi wenye uwezo mdogo wa kutafsiri, kutafakari na kupembua mambo kifalsafa na hao ndio wapiga kura wengi kuliko wanazuoni na wanafalsafa.

Barani Afrika Njia hii imesaidia sana kuwafanya viongozi mbalimbali kukaa muda mrefu madarakani mfano Paul Biya ni raisi wa Cameroon tangu mwaka 1982 na kila ikikalibia uchunguzi Mkuu huwa anakuja na vituko vingi mfano kuwalipia ada wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Cameroon, kutoa mikopo kwa wanawake na kuzusha vurugu ili wananchi wamuonee huruma, vituko hivi huwavuta wananchi wa Cameroon kusahau maovu yake.

Nchini Uganda ndugu Yoweri Kaguta Museveni ni Rais wa Uganda tangu mwaka 1986 mara nyingi huwa anawaandaa wapinzani ili kuonyesha upinzani kuelekea uchaguzi Mkuu mfano Kiza Besigye na Amama Mbambazi pili hata Joseph Kony wa Lord Resistance Army alimuandaa yeye ili waganda wamuonee huruma.

Msanii Boby Wine anateseka sana kwa sababu sio pandikizi la Museveni.
Hiyo ndio spin Doctor njia ya kijasusi yenye propaganda nyingi ili kuwazubaisha wananchi.

Nchini Burundi Mwaka 2015 Raisi wa nchi hiyo ndugu Pierre Nkurunzinza aliandaa mapinduzi bandia yenye mazingaombwe eti GENERAL GODEFROID NIYOMBALE alimpindua, tukio hili lilisababisha wananchi wengi kusahau maovu ya Pierre Nkurunzinza hasa kadhia ya wakimbizi kuihama Burundi na kuja Tanzania.

Nchini Rwanda Raisi Paul Kagame mara baada ya mauaji ya kimbali mwaka 1994, alianza kutumia Spin Doctor dhidi ya Raisi Pasteur Bizimungu.

Mwaka 2000 Raisi Bizimungu aliamua kujiuzuru kutokana na kupewa kesi bandia za matumizi mabaya ya fedha za umma. Tangu mwaka 2000 Kagame ni Raisi wa Rwanda mpaka leo.

NB: PLEASE USIIBE MAKALA YOYOTE YA INFANTRY SOLDIER KATIKA MITANDAO YA FACEBOOK PAMOJA NA WHATSAPP
 
Duniani vilaza hawaishi.yaani kuna mtu kabisa anaweza akaiba makala yako? Kweli tembea uone. Ni ukilaza uliopitiliza.na ujue mtu wa namna hiyo hana shule kabisa.

NB: PLEASE USIIBE MAKALA YOYOTE YA INFANTRY SOLDIER KATIKA MITANDAO YA FACEBOOK PAMOJA NA WHATSAPP

KIFO CHA GENERAL QASEM SOLEIMAN NI MPANGO WA DONALD JOHN TRUMP KUJIKINGA NA MCHAKATO WA KUPIGIWA KURA ZA KUMFUKUZA KAZI (IMPEACHMENT PROCEDURES).

Spin Doctor ni moja kati ya mbinu za kijasusi na propaganda ambazo wanasiasa na watu maarufu hutumia mbinu hiyo kwa lengo la kuwasahaulisha wananchi juu ya kashfa fulani mbaya kwa kuzua tukio jingine.

Hapo wananchi wanasahau tukio la nyuma na kuweka akili zao kwenye jambo jingine ambalo limezuka ghafla. Hapo kiongozi fulani atatumia vyombo vya habari na wanasiasa wa upande wake ili kuwazubaisha wananchi wake.

Kiujumla Spin Doctor hujikita zaidi katika kumpandisha chati kiongozi fulani na kuwafanya wananchi wasahau mabaya yake.

Mwezi December mwaka 2019 vyombo vya ulinzi na usalama nchini Marekani vilitoa ripoti yenye zaidi ya kurasa Mia tatu yenye kueleza uovu wa raisi wa 45 wa Marekani DONALD
JOHN TRUMP.

Ripoti hiyo ilipitishwa kwenye Bunge la wawakilishi (House of Representatives) chini ya mwanamama mtata Bi Nancy Pelosi. Vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama Marekani kama CIA na vyombo vingine nyeti vilifanya uchunguzi huru dhidi ya Raisi Trump na kubaini makosa yafuatayo.

