Kifanyika kitu hapa

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,201
233
Fani yetu ya ICT haswa katika upande wa Ufundi ambayo mimi nipo imekuwa ya ubabaishaji sana , kadri ya siku zinavyozidi kwenda mambo yale ambayo tunayekemea na kuyanyooshea kidole ndio yale yale watu wanaendelea kufanya au kutekeleza , imekuwa bahati mbaya sana kwa Tanzania hakuna taasiri au shirika ambalo linasimamia mikakati ya ICT kama liko mimi silitambui hata sijui hawa watu wako wapi .

Juzi hapa nilikuwa katika kazi sehemu moja ya serikali , walinunua komputa kama 20 hivi kati ya hizo 5 zikawa haziwaki , mmoja wa wafanyakazi pale akanipigia simu msaada wangu unahitajika kwa sababu alinisoma katika mtandao , nilijadiliana nae katika simu kabla ya kwenda kule lakini mwisho nilimwambia awasiliane na mtu ambaye kawauzia kwa sababu zina warranty .

Huyu mtu akanipigia simu tena kuniomba niende , nikafika pale kwanza nikamwomba niongee na jamaa yao wa ICT yule Administrator , ujue shirika hili liliajiri watu karibu 5 mwezi uliopita ( kutokana na matangazo yao katika notice board ) kwanza wakaniambia hayupo nilipodadisi nikaambiwa ni Fulani nikaonana nae , yule kijana akaniambia yeye hawezi kutoa maamuzi yoyote hana uwezo huo .

Nikaachana na yule kijana sasa kurudi katika kazi yangu nikaangalia nikawaambia kwamba hiyo computer ina RAM mbovu kwahiyo ni kubadili RAM ndio mambo mengine yaendelee nikawaelekeza pa kwenda kununua RAM , kumbe huyu jamaa aliyeniita nae ana kampuni yake , anataka kazi hiyo aipe kampuni yake kwa kivuli changu sikujali nilimwambia cha kufanya kisha nikaondoka kuendelea na shuguli zingine .

Baadaye niligundua kwamba aliyenunua komputa zile ni mhasibu na hakununua kutumia kampuni inyojulikana , tenda hiyo alimpa ndugu yake ndio maana mhasibu linapotokea kitu kama hichi hawezi kufanya chochote anaongea na ndugu yake mwingine kama huyo aliyenipigia mimi bila kwenda kwa jamaa yao wa ICT na mambo yanaenda kama walivyopanga wao

Hebu angalia hii orodha


This is to accept that we have received the information and communication equipment with particulars and quantities listed hereunder, in good working order and conditions.


S/No. ITEM DESCRIPTION QUANTITY TOTAL PRICE USD
1 Server 1 12,752.64
2 Desk Top Computers 34 41,016.24
3 Lap Tops (Note Books) 5 7,695.00
4 Printers (Coloured) 1 3,744.36
5 Printers (Black and White) 24 30,792.96
6 Printers-Plotters (Various Colours) 1 2,608.20
7 UPS (Server) 1 469.80
8 UPS (Desk Top) 34 8,262.00
9 Printer Catridge 10 702.00


Please note that this letter does not relieve you from the other obligations which are set out in the above mentioned contract agreement

Hii ndio Tanzania yetu , ndio maana nasema tunatakiwa tuwe na taasisi maalumu ya kusimamia mambo haya , lazima tuwe na starndard zetu na mambo mengine kwa ajili ya nchi yetu

YAKAIZARI TUMWACHIE KAIZARI

MAISHA MEMA
 
Back
Top Bottom