Kifo cha Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Daudi Balali kinaonekana kugeuzwa kuwa mtaji wa kisiasa miongoni mwa vyama vya siasa nchini.
Kwa mfano, vyama vilevile na wanasiasa walewale waliokuwa wakimuita marehemu Balali kuwa ni mwizi na fisadi anayepaswa kushtakiwa mahakamani kutokana na kashfa ya shilingi bilioni 133 zilizochotwa kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya BoT ndiyo walewale ambao leo wanakuja na kauli tofauti.
Wanasema eti Balali amefanywa kuwa kondoo wa kafara, kwamba kamwe hahusiki kwa namna yoyote ile na kuchotwa kwa mabilioni hayo ya fedha kutoka EPA, badala yake mhusika mkuu ni Serikali ya CCM.
Kinachotisha zaidi ni hatua ya baadhi ya vyama kufikia hatua ya kudai eti kuwa Balali hajakufa bali yuko hai, badala yake serikali imeamua kumficha sehemu isiyojulikana ili asirudi Tanzania kuja kutoa ushahidi wa jinsi fedha hizo zilivyotumiwa kifisadi na viongozi serikalini kwa ajili ya maslahi ya kisiasa ya Chama Cha Mapinduzi.
Wendawazimu huu mkubwa kabisa katika kilele cha vyama na wanasiasa wetu kuchanganyiwa si tu kwamba kinathibitisha jinsi nchi yetu ilivyo nyuma kabisa kisiasa, lakini pia kimetuonyesha idadi halisi ya wanasiasa wendawazimu tulionao nchini na vyama vyao.
Hao ndio mabingwa wa kusema hawatalala mpaka kieleweke wakati wa kampeni za urais huku wengine wakitaka tuwe na vyama vidogo vya kisayansi kama ilivyo NCCR Mageuzi!