1.Raisi Donald Trump alinaswa akifanya mawasiliano na Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky ili serikali ya Ukraine imchunguze makamu wa Raisi wa zamani wa Marekani enzi za Obama ndugu Joe Biden na mwanae Hunter Biden. Simu hiyo ilipigwa tarehe 25/7/2019 kuanzia saa tatu na dakika tatu asubuhi hadi saa tatu na dakika thelathini na tatu asubuhi.
Joe Biden huenda akagombea Urais kupitia chama cha Democratic hivyo Trump alitaka kujua kashfa zake ili amuangamize mapema.

2.Raisi Trump analizuia Bunge kufanya kazi zake kisheria mfano mwaka 2019 tarehe 4/7 Kwenye maazimisho ya miaka 243 ya uhuru wa Marekani DONALD TRUMP alimtaka spika wa Baraza la wawakilishi Nancy Pelosi kuidhinisha kiasi cha Dola million kumi kwa sherehe za uhuru, Nancy Pelosi aligoma, kitu kingine ni fedha za ujenzi wa ukuta mpakani mwa Marekani na Mexico kwenye jambo la Texas.

3.Matumizi mabaya ya vyombo vya ulinzi na usalama, mfano kuna maafisa wa CIA Trump aliwatuma kwenda Ukraine kuonana na Raisi wa nchi hiyo ndugu Volodymr Zelensky. Maafisa hao Trump aligoma wasihojiwe kwenye tume ya watumishi wa idara za ujasusi na intelijensia.

4.Lugha chafu kwa watumishi wa umma mfano wafanyakazi ofisi mbalimbali ikulu na sehemu nyingine nyeti.

5.Ufisadi ndio maana baadhi ya watu wake wa karibu wako jela akiwemo mwanasheria wake wa zamani Michael Cohen.

6.Raisi Trump ana matatizo ya akili yaani kulingana na jinsi anavyoongea na kutafsiri mambo mbalimbali.

7.Raisi Trump anatoa siri za serikali na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii kama Twitter.

8.Rushwa, Raisi Trump kwenye uchaguzi wa Urais mwaka 2016 alitumia zaidi ya Dola za Marekani Milioni sita kwenye matangazo kupitia Facebook na twitter.

9.Kuhusu uchaguzi wa Marekani kuingiliwa na Urusi bado ni mnyukano wa hoja na upelelezi kati ya CIA na FBI, Kuna ushahidi kwamba huenda serikali ya Urusi ilidukua mfumo wa mawasiliano kwenye uchaguzi lakini hakuna ushahidi wa moja kwa moja kama ndugu Trump alitoa fedha ili hizo njama zifanyike.

Hoja hizo zilitosha kumng'oa Donald Trump madarakani kwa sababu Baraza la wawakilishi lilibariki zoezi hilo na kuwaachia seneti ambalo ni upper Legislature. Yaani seneti lina nguvu kuliko Baraza la wawakilishi chini ya Nancy Pelosi.
Seneti jana usiku limekula kiapo Cha uadilifu, uaminifu na haki ili kuendesha mchakato wa mwisho wa kura dhidi ya Donald Trump, hivyo mpaka tarehe 21/1/2020 itajulikana kama Trump atafukuzwa kazi au atasalia madarakani.

Raisi wa 37 wa Marekani RICHARD NIXON alijiuzuru mwaka 1974 Kutokana na kashfa ya WALTER GATE SCANDAL yaani kutumia vyombo vya ulinzi na usalama kupambana na maadui zake binafsi bila kujali maslahi ya umma.

Baraza la seneti lina jumla ya maseneta 100.
53 wanatoka chama cha Trump yaani Republic huku 45 wakitoka chama cha Democratic na 2 wakiwa hawana vyama.

Kwakuwa Trump anataka kujisahihisha na kujisafisha mbele ya wananchi wa Marekani na seneti ikabidi amuue Generali Qasem Soleiman kamanda mtiifu na msiri wa Kiongozi wa mashia Iran ALI AYATOLLAH KHAMENEI.
Kwakuwa Marekani, uingereza, Ufaransa, Israel na Saudi Arabia walikuwa wanamtafuta Qasem Soleiman wamuue tangu mwaka 1993 ikabidi Trump ashauliane na Mkuu wa vikosi vya anga Marekani Madam Barbara Barrette na mnamo tarehe 3/1/2020 General Qasem Soleiman aliuawa akiwa Iraq na mwenzake ABU MAHD AL_MUHANDIS kiongozi wa kundi la kijasusi nchini Iraq.
Lengo la Trump kumuua General Qasem Soleiman alikuwa anatafuta huruma kwa wananchi wa Marekani kuelekea uchaguzi, pili kuwasahaulisha wananchi wa Marekani Kuhusu mchakato wa kupigiwa kura na seneti ili afukuzwe kazi, tatu kulinda sera za mambo ya nje ya Marekani. Ikumbukwe kwamba nchi ya Marekani linapokuja suala la kitaifa watu wote huwa kitu kimoja ukiachilia mbali tofauti zao kisiasa, itikadi, falsafa na jiografia.

