Kifo Cha Chacha Wangwe msiba wa Chadema mikononi mwa CCM

George zimmerman

New Member
Jul 23, 2013
2
2
Kifo cha Wangwe:
Msiba wa
CHADEMA
mikononi mwa
CCM
Na Saed Kubenea -
Imechapwa 05 August
2008
KITENDAWILI kuhusiana na
kilichosababisha kifo cha
mbunge wa Tarime, mkoani
Mara, Chacha Zakayo
Wangwe (CHADEMA), bado
hakijateguliwa.
Wangwe, mwanaharakati na
mwanasiasa, alikutwa na
mauti Jumatatu 25 Aprili,
2008, katika kijiji cha
Pendamili, wilayani Kongwa,
mkoani Dodoma, baada ya
gari alilokuwa akisafiri
kudaiwa kupata ajali.
Mbali ya kuwa mbunge wa
Tarime, Wangwe alikuwa
Makamu Mwenyekiti wa
Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) na
Mwenyekiti wa chama hicho
mkoa wa Mara, na Diwani wa
Tarime mjini.
Mengi yamesemwa
kuhusiana na kifo chake.
Kuna waliosema alikufa kwa
risasi na wengine kusema ni
mapenzi ya Mungu tu. Kuna
ya kweli na kuna yaliyotiwa
chumvi.
Hata hivyo, bado kuna
maswali mengi ambayo
hayajapatiwa majibu mpaka
sasa.
Kwanza, katika gari la
marehemu kulikuwa na watu
wangapi? Je, ni kweli kwamba
kulikuwa na mtu mwingine
wa tatu? Yuko wapi sasa?
Suala hili la kuwapo kwa mtu
mwingine wa tatu, mbali na
marehemu na Deus Mallya,
ambaye tayari amekiri kuwa
alikuwa katika gari la
marehemu siku ya tukio,
limeibuliwa na Mwiguni
George, anayedaiwa kufika
eneo la tukio dakika chache
baada ya ajali.
George amethibitisha
kwamba alimkuta marehemu
Chacha akiwa amefunga
mkanda katika kiti cha mbele
kushoto mwa dereva.
Ni yeye aliyesema alimkuta
Mallya akiwa kiti cha nyuma.
Ni George aliyesema Mallya
hakuwa dereva wa gari hiyo,
na kwamba Chacha pia
hakuwa akiliendesha.
Awali Mallya katika maelezo
yake kwa waandishi wa
habari na polisi, alisema
kuwa hafahamu hata
kuendesha gari.? Lakini
hakuna chembe ya mashaka
kwamba Mallya anajua
kuendesha gari, ingawa
inawezekana akawa hana
leseni.
Pili, nani alikuwa wa kwanza
kuijulisha familia ya
marehemu juu ajali hiyo?
Swali hili ni muhimu sana
kutokana na kile
kinachoelezwa kwamba
mmoja wa wake zake
Wangwe, Mariam Chacha
Wangwe, alikuwa miongoni
mwa watu wa awali kabisa
waliojulishwa juu ya tukio
hilo.
Kama alijulishwa na Mallya,
kwa nini basi Mallya
hakuwajulisha kwanza
viongozi wa ngazi za juu wa
CHADEMA? Je, hafahamu
simu zao? Mbona anadai
kuwa anawafahamu? Na
hakika anawafahamu.
Tatu, nani aliyekuwa wa
kwanza kutoa taarifa polisi?
Alipata wapi namba za polisi?
Alipiga namba gani ?zile za
kawaida au alipiga kwa
mmoja wa polisi? Ilichukua
muda gani polisi kufika
kwenye eneo la tukio tangu
ajali kutokea? Mtoa taarifa
alijuaje kama Wangwe
amefariki?
Hili ni muhimu pia kwa
sababu kuna utata wa mtu
aliyetoa taarifa polisi. Huyu
