- Mfumo wa serikali ya CCM ambao unawakilisha na kulinda maslahi ya matajiri na wafanyabiashara wachache (Rostam, Lowasa, Manji, Baricks, Ortello Business Corporation, Vodacom na wengineo). Hili hawawezi kujitenga nalo na ndio msingi mkubwa wa kifo cha CCM: mfano mzuri kitendo cha kumtetea Chenge kupitia taasisi yake TAKUKURU ili hali bado ana kesi ya kujibu.
- Wanachama wafu katika ngazi za chini ambao shughuli kubwa wanazofanya ni kuhudhuria mikutano na kupewa nafasi katika kamati mbalimbali za chama na serikali bila ya kujua kinachoendelea katika kundi la wachache wanaotoa maamuzi mazito.
- CCM kuwa na wanachama wenye mtazamo tofauti na waasisi wa chama hususani katika ushawishi wa kuongeza ushiriki wa wanachama katika maswala muhimu ya kichama na kitaifa; mfano Mwakyembe, Sendeka, Shibuda, Seleli, Lembeli na wengineo wanaokubalika ndani na nje ya chama huku wakinyimwa nafasi ya kurekebisha chama. CHAMA KUKATAA MABADILIKO!
- Chama Cha Mapinduzi kinanuka Rushwa (EPA, MEREMETA, UCHAKUZI 2010, RICHMOND, MIKATABA YA MADINI) matumizi mabaya ya nguvu za dola(USALAMA WA TAIFA, POLISI, JESHI) ambayo yote yanahusishwa na ofisi ya raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Raisi hajaweza kukanusha tuhuma hizo na kuwaridhisha watanzania.
- Kujitenge kwa utawala wa CCM na wananchi wa kawaida na wengi walio maskini, huku wakikazana kugombania madaraka na nguvu za kuliongoza taifa bila ridhaa ya wananchi-UDIKTETA
- Kuongezeka kwa uelewa wa watanzania kuhusiana na matatizo yanayowakabili kuliko CCM inavyoyaelewa matatizo hayo na kukifanya chama hicho kupata wakati mgumu wa kuwangoza wananchi hao.
- CCM kutoa ahadi nyingi za kutatua matatizo ya wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi huku wakishindwa kuyatimiza mara wanapoingia madarakani-WANANCHI WANAWANGOJEA KATIKA CHAGUZI ZIJAZO NA KUWAADHIBU.
- Kuongezeka kwa vyama vya hiari nchini vyenye msimamo mkali katika kusimamia haki za binadamu na kuikosoa serikali hadharani.
- Umaskini wa watanzania unaohitaji mfumo mpya wa kisiasa kuyashughulikia. Sina haja ya kusema CHADEMA wamechukua nafasi hiyo walioshindwa CCM.
- La mwisho ni Uchemfu wa chama katika mapendekezo yao ya spika wa bunge la 10. HILI limekula kwao kwa misingi ya kwamba BUNGE HILI si la kuwaweka watu wasiokuwa na uwezo wa kuchambua na kusimamia issues.