Hivyo Ndugu Donald Trump amechanga karata zake vizuri sana kwa sababu seneti watamuunga mkono na hawawezi kupiga kura za kumfukuza kazi na wananchi wa Marekani watampa kura nyingi sana, kitendo cha Trump kumuua General Qasem Soleiman ni furaha kwa chama cha Republican ambacho maraisi wao waliopita walikuwa makatiri na wahafidhina.

Hii ndio spin Doctor njia ambayo huwaokoa viongozi mbalimbali pale wanapokumbwa na kashfa mbalimbali na huitumia mbinu hii kuwazubaisha wananchi wenye uwezo mdogo wa kutafsiri, kutafakari na kupembua mambo kifalsafa na hao ndio wapiga kura wengi kuliko wanazuoni na wanafalsafa.

Barani Afrika Njia hii imesaidia sana kuwafanya viongozi mbalimbali kukaa muda mrefu madarakani mfano Paul Biya ni raisi wa Cameroon tangu mwaka 1982 na kila ikikalibia uchunguzi Mkuu huwa anakuja na vituko vingi mfano kuwalipia ada wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Cameroon, kutoa mikopo kwa wanawake na kuzusha vurugu ili wananchi wamuonee huruma, vituko hivi huwavuta wananchi wa Cameroon kusahau maovu yake.

Nchini Uganda ndugu Yoweri Kaguta Museveni ni Rais wa Uganda tangu mwaka 1986 mara nyingi huwa anawaandaa wapinzani ili kuonyesha upinzani kuelekea uchaguzi Mkuu mfano Kiza Besigye na Amama Mbambazi pili hata Joseph Kony wa Lord Resistance Army alimuandaa yeye ili waganda wamuonee huruma. Msanii Boby Wine anateseka sana kwa sababu sio pandikizi la Museveni.
Hiyo ndio spin Doctor njia ya kijasusi yenye propaganda nyingi ili kuwazubaisha wananchi.

Nchini Burundi Mwaka 2015 Raisi wa nchi hiyo ndugu Pierre Nkurunzinza aliandaa mapinduzi bandia yenye mazingaombwe eti GENERAL GODEFROID NIYOMBALE alimpindua, tukio hili lilisababisha wananchi wengi kusahau maovu ya Pierre Nkurunzinza hasa kadhia ya wakimbizi kuihama Burundi na kuja Tanzania.

Nchini Rwanda Raisi Paul Kagame mara baada ya mauaji ya kimbali mwaka 1994, alianza kutumia Spin Doctor dhidi ya Raisi Pasteur Bizimungu.
Mwaka 2000 Raisi Bizimungu aliamua kujiuzuru kutokana na kupewa kesi bandia za matumizi mabaya ya fedha za umma. Tangu mwaka 2000 Kagame ni Raisi wa Rwanda mpaka leo.
 
Hata lile shambulio la kumuua Osama Bin Laden,watu walihusisha na mpango wa kutaka kumpa ujiko Obama ili ashinde uchaguzi 2012..USA kila tukio huwa linahusishwa na kitu,ishazaeleka hiyo..
But man,Trump is there to stay,he's nat going anywhere...Mark my word.
 
Thanks
 
Kitendo cha kuandika kuwa mapinduzi ya burundi yalipangwa na Nkurunzinza mwenyewe umefanya nikuone kama mjinga fran hivi anaetamani kuwa jasusi ila hana connection

Sent using Jamii Forums mobile app

Vijana wengi wa siku hizi wapo hivyo. Akisoma habari online akaongeza na anachodhani ndo ukweli basi anaaminisha wengi hivo hivo. Too bad watu wengi hawajui chochote na kuishia kukubali wanachoaminishwa na waandishi “wannabes” uchwara kama huyu
 
Back
Top Bottom