Kifo cha baba wa kiroho huwaacha waumini wengi njia panda

Baraka21

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
1,265
3,177
Kumekuwa na hii tabia hasa kwenye makanisa ya kilokole kumuita Mchungaji wako kuwa ni baba yako wa kiroho.

Huyu ni mtu ambaye hutakiwi kufanya jambo lolote bila kumshirikisha. Ukitaka kuoa au kuolewa lazima ukamuulize kwanza, umepata kiwanja lazima umuulize kuwa ununue au usinunue, unataka kuanza ujenzi lazima umwambie, mkeo hataki kutoa unyumba lazima umshirikishe.

Mwisho lazima ajue kipato chako chote na mapato na matumizi ikiwemo michango ya kanisani.

Kuna watu TB Joshua alikuwa ndio baba yao wa kiroho yaani tumaini lao lote lilikuwa kwa TB JOSHUA. Kila mwaka ilikuwa lazima waende SCOAN mara moja au mara mbili kwa baba yao. Leo hii baba yao wa kiroho amekufa hawana tena direction/muelekeo wa maisha ya kiroho. Wao walimuamini mwanadamu sio Mungu.

Wapendwa naomba tuweke tumaini letu kwa Mungu sio wanadamu. Mungu hafi, halali wala hasinzii.

AMELAANIWA YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU.
 
Hapo kwamba huwezi kufanya kitu chochote bila baba wa Kiroho kulifanya niachane na aliye kuwa mke wangu.

Yaaani mpaka ratiba ya kurudi nyumbani au aende mkesha alikua anapanga baba wa kiroho... sikutaka ugomvi kabisa nikabeba begi nikandoka mpaka leo hajaolewa tena.
 
Kumekuwa na hii tabia hasa kwenye makanisa ya kilokole kumuita Mchungaji wako kuwa ni baba yako wa kiroho...
Upuuzi wa walokole,pentekostal churches,hao wachungaji huwashikilia watu ili waendelee kuwanyonya.

Haya majitu huwa hawajiulizi mtu kama bakhresa,Mengi,Dangote baba wao wa kiroho ni kina nani?

Ukikutana na waumini wa mwamposa hapo Kawe,wanasikitisha sana,wanatembea kwa miguu,wamebeba watoto,hapo wanakuwa wanatafuta usafiri wa kwenda Mbagara,bunju,tabata,
Unajiuliza hivi aliyewaaminisha kwmaba wakipiga hizi makitaimu watafanikiwa kwa kipato ni nani?
 
Kumekuwa na hii tabia hasa kwenye makanisa ya kilokole kumuita Mchungaji wako kuwa ni baba yako wa kiroho...

Yer 17:5 SUV​

BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA.
 
Hapo kwamba huwezi kufanya kitu chochote bila baba wa Kiroho kulifanya niachane na aliye kuwa mke wangu. Yaaani mpaka ratiba ya kurudi nyumbani au aende mkesha alikua anapanga baba wa kiroho... sikutaka ugomvi kabisa nikabeba begi nikandoka mpaka leo hajaolewa tena.
Mke au demu wako?? unabeba begi kirahisi hivyo kwa mkeo?? thubutuuu!!!!
 
Hapo kwamba huwezi kufanya kitu chochote bila baba wa Kiroho kulifanya niachane na aliye kuwa mke wangu. Yaaani mpaka ratiba ya kurudi nyumbani au aende mkesha alikua anapanga baba wa kiroho... sikutaka ugomvi kabisa nikabeba begi nikandoka mpaka leo hajaolewa tena.
Dah mkuu pole sana.
 
Upuuzi wa walokole,pentekostal churches,hao wachungaji huwashikilia watu ili waendelee kuwanyonya,
Haya majitu huwa hawajiulizi mtu kama bakhresa,Mengi,Dangote baba wao wa kiroho ni kina nani?Ukikutana na waumini wa mwamposa hapo Kawe,wanasikitisha sana,wanatembea kwa miguu,wamebeba watoto,hapo wanakuwa wanatafuta usafiri wa kwenda Mbagara,bunju,tabata,
Unajiuliza hivi aliyewaaminisha kwmaba wakipiga hizi makitaimu watafanikiwa kwa kipato ni nani?
Ha ha ha wanafata mafuta na maji
 
Wengi hufuata uponyaji tu hapo
 
Miafiliki ni mituumua ya diinii

Utakuta mtu anahubiliwa achukukie dhehebu au dini fulani.

Mafundisho yao sio kuhubiri habari za msalaba wao ni mafanikio na miujiza.

Hawaifundishi kweli na watu waijue kweli wanafundisha waaminiwe na kuabudiwa.
 
Back
Top Bottom