Kifahamu kisiwa cha Christmas

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
KIFAHAMU KISIWA CHA CHRISTMAS.
FB_IMG_16404982250483409.jpg

Kisiwa cha Krismasi ni eneo dogo la Australia katika Bahari Hindi takriban 500 km upande wa kusini ya Jakarta mji mkuu wa Indonesia na 2,400 km kaskazini ya Australia yenyewe.

Kuna wakazi 1,600 wanokalia vijiji katika kaskazini ya kisiwa. Theluthi mbili za eneo lake ni hifadhi la taifa kwa sababu ya mazingira yake ya pekee pamoja na mimea na wanyama wake wasiopatikana mahali pengine duniani.

Jina na Historia

Jina lake liliteuliwa kwa sababu nahodha Mwingereza William Mynors aliyekuwa kati ya watu wa kwanza wa kuona kisiwa hiki alifika hapa siku ya Krismasi mwaka 1643. Wakati ule kisiwa kilikuwa bila watu.

Katika karne zilizofuata kisiwa kilitembelewa mara chache kwa sababu mwambao wake ni vigumu kukaribia kwa jahazi kubwa. Lakini baada ya kugunduliwa fosfeti kisiwani migodi ikaanzishwa na wafanyakazi kupelekwa hapa kutoka Singapur, China na Malaysia.

Hawa walikuwa mababu wa wenyeji wa leo. 1958 kisiwa kikakabidhiwa kwa Australia.

NB: Kaa(🦀) mwekundu ni mnyama wa pekee kisiwani

Mazingira

Kiswiwa cha Krismasi ni mahali pa pekee kwa sababu kinaonekana hakikutembelewa na watu hadi karne ya 16 na hakukukaliwa na watu hadi mwishow a karne ya 19. Hivyo spichi nyingine zimehifadhiwa zilizoharibiwa penginepo.

Cc: Fahamu Leo
 
Back
Top Bottom