Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,467
- 113,567
Wanabodi,
Wale wa zamani kama mimi mtayakumbuka baadhi ya maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (RIP) akizungumzia upinzani wa kweli, alisema angependa kuona serious oppositions wa vyama viwili au vitatu na sio utitiri wa vyama, japo Mwalimu aliongezea "Upinzani wa Kweli Utatoka CCM!", by now atakuwa ameshabadili msimamo wake ule kwa kutuma salamu kupitia kwa mjukuu wake kuwa " Upinzani wa Kweli, Utatoka Chadema".
Tanzania tunavyo vyama 19 mpaka sasa, na hakuna limit number ya vyama vipya kusajiliwa, hii tayari ni utitiri wa vyama ambao hauna maslahi yoyote kwenye serious opposition zaidi ya kubakiwa na vyama vichache vyenye serious oppositions na vyama vilivyobakia kuwa ni vyama jina tuu, vyama mtu na vyama makaratasi tuu kule ofisi ya msajili.
Nikirudi kwenye vyama serious vya opposition viko vitatu tuu, ukiondoa CCM ambacho ni chama tawala, vyama serious vinabaki kuwa ni CHADEMA, CUF na NCCR MAGEUZI kwa mbali, na kujumlisha 'vyama watu' viwili UDP (ni Cheyo) na TLP (Mrema) ambavyo siviingizi kwenye hesabu ya 2015, just time in between will tell!, vyama vyote vingine vilivyobakia ni vyama jina au vyama makaratasi.
Kufuatia muafaka na CCM, sasa chama cha CUF ni mshirika mkuu wa CCM na juzi nimemona Katibu Mkuu wake, Maalim Seif, akijivinjari jijini Dar es Salaam na matunda ya muafaka, S-Class 3 zikitanguliwa na pikipiki. Hivyo kwa sasa Zanzibar inatawaliwa na chama kimoja kikuu kiitwacho 'Umoja wa Kitaifa' (CCM-CUF).
Kama CUF ina wenye busara, adui mliokuwa mkigombea naye mkate, anapokukaribisha mumegeane huo mkate ambao mwanzo mligombana sana kuugombea, then utaupokea ulikiwa very cautious usije kuwa umetiliwa sumu ya polonium 210 which kills slowly and very softly. "I fear the Greeks especially when they bring gifts.
Kwenye kampeni za 2015, msifikiri tena kama kutakuwa na upinzani wowote wa maana kule Zanzibar, kwa sababu baada ya kuishuhudia hii miaka mitano ya amani, utulivu na ustawi wa Zanzibar, why vote for CCM or CUF any more, just vote for Umoja wa Kitaifa, maana popote utakapopiga kura, it doesn't matter anymore, kama keki tutakula wote kwanini kuigombania!..na huu ndio mwanzo wa kifo cha CUF!.
Tukija CUF bara, kwa vile CUF imefanikiwa kukishauri NCCR-Mageuzi na hivi vyama watu viwili (UDP na TLP) kuunda alliance yao dhidi ya Chadema, kwa maneno mangine vyama hivi vimekubali kuwa vyama vikaragosi vya CCM kupitia mlango wa nyuma wa mgongoni mwa CUF, hivyo kubakiwa na chama kimoja tuu cha upinzani cha kweli nchini ambacho ni Chadema.
Mwanzo niliwalaumu na kuwalaani Chadema, kuunda kambi ya upinzani peke yao, kumbe nilikuwa myopic, sikuweza kuona mbali kwenye bigger picture, niliwaona Chadema ni wabaguzi, wabinafsi na wenye umimi, bila kuifahamu hali halisia ya mambo.
Kupitia michango mbalimbali ya wana JF, nimefunguka macho na sio tuu kuanza kuielewa Chadema, bali kuikubali kuwa ndicho Chama Pekee cha upinzani kwa uchaguzi wa 2015 dhidi ya chama tawala CCM na msharika wake CUF na vyama vikaragosi vyao.
Nasisitiza huu ndio mwanzo wa kifo cha CUF na Neema kwa Chadema, kwa sababu baada ya uchaguzi huu, ruzuku ya mamilioni ya CUF yatakula panga la msajili sambamba na CCM ambayo sasa itakombwa na Chadema, na kama hakutatokea vita vya kimaslahi kugombea ruzuku hivyo (kama ilivyotokea kwa NCCR), na kuitumia kuimarisha chama, then 2015 Chadema itakuwa kwenye the best prospects kuchukua nchi.
Hivyo huu ushirikiano wa CCM na CUF na vikaragosi wao, ni very healthy kwenye safari ya kuelekea kwenye serious opposition kwa vyama utitiri kujifia natural death kwa kufuata kanuni law of the jungle ya 'Struggle for Existance, Survival for the Fittest', CUF inaelekea kufa na maneno ya Mwalimu ya serious oppositions yameanza kutimia.
Angalizo: Paskali sio mtafiti wa siasa bali ni mtazamaji na mfuatiliaji wa masuala ya kisiasa ambaye ana chama chake, ila ametanguliza mbele maslahi ya taifa kuliko kufungamani na siasa za vyama, mshabiki wa baadhi ya watu, some good people ila sio mfuasi wa mtu yoyote, bali mshabiki wa demokrasia ya kweli ndani ya Bunge.
Paskali