leipzig
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 2,766
- 1,707
Hivi karibuni nilisikia abiria aliyefia ndani ya basi baada ya kujigonga juu kwenye basi akiwa katika kiti cha nyuma kabisa.
Ajali hiyo ilitokea njia ya Arusha na kumsababishia kuvunjika shingo yake.
Wachunguzi binafsi walisema kwa kawaida abiria hutakiwa kuvaa mikanda wawapo safarini lakini marehemu hakuvaa mkanda na hivyo kurushwa juu na kujigonga katika basi hilo.
Wachunguzi hao wakaendelea kwa kusema dereva aliyekuwa katika mwendo kasi alilipanda tuta la barabarani bila kujua au kuliona na hivyo kusababisha abiria kumlalamikia.
Taarifa zinasema mapendekezo yametolewa kwa wenye mabasi kuwakumbusha abiria wao mara kwa mara kufunga mikanda kama ilivyo katika usafiri wa ndege.
Pia imependekezwa wenye mabasi kuweka aina fulani ya sponji ngumu sehemu ya juu katika basi hasa upande wa nyuma ili kuwaepusha abiria kuumia ikiwa watajisahau kufunga mikanda.