Kifimbo Cha Mwalimu Nyerere!!

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,701
Naombeni kufahamishwa kuhusiana na kifimbo kile cha mwalimu Nyerere.

Alikipata wapi, na je habari zilizoenea huku mtaani kuwa eti aliwahi kukisahau hotelini wakati akiwa ziarani ulaya, lakini wahudumu wa hoteli walishindwa kukitoa juu ya meza ni za kweli?

Kipo wapi kwa sasa? Makumbusho au alizikwa nacho?
 
Maana ya kushika fimbo ni kuwa wewe ni kiongozi na hata polisi wakisha pata cheo kuwa na v tatu wanabeba fimbo.

Na kumbuka alikuwa mwalimu, na mwalimu na fimbo unajua ina maana gani.
 
Naombeni kufahamishwa kuhusiana na kifimbo kile cha mwalimu Nyerere. Alikipata wapi, na je habari zilizoenea huku mtaani kuwa eti aliwahi kukisahau hotelini wakati akiwa ziarani ulaya, lakini wahudumu wa hoteli walishindwa kukitoa juu ya meza ni za kweli?
Kipo wapi kwa sasa?? Makumbusho au alizikwa nacho??

Kama unayo yasema ni kweli basi alikuwa mchawi au anatumia majini.
 
hata mm nlisika alikipata kwa mganga maarufu akiwa na kenyatta enzi hizo, nakumbuka walisema mama yake ndie ngao yake na mlinzi wake mkuu wakasema.

Mama yake akifa hataishi miaka miwili wkt huo nikiwa mkwawa high school
sikuamini hayo ila alipofariki ndani ya miaka 2 tangu afe mama yeke nkaanza kupata mashaka na yaliyosemwa juu yake

kile kifimbo wadau walisema pia haendi nacho kanisani hata kidogo sina uhakika kwa hili.
 
Maana ya kushika fimbo ni kuwa wewe ni kiongozi na hata polisi wakisha pata cheo kuwa na v tatu wanabeba fimbo
Na kumbuka alikuwa mwalimu,na mwalimu na fimbo unajua ina maana gani.

Kumbe kuwa na kifimbo ni heshima?? Alikipata wapi?
 
hata mm nlisika alikipata kwa mganga maarufu akiwa na kenyatta enzi hizo
nakumbuka walisema mama yake ndie ngao yake na mlinzi wake mkuu wakasema
mama yake akifa hataishi miaka miwili wkt huo nikiwa mkwawa high school
sikuamini hayo ila alipofariki ndani ya miaka 2 tangu afe mama yeke nkaanza kupata mashaka na yaliyosemwa juu yake
kile kifimbo wadau walisema pia haendi nacho kanisani hata kidogo sina uhakika kwa hili.
Kuna stori nyingi tu mtaani kuhusu kile kifimbo, na nyingi huwa ni hisia tu za watu....
 
wakati anapigania uhuru alipenda kutembea na bakola.baada ya uhuru akawa anatembea na fimbo ndogo zaidi ya ile ya uhuru kwa urefu.baada ya kustaafu alikua na fimbo nyingine iliyotengenezwa kwa pembe ya ndovu kwa kila ncha lakini katikati mti.

fimbo zote zipo butihama kwenye jumba la makumbusho la nyerere lililojengwa miezi saba kabla ya kifo chake.roger
 
wakati anapigania uhuru alipenda kutembea na bakola.baada ya uhuru akawa anatembea na fimbo ndogo zaidi ya ile ya uhuru kwa urefu.baada ya kustaafu alikua na fimbo nyingine iliyotengenezwa kwa pembe ya ndovu kwa kila ncha lakini katikati mti.fimbo zote zipo butihama kwenye jumba la makumbusho la nyerere lililojengwa miezi saba kabla ya kifo chake.roger
Asante sana, nitaenda kutembelea huko makumbusho Butiama
 
Hawezi kuthibitisha!
Kitavi mpaka miaka ya leo unaamini uchawi?

Kama kuna uchawi mbona Bush na blair wame uwa watu wasio na makosa, hawakuweza kulogwa?

Je mkuu umesha sikia mtu alikuwa anaitwa Abunuasi?
 
Nilipo kua mdogo miaka ya ile ya 90 niliwahi kuyasikia mambo kadhaa kuhusu nyerere na mpaka leo sijajua kama ni kweli au zilikua stori tu.

1.ile fimbo ya nyerere ili kua ni kinga dhidi ya maadui,eti wanadai akienda sehemu km kuna maadui fimbo inakua nzito mkoni kwa jk na hapo mwalimu alikua anajua kua eneo hilo si shwari.

2.kale kafimbo inasemekana kama amekisahau mahali basi hata muwe watu mia hamuwezi kukanyanyua mpaka aje mwenyewe.

3.Ilitokea hafla moja huko nchini zimbabwe nyerere akawa ni miongoni mwa waalikwa pia na wasanii kibao akiwemo bob marley,basi katika harakati za kupeana mikono eti jk haku mpa mkono bob kisa ni mvuta bangi mhuni na mchafu kutokana na zile rasta zake,bob akapata nafasi ya kutumbuiza basi mzee mzima akatupia kitu cha "africa unite" kibao kika mkuna sana julius na mwwnyewe aka inuka kwenda kumpa mkono Robert Nesta Marley.

4.Kutokana na kiburi na jeuri ya mzee wetu kamabtage naskia pia aligoma kushikana mkono na malkia wa uingereza eti kwa sababu malkia alikua amevaa gloves ndipo kambarage badala ya kumshika mkono kavu kavu akatumia kifimbo kusalimiana na mama wa uingereza.

SASA SIJUI NI KWELI HAYA MAMBO AU NI STORI TU? WAKUBWA WA ENZI HIZO HEBU NIJUZENI...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom