Kifo cha Baby Lawyer wa UDSM mwaka 2011

Umenikumbusha mbali sana aisee, nimekaa na huyo jamaa block c mwaka 2010, alikuwa analewa sana sana na akilewa anaingia room yoyote anaomba kulala
Kuna mwenzake mmoja tulikuwa tunamuita doctor jina lake halisi ni elvis chembangula.
R.I.P Baby lawyer, ila kiukweli alikuwa ni mlevi kupita kiasi yaani kupita kiasi alafu alikuwa hali kabisa
 
Kwani wagonjwa wa kifafa wanaamua wenyewe sehemu za kuangukia au inatokea tu ghafla
Hakuna kifo kilichoniuma kama kile cha rafiki yangu.
Ilikuwa hivi:
Siku ya harusi yake alikuwa amekaa pale mbele na mumewe wanasherehekea ndoa yao.
Ghafla bibi harusi akabanwa na haja, akatoka na matron kwenda kukojoa.
Kufika msalani, bibi harusi akamwambia matron amsubiri nje.
Bibi harusi kuingia msalani, ndo ikawa nitolee...hakutoka mpaka matron alipousukuma mlango na kumkuta akiwa ameanguka chini na amefariki.

Tukaja kutangaziwa ukumbuni, harusi imekufa...haipo tena.
Maiti ikapitishwa, ikatolewa nje.
Baadae nikaja sikia bibi harusi alikuwa na kifafa.
Sasa nahisi kuepuka aibu ya kuanguka ukumbini mbele za watu, akaona heri akaangukie chooni.
Kumbe ndio anaenda moja kwa moja

Kifo ni popote aisee.
 
Kwa mliopitaga Udsm miaka ya 2005/2006 hadi around 2010/2011 na ambao mlikuwa MNA hang out na kundi la walevi wa ud kama kina Sajo wa daz nundaz, yule mzungu wa kuitwa Afande Jesus et al, mtakuwa mnamkumbuka jamaa wa kuitwa Baby Lawyer.

Sikuwahi kumjua jina lake halisi na nadhani alipewa jina Baby Lawyer kwa sababu alikuwa Law student pekee aliekuwa ana hang out na kampani hiyo.

Jamaa alikuwa MTU wa Mbeya na alijulikana sana kwa uwezo wake mkubwa wa kuchomoa vimeo.
Inasemekana kila mwka alikuwa anapata vimeo na vyote alikuwa anavichomoa.
Alihitimu Llb somewhere in 2010 kama sikosei and after that akaendelea na law school wakati huo wanasomea majengo ya udsm.

Wakati anasoma Law School alikuwa anaishi Mabibo Hostel kuna mlevi mwenzake ambae bado alikuwa undergraduate alikuwa amembeba pale.

Matokea yalivyotoka inasemekana jamaa alikuwa ama amefaulu first sitting au amepata vimeo vichache

Kwa sababu ya furaha ya kufaulu vizuri @ law school Baby Lawyer alienda kupiga mtungi.

Wakati anarudi hostel aligongwa na gari mitaa ya Mabibo Hostel na kupoteza maisha yake papo hapo.

Na huo ndio ukawa mwisho wa Babylawyer
Kwa hiyo!!
 
Kwani wagonjwa wa kifafa wanaamua wenyewe sehemu za kuangukia au inatokea tu ghafla
Kuna wengine wana tarehe zao kila mwezi zitatofautiana siku 2 au 3 tu,yaan kama inatokea tarehe 26 basikuanzia tarehe 23 anakua standby mpaka itokee!!na kuna dalili zinajionyesha kabla,mfano kuwa na maluelue,kukosa usingizi,Deja Vu,hata uchizi muda mwingine
 
Ahsante Sana.
 
Rakini kuna jirani yangu kijana wake alikuwa na kifafa alimtibia akapona kabisa inakuaje wengine hawaponi au kuna kifafa cha aina nyingi.
 
Siamini hii
Hakuna kifo kilichoniuma kama kile cha rafiki yangu.
Ilikuwa hivi:
Siku ya harusi yake alikuwa amekaa pale mbele na mumewe wanasherehekea ndoa yao.
Ghafla bibi harusi akabanwa na haja, akatoka na matron kwenda kukojoa.
Kufika msalani, bibi harusi akamwambia matron amsubiri nje.
Bibi harusi kuingia msalani, ndo ikawa nitolee...hakutoka mpaka matron alipousukuma mlango na kumkuta akiwa ameanguka chini na amefariki.

Tukaja kutangaziwa ukumbuni, harusi imekufa...haipo tena.
Maiti ikapitishwa, ikatolewa nje.
Baadae nikaja sikia bibi harusi alikuwa na kifafa.
Sasa nahisi kuepuka aibu ya kuanguka ukumbini mbele za watu, akaona heri akaangukie chooni.
Kumbe ndio anaenda moja kwa moja

Kifo ni popote aisee.
Story
 
Rakini kuna jirani yangu kijana wake alikuwa na kifafa alimtibia akapona kabisa inakuaje wengine hawaponi au kuna kifafa cha aina nyingi.
Ndio kinapona hasa ukiwahi mapema ila wataalam wanasema at least ifike miaka 3 bila kutokea ndio unasema umepona,Kuna vifafa vingine vinasababishwa na stress,homa,mwanga nk so ukitibu chanzo unapona BTW Kuna mtu wa karibu alikua na dalili za kupata kifafa so nilielimishwa kidogo wakija wataalam wanaweza wakaongeza nyama
 
Ahsante nimekuelewa mkuu
 
Amina.
Mungu atunusuru tu kwa kweli.
Ila nadhani ukweli pia unahitajika kati ya mke na mume.
Mimi nina imani mwanamke angemueleza ukweli mwanaume tatizo lake la kuanguka kifafa,huenda wangesogeza mbele au kurudisha nyuma tarehe ya harusi na huenda kifo kisingetokea kwa mwanamke.
Kama ilikua itokee ingetokea tu.

Kifafa hakina tarehe maalum za kutokea kwake sema tu kwa mgonjwa anayejijua vyema huwa kuna dalili kadhaa zinatangulia.
 
Kwani wagonjwa wa kifafa wanaamua wenyewe sehemu za kuangukia au inatokea tu ghafla
Kiukweli sina utaalamu huo.
Ila mara nyingi ninachojua ni kwamba huwa tarehe zao za kuanguka baadhi huwa wanazijua ndio maana baadhi ya wazazi/walezi hupendelea kuwa na watoto wao kimakini kuanzia wanapolala mpaka wachezapo siku za kuanguka kifafa za watoto wao.

Ila sijajua
Lakini baadhi yao huanguka popote pale...nilishashuhudia
 
Kama ilikua itokee ingetokea tu.

Kifafa hakina tarehe maalum za kutokea kwake sema tu kwa mgonjwa anayejijua vyema huwa kuna dalili kadhaa zinatangulia.
Na ndio maana kama ulinisoma tangia awali nilisema kuwa aidha alifanya siri ya kuaibika kudondoka mbele za watu ndio maana akaenda msalani.
Na mama yake mzazi alisema tangu asubuhi siku ya harusi yake, mwanae hakuwa na raha, mama alijua kwanini ila mtoto kwa kuepuka kufedheheka ndio maana alikimbilia msalani.
Alijua kinachotaka tokea
 
Back
Top Bottom