Kifo cha CCM ni mafanikio makubwa JK alowapa watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifo cha CCM ni mafanikio makubwa JK alowapa watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by magistergtz, Apr 13, 2012.

 1. magistergtz

  magistergtz JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 282
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna wengi walodai kuwa jk na serikali yake ni legelege. Zipo pia takwimu za kisayansi kuonesha kiwango cha uongozi duni wa jk; mfano ni zile za mfumuko wa bei unaoambatana na kupanda kwa gharama za maisha; kushuka kwa kiwango cha elimu, kushuka kwa morali ya wafanyakazi, kuongezeka kwa utegemezi wa nchi, ufisadi na wizi wa mali za umma, na mengine mengi. Haya yote yako wazi kwa kila mwenye akili nzuri, na mtu huitaji nguvu nyingi kumfanya mtanzania ayaone. Hivo. nakubaliana na takwimu zote hizo ambazo zimewafanya baadhi ya wadau waione serikali ya jk janga la kitaifa.

  Hata hivo, mnyonge mnyongeni, haki yake mpe. Kubali kataa Jk amefanya kazi nzuri ya kuwaepusha watanzania na ccm. Hii kazi ameifanikisha kwa asilimia kubwa na anaendelea vizuri kuikamilisha. Tumpongeze kwa hili maana walau liko wazi kwamba 2015 ccm itazikwa lasmi, na jk mwenyewe agongelea msumari wa mwisho ktk jeneza lake.

  Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki. Jk
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kumlilia mtu kwamba kafa kabla hajafa ni uthibitisho kwamba ataishi muda mrefu.

  Hadi kaburi lichimbwe na kufukia ndipo machozi ya kumlilia marehemu hufutwa.

  CCM bado wameshika dola utasema kirahisi tu kwamba kimekufa!!!!!!!!!!!
   
 3. s

  sangija Senior Member

  #3
  Apr 13, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 4. m

  matawi JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Majister hili bonge la article nimelipesti na kulihifadhi mahali. Weldone jf umeifanya week end yangu kuwa nzuri saana
   
 5. d

  davidie JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu jk anavichembe chembe vya upinzani na ameingia kwa gia kuwa yeye ni m ccm lakini ukiangalia kwa undani utagundua kuwa anaisambaratisha ccm kiujanja ujanja, hivi mnamkumbuka MICHAEL GOLBACHEV WA RUSSIA BY THAT TIME? ALIFANYA HIVI HIVI KAMA JK NA MWISHO DOLA KUBWA ILISAMBARATIKA.
   
 6. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Hakuna chama mbadala wa CCM: Dr. Benson Bana
   
 7. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Huu wimbo wa kifo cha CCM ni moja kati ya mbinu za kukiimarisha chama hicho. Kuna usemi adui muombee njaa ila akijua unamuombea njaa anatumia kila njia kujiimarisha kwenye suala la chakula.

  Sidhani kama CCM inakufa na nisingependa CCM ife kwani role ya CCM ni ileile ambayo leo hii ni role ya CDM. Mimi binafsi siiombei CCM kifo ila ninaiombea ipoteze dola na hilo ndilo lengo hasa la kuwa na vyama vingi. Kuufanya uongozi wa nchi kuwa ni dhamana ya wananchi na si mali ya chama fulani.

  Ninaamini CCM bora na imara yenye watu wenye nzuri na nchi ni jambo jema kwa Tanzania. Ila kuipata CCM ya aina hiyo ni sharti CCM itolewe madaraka kwa muda na kupukutisha kupe wote walijipachika katika chama hicho kwa lengo la kuinyonya nchi. I wish Tanzania tungekuwa na vyama vikuu viwili yaani CCM na kingine kama CDM vikiwa na ushawishi unaowiana katika jamii na kuwa na viti vya wabunge vinavyokaribiana ili kuleta national concesus kwenye mambo muhimu badala ya party monopoly.

  Nafikiri tusiiombee kifo CCM tuiombee ikubali kushindwa katika chaguzi na kukubali Tanzania kuwa na fair and free elections, kwanza kukiwa na fair and free elections itakuwa pia ni heathy issue kwa uhai wa CCM kwani mtindo wa kutoa rushwa ndani ya chama kugombea uteuzi haitakuwa guarantee ya kuingia Ikulu, na hivyo itasababisha watu waache kuchukua risks za kuhonga wajumbe wakati uongozi unatoka kwa wananchi.
   
 8. RUV ACTVIST.

  RUV ACTVIST. JF-Expert Member

  #8
  Apr 13, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 471
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Naunga mkono hoja.
   
 9. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Deni la Taifa limeongezeka kwa 38% kutoka mwaka wa fedha 2009/10 Trillion10.5 mpaka 2010/11 Trillion14.5.

  Source: CAG report
   
 10. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe bado una-quote hii mtu!!
   
 11. a

  alph Member

  #11
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  CCM haifai lakini bado hakuna upinzani hovyo kabisa. tuwaombee wote waimarike ili tupate viongozi 2015.
   
 12. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wala hata haiko hivyo!, Wahenga walisema, Sikio la kufa halisikii dawa; Sema chochote cha kuiamsha CCM usingizini, lakini kamwe haiwezi kuamka, tayari imejitwisha jeneza lake ikielekea kaburini!
   
Loading...