akipatikana anaweza kusaidia
kujulikana taarifa nyingine za
ziada, ikiwamo alijuaje
kwamba Wangwe amepata
ajali na amefariki.
Itajulikana jinsi yeye
alivyopata taarifa. Nani
alimjulisha? Alikuwa wapi
wakati wa tukio? Kama
alikuwa katika eneo la tukio,
ni kweli kwamba Mallya
hakuwa anaendesha gari
linalodaiwa kuwa lilipinduka
na kumuua Wangwe? Kama
ndiyo, nani alikuwa dereva.
Alimuona nani mwingine
ndani ya gari? Huyu
anayedaiwa kuwa alisema,
"Chukua fedha katika koti,"
alikuwa nani? Sasa yuko
wapi?
Nne, nani aliyewajulisha watu
wa Tarime kuhusiana na kifo
cha mbunge wao? Hii ni
muhimu kutokana na ukweli
kwamba watu wa Tarime
walikuwa miongoni mwa
watu wa awali kupewa
taarifa.
Inaelezwa kuwa wapiga picha
hawa walipata taarifa kabla
ya viongozi wa CHADEMA
waliokuwa mita chache
kutoka eneo la tukio.
Tano, mkuu wa mkoa wa
Dodoma, William Lukuvi,
alijulishwa na nani kuhusu
kifo cha Wangwe, hadi naye
akaziamini taarifa hizo na
kumjulisha Waziri wa Mambo
ya Ndani, Laurance Masha,
ambaye naye aliwajulisha
viongozi wa CHADEMA.
Je, Lukuvi alijulishwa na Mkuu
wa wilaya ya Kongwa,
anayesema kwamba alifika
eneo la tukio dakika 30 baada
ya ajali? Kama ni hivyo, yeye
alijulishwa na nani na alijuaje
kuwa ni muda huo tangu ajali
itokee? Alikuwa wapi wakati
huo?
Taarifa kwamba viongozi wa
CHADEMA walijulishwa na
Waziri Masha zimetolewa na
Naibu Katibu Mkuu wa
CHADEMA, Zitto Kabwe.
Sita, zipo taarifa zinazosema
marehemu Wangwe, alikuwa
na kompyuta ya mkononi
(Laptop) na inaelezwa
kwamba siku ya tukio alikuwa
nayo. Je, hivi sasa iko wapi?
Nani anaishikilia?
Inaelezwa pia kwamba
Wangwe alikuwa na silaha ya
kujilinda (bastola). Sasa
anayo nani?
Saba, Deus Mallya ambaye
sasa imethibitika kwamba
alikuwa na marehemu kabla
ya ajali, ni nani hasa?
Anafanya shughuli gani?
Anaishi wapi? Uhusiano wake
na marehemu ni upi na
ulianza lini?
Je, ni kweli kwamba Mallya
amepata mafunzo ya kijeshi,
au mafunzo mengine nchini
Libya? Kama ndiyo, ni
mafunzo yapi na yalichukua
muda gani?
Madai kwamba Deus Mallya
anajua kwa ufasaha lugha ya
Kiarabu yana ukweli gani?
Kama madai haya yana
ukweli, vyombo vya ulinzi na
usalama vinafahamu jambo
hilo? Kwa kiwango gani?
Ni wapi Mallya alijifunzia
lugha hiyo? Nini kilimshawishi
kujifunza Kiarabu? Alitaka
kutumia lugha hiyo kwa kazi
gani?
Nane, viongozi wa CHADEMA
wana uhusiano gani na
Mallya hadi wakadiriki
kumuacha kufuatana na
makamu mwenyekiti wao na
mbunge wao pekee katika
eneo la Kanda ya Ziwa
Viktoria?
Wamemfahamu toka lini na
wapi? Kabla ya hapo
hawakuwahi kumtilia
mashaka? Kama ndiyo ni kwa
kiwango gani? Walichukua
hatua gani?
Tisa, mahusiano ya
marehemu na familia yake
yakoje? Je, walikuwa
wanapikika chungu kimoja na
mdogo wake, Peter Wangwe.
Peter Wangwe alikuwa diwani
kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM) na mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya
Tarime, wakati Chacha
Wangwe akiwa diwani wa
Tarime mjini, kupitia chama
cha NCCR-Mageuzi, mwaka
2000.
Vituko na vitimbi
alivyofanyiwa Wangwe wakati
huo bado vinakumbukwa.
Kwa kile Wangwe
alichopenda kuita, "mtandao
wa viongozi wa CCM,"
alihukumiwa kifungo cha
mwaka mmoja gerezani.
Alitoka gerezani baada ya
viongozi wa CHADEMA, chini
ya mwanasheria Tundu Lissu,
kukata rufaa Mahakama Kuu
kanda ya Mwanza.
Alipotoka gerezani alikuwa ni
Wangwe aliyeandaa kaburi la
kisiasa la Peter, mdogo wake
ambaye alidondoshwa
kwenye nafasi ya diwani na
kupotea kabisa kwenye ngazi
ya uongozi wa CCM.
Hii ndiyo maana kuna
wasioshangazwa na taarifa
kwamba siku ya mazishi
Peter alibeba bango
lililokebehi viongozi wa
CHADEMA na CCM kwa
pamoja kwa kuuliza, "Ni ajali
au risasi?" Ni Peter aliyebeba
bango ambaye anajua
alikopata msamiati wa
"risasi."
Kumi, Wangwe alikuwa
anajiandaa kupeleka hoja
binafsi bungeni kuhusiana na
kile alichoita, "Vitendo vya
mwekezaji katika mgodi wa
North Mara." Mgodi huo
unamilikiwa na kampuni ya
Barrick iliyokumbwa na
mizozo na wananchi katika
maeneo mbalimbali nchini.
Siku moja kabla ya kukutwa
na mauti, Wangwe alimueleza
Spika wa Bunge, Samwel Sitta
kwamba anadhamiria
kupeleka hoja binafsi
bungeni; akisema watu 84
walikuwa wamekamatwa na
polisi katika eneo la
Nyamongo, wilayani Tarime.
Je, mahusiano yake na
wawekezaji waliopo katika
jimbo lake na mkoa wa Mara
kwa ujumla yalikuwaje?
Walikuwa wanaiva? Kama
walikuwa hawaivi, ni kwa nini
na kama walikuwa wanaiva ni
kwa kiwango gani? Je,
mahusiano hayo yaweza
kuhusishwa, kwa aina yoyote
ile, na kifo chake?
Ukiacha yote hayo, msiba
huu umekuja wakati kuna
mnyukano wa uongozi kati ya
Wangwe na wenzake katika
CHADEMA.
Lakini jambo jingine kubwa ni
kwamba msiba ulikuwa wa
CHADEMA, lakini bado
ulikuwa mikononi mwa
makada wa CCM na serikali
yao.
Profesa Samwel Wangwe, ni
Mjumbe wa Halmashauri Kuu
ya Taifa (NEC) na mdogo
wake Peter Wangwe, ni
mmoja wa waumini wa CCM
anayetaka kurejea katika
udiwani wilayani Tarime.
Kutokana na hali hiyo,
hakuna ubishi kwamba
vitimbwi vya aina yoyote
vingeweza kutokea kwenye
mazishi yake.
Katika hoja yake ambayo
alikuwa awasilishe bungeni
kupinga kukamatwa kwa
wapigakura wake 600,
Wangwe anahoji, "Jambo la
kushangaza, hakuna taarifa
yoyote iliyotolewa kueleza ni
vipi wananchi hao waliingia
ndani ya mgodi wenye uzio
na ulinzi mkali wa polisi na
mbwa."
 
chakushangaza Malya leo hii ni mpiga picha wa CHADEMA, huyu mtu na Saa.Nane siwaamini kabisa. :CHADEMA haiko salama at all, kuna ajenda nyingi nyuma ya pazia, ambazo zikiwekwa wazi watu watabaki midomo wazi. alafu video ya soweto arusha mbona haijawahi tolewa!?
 
Ooh...Mwanahalisi.
ipo siku tutakutana tena unipe habari kama zamani? nakutamani na nakuhitaji sasa huwenda kuliko wakati mwingine, tukielekea 2015. fanya hima urudi.
 
Mwanahalisi gazeti linaloeleza ukweli bila upendeleo. Lakini wasiopenda ukweli wamelifungia na hawataki kutoa sababu ila kudhihirisha ubabe wao. Ipo siku itarejea.
 
chakushangaza Malya leo hii ni mpiga picha wa CHADEMA, huyu mtu na Saa.Nane siwaamini kabisa. :CHADEMA haiko salama at all, kuna ajenda nyingi nyuma ya pazia, ambazo zikiwekwa wazi watu watabaki midomo wazi. alafu video ya soweto arusha mbona haijawahi tolewa!?
Ujue katiba ....
 
chakushangaza Malya leo hii ni mpiga picha wa CHADEMA, huyu mtu na Saa.Nane siwaamini kabisa. :CHADEMA haiko salama at all, kuna ajenda nyingi nyuma ya pazia, ambazo zikiwekwa wazi watu watabaki midomo wazi. alafu video ya soweto arusha mbona haijawahi tolewa!?

Ila CDM haina majasusi wa kitaalam, ina ma "baunsa" tu aka watunisha misuli!!!!
 
Mwaka 2005 kipindi Chacha Wangwe anagombea nilikuwa kidato cha 3 lakini nilizunguka vijijini karibia vyote vya jirani kumpigia kampeni huku nikitishiwa kupigwa na vijana wa CCM kwa kitendo changu cha kushiriki siasa, lakini mazuri yote tuliyoahidiwa na mbunge wetu hakuyatekeleza baada ya kukumbwa na umauti ghafla kwa ajali ya gari, mengi yameongelewa lakini kutufuta machozi wanatarime(nikiwemo) naomba mwenye ushahidi wa Wangwe kuuawa na Chadema kama wengi mnavyodai muupeleke polisi kuliko kutawaliwa na mihemuko ya kisiasa na ushabiki binafsi bila ushahidi.
 
subiri wazee wa document waje,ila najuwa hii movie ilichezwa kwa ustadi mkubwa na mbowe,ila sibir watu wa intelijensia wanakuja
 
Mwaka 2015 kipindi Chacha Wangwe anagombea nilikuwa kidato cha 3 lakini nilizunguka vijijini karibia vyote vya jirani kumpigia kampeni huku nikitishiwa kupigwa na vijana wa CCM kwa kitendo changu cha kushiriki siasa, lakini mazuri yote tuliyoahidiwa na mbunge wetu hakuyatekeleza baada ya kukumbwa na umauti ghafla kwa ajali ya gari, mengi yameongelewa lakini kutufuta machozi wanatarime(nikiwemo) naomba mwenye ushahidi wa Wangwe kuuawa na Chadema kama wengi mnavyodai muupeleke polisi kuliko kutawaliwa na mihemuko ya kisiasa na ushabiki binafsi bila ushahidi.

"Mwaka 2015 kipindi Chacha
Wangwe anagombea"
wap!?
 
Mwaka 2015 kipindi Chacha Wangwe anagombea nilikuwa kidato cha 3 lakini nilizunguka vijijini karibia vyote vya jirani kumpigia kampeni huku nikitishiwa kupigwa na vijana wa CCM kwa kitendo changu cha kushiriki siasa, lakini mazuri yote tuliyoahidiwa na mbunge wetu hakuyatekeleza baada ya kukumbwa na umauti ghafla kwa ajali ya gari, mengi yameongelewa lakini kutufuta machozi wanatarime(nikiwemo) naomba mwenye ushahidi wa Wangwe kuuawa na Chadema kama wengi mnavyodai muupeleke polisi kuliko kutawaliwa na mihemuko ya kisiasa na ushabiki binafsi bila ushahidi.
Umeongea na mwenyekiti wako kwanza kabla ya kupost?
 
Lengo kuu la siasa nadhani ilikuwa ni kuhamasisha watu/vikundi vya kijamii kwenye mambo mbali mbali ya kijamii lakini naona sasa kuna kidudu mtu anapandikiza makusudi ama kwa kutojua mbegu chafu ilihali akijua wananchi kwa kiasi kikubwa wamejikatia tamaa ya maisha na wapo kimtego tu kutafuta pa kuanzia...

Hofu yangu ni kwamba ikiwa haya yatafanikiwa si wapishi wala wasambazaji wa chuki na mpasuko huu watakuwa salama,nawaza tu kwa upole!
 
Chacha aliondolewa uhai na wahafidhina. Siku inakuja watajitaja wenyewe kwa majina.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom