Kifahamu Kifo cha Utata na Kusisimua cha Mwanaume wa Somerton: The Somerton Man (TSM)

4G LTE

JF-Expert Member
Aug 4, 2015
6,777
10,533
Huu ni mkasa wa kipekee wa kifo cha mwanaume mmoja amabye hajawahi kufahamika kwa takribani miaka 70 sasa, kesi hii ilisumbua vichwa vya mamlaka kwa jinsi ilivyokuwa tata na kadiri walivyosonga mbele mambo yalizidi kuwa magumu kwako. Kisa hiki kilitokea jiji la Adelaide katika mtaa wa Somerton Kusini mwa Australia. Kesi hii ilivuta hisia za watu wegi kutokana na upekee wake mamlaka za upeleleze nchini humo ziliamua kushirikiana na magwiji wa upelelezi na ujasusi kama Scotland Yard na FBI na walitoa ushirikiano wa kutosha, pamoja na hayo yote bado hawakuweza kung’amua chochote kwenye kesi hii na kugeuka kuwa ndoto ya mchana.

IMG_20190731_020056.jpg


Ilikuwa jioni tulivu na ya joto katika jiji la Adelaide haswa katika ufukwe wa Somerton, na ikumbukwe kuwa kilikuwa kipindi cha joto kwasababu ni mwisho wa mwaka. Mnamo saa 1:00 usiku siku ya Jumanne Novemba 30, 1948….kikiwa ndio kipindi cha vuguvugu la vita baridi, huku kukiwa ndio kwanza vita ya pili ya dunia imemalizika, wapendano wawili Sonara John Bain Lyons na mkewe walikuwa wakitembea pembezoni mwa fukwe ya Somerton, maili chache kutokea Adelaide. Kadri walivyokuwa wakisogea kuelekea Glenelg, waliona mtu ambaye amevalia nadhifu, huku kalala mchangani kama umbali wa yard 20 kutoka walipokuwepo, miguu ikiwa imeachana huku kwenye sehemu za kukanyagia zikiwa zimetengeneza alama ya X.

IMG_20190730_203703.jpg



Walipoendelea kutazama mtu huyo alinyoosha mkono wa kulia juu, kisha akauachia na kuanguka mchangani. Lyon’s akahisi labda atakuwa emejilewea huku akijaribu kuvuta sigara. Kama ilivyo ada kipindi cha mwisho wa mwaka watu wengi wanakuwa kwenye mapumziko mbalimbali na starehe kadha wa kadha huchukua nafasi na ndio maana wawili hao walihisi jamaa alipiga gambe la kutosha na kuamua kujipumzisha pale ufukweni.

Nusu saa baadaye, couple nyingine waligundua mwili huo ukiwa umejilaza pembezoni mwa fukwe hiyo. Walipomwangalia kutokea juu, mwanamke aligundua amevalia suti nadhifu, na viatu va maana vipya vikiwa na mng’aro wa maana. Wakashangaa huyo mtu anafanya nini hapo na mavazi ambayo si ya sehemu hiyo kwani yamekaa kiofisi zaidi tena msimu wa joto ambao ni ngumu mtu kuvaa nguo nyingi. Akiwa hajigusi huku mkono wake mmoja ukiwa chini, couple hiyo ilihisi labda kajilalia tu, huku uso wake ukiwa umezingirwa na mbu. Mwanaume akatania kwa kusema “atakuwa amejifia huku dunia haitambui”.

Ni mpaka ilipotimu asubuhi kesho yake huku Lyon’s akitokea kuogelea alipokuta kundi la watu likiwa limezunguka eneo lile waliloona mtu jana yake usiku. Akajongea tena karibu na kukuta mtu yuleyule amelala upande uleule na miguu imeweka alama ya X. Mwili wake ulikuwa umeshaanza kutoa harufu, huku kukiwa hakuna dalili za fujo zozote zilizotokea eneo hilo na akiwa na kipande cha sigara kikiwa kimeangukia kola ya shati lake, kikionekana kuwa kimetokea kwenye mdomo wake.

Ikabidi waite polisi, ma ndipo uchunguzi wa awali ulipoanza kwa kuuliza watu waliokutwa eneo la tukio na baada ya saa tatu wakabeba mwili na kuondoka nao. Hao polisi waliokuwepo eneo la tukio walikuwa polisi wa kawaida, sasa ikabidi wenye taaluma yao washirikishwe ambao ni wapelelezi na mwili ule ukapelekwa hospitali ya Royal Adelaide na kukabidhiwa kwa madaktari bingwa Dr. John Barkley Bennet na John Dwyer wakaanza mara moja uchunguzi ukiendelea mwanaume huyo alikuwa amevuliwa nguo zote. Wapelelezi wakaomba vitu vyote alivyopatikana navyo wapewe kwani vitawasaidia huko mbeleni kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Dr. Bennet aliweka muda wa kifo kuwa si zaidi ya 8:00 usiku, na kuendelea huenda kifo chake ni moyo kufeli au sumu. Vitu alivyoukutwa navyo mfukoni ni kama ticket nusu ya treni ya kwenda Adelaide, kitambaa kidogo cha mkononi, kipakti cha chewing gum, kiberiti, chanuo mbili, pakiti ya sigara aina ya Army ikiwa na sigara saba tofauti ndani. Hakuwa na pochi wa kitambulisho chochote kile wala fedha taslimu. Hakuna nguo hata moja iliyokuwa na lebo ya utambuzi na zikiwa zimeondolewa kitaalamu kabisa. Hili likazidi kuwapa baridi wapelelezi kwanini lebo zimeondolewa? Wakakuta mfuko mmoja wa suruali umerepewa na uzi usio wa kawaida wa rangi ya machungwa na cha mwisho alichokutwa nacho ni kipande cha ujumbe unaosomeka “Tamam Shud”, ambacho kilipatikana kimeshonewa kwa siri sana kiunoni kwenye suruali yake. Lugha hiyo ya huo ujumbe ni asili ya Kiajemi (Persian) na unapatikana kwenye ushairi wa zamani wa jamii hiyo ya Kiajemi. Waajemi leo hii wanapatikana taifa la Iran na karibu nusu ya raia wake ni Waajemi. Sasa wapelelezi wakiongozwa na Thomas Cleland walishtushwa na ujumbe na ujumbe huo kati ya vitu walivyovikuta katika nguo za mwanaume huyo, ingawa kwa hapo hawakujua maana yake.

Lakini wao kama wapelelezi walishajua kwenye ujumbe huo lazima kuna kitu kimejufucha (coded message), hivyo wakaanza mara moja kufuatilia ujumbe huo, na ripota wapolisi Frank Kennedy Adelaide Advertiser aligundua maneno hayo ni ya asili ya Kiajemi na kuwataarifu wapelelezi kuwa kuna kitabu cha ushairi –“The Rubaiyat of Omar Khayyam’’ na kuelezea kuwa ushairi huo ni wa karne ya 12, na umekuwa maarufu nchini Australia kipindi cha vita na kikitafsiriwa na Edward FitzGerald. Shairi hilo lilikuwepo kwenye matoleo anuwai, lakini maswali kutoka kwa wapelelezi kwenye maktaba mballimbali, wachapishaji na maduka ya vitabu vilishindwa kupata nakala inayofanana na mwandiko huo. Angalau iliwezekana kusema maneno hayo “Tamam shud” (au “Taman shud”, kama baadhi ya magezeti yalivyochapisha kimakosa tokea enzi hizo) yalitokana na tafakari za kimapenzi za Khayyam juu ya maisha, vifo na mapenzi. Na kweli yalikuwa maneno ya mwisho kwenye tafsiri nyingi za kingereza-haishangazi, kwa sababu kifungu hicho kinamaanisha “mwisho”.

IMG_20190730_203152.jpg



Hapa wapelelezi wakavuta pumzi kwanza, maana sasa mikanganyiko ndio kwanza inaanza. Maana ukilichukulia juu juu tukio hilo na ujumbe huo moja kwa moja inaonekana ni tukio la kujiua; kwa ukweli wake, polisi wa Kusini mwa Australia hawakugeuza maswali yao ya “mtu aliyepotea” kuwa uchunguzi kamili wa mauaji.

Wakiwa wanaendelea kujiuliza, wakarudisha taswira yao kwa huyo mwanaume na kuhisi ni raia wa Marekani kwa jinsi mavazi yake yalivyokuwa na rangi ya mwili wake. Lakini wakashangazwa na kutokuwa na pochi wala kofia, kwani kwa miaka hiyo ni nadra kwa mtu kukosekana na vitu hivyo hasa kofia kwani ndiyo fashion hasa kwa wageni kutokea Marekani. Madaktari walifanya uchunguzi zaidi wa maabara (autopsy) siku moja baadaye maana mikanganyiko ilizidi kutanda kuhusu mwanaume huyo huku wapelelezi wakiwa wameshapata vidokezo kadhaa kuhusu mwanaume huyo, na ripoti ya post-mortem iliwapa mwanga kidogo, kwani ilieleza kuwa mtu huyo hakufa kwa kisababishi chochote kile cha nje kama kupigwa, hata chakula tumboni mwake kilionekana ni cha muda mfupi kabla ya kifo chake na mfumo wake wa meno ulikuwa wa kipekee kwai ulikuwa haufanani na rekodi ya kiumbe hai chochote duniani, mwisho madaktari wakasema wanaamini kifo chake si cha kawaida kwani vipimo vyote vimeshindwa kutanabaisha kilichosbabisha kifo chake.

Wapelelezi wakazidi kuchanganyikiwa, maana mashuhuda wanasema mwili wa mwanume huyo ulikuepo ufwekeni hapo toka saa moja usiku na alikuwa hai maana aliweza kunyanyua mkono, huku madaktari wakisema chakula alichokula alichokula kilipita masaa manne au matatu kabla ya kifo chake. Wakati ripoti inasema kifo kilitokea si zaidi ya saa nane usiku, maana yake ukirudisha masaa manne nyuma maanake alikula chakula hicho saa nne usiku na wakati watu walimuona mapema zaidi ya muda huo akiwa ameegema ukuta wa fukwe na kuonekana yu hai. Wapelelezi wakazidi kuvurugwa kuwa kipi ni kipi, ikabidi sasa mwili huo uchunguzwe tena upya kitabibu na akapewa hiyo kazi John Barton Cleland ambaye nae alikuja na majibu tofauti na ya awali. Tofauti ilikuwa ni muda aliokufa mwanaume huyo kwani ripoti ilisema hakufa eneo alipokutwa maana yake aliletwa ufukweni hapo akiwa ameshakufa, anaendelea kusema chakula ambacho kilikutwa tumboni mwake ambacho ndich cha mwisho kuliwa na huyo mwanaume ni aina ya chakula ambacho huchelewa kumeng’enywa na ndicho kilichofanya aonekane amekula muda mfupi uliopita na pia hakuishia kukagua mwili wake tu bali hadi mavazi yake na kugundua kitu kwenye viatu vyake.

Kwanza aligundua havikuwa na dalili ya kutembelewa kutoka sehemu moja kwenda nyingine, kwanza vilikuwa na mng’aro kama ndio vimetoka kwa shoe shiner. Pili, havikuwa na harufu ya joto la miguu ili kuonesha vilivaliwa muda mrefu na kubaki na unadhifu wake. Wapelelezi ikabidi wajidhihirishie hili, wakachukua viatu vipya wakavivaa na kuzunguka navyo ufukweni pale na kugundua vimechafuka na harufu ya miguu ilibaki pia, na vile haioneshi ameuawa basi wakatoa dokezo la sumu hatari mbili zinazoweza kuwa zimetumika kukatisha maisha yake nazo ni “digitalis” na “strophanthin” –strophanthin ni glucoside adimu inayopatikana kwenye mbegu flani zinazopatikana barani Afrika. Kihistoria, zilikuwa zinatumika na kabila dogo la Wasomali kuweka sumu kwenye mishale yao.

Sumu hizi zinatabia ya kuyeyuka na kufyonzwa mwilini haraka sana baada ya kutumika, hivyo kufanya uchunguzi wa kitabibu kuwa ngumu kugundulika. Pia ripoti hizi mbili zilitaja mtu huyu anaweza kuwa raia wa Marekani au Uingereza, umri kati ya miaka 40-45, mwenye urefu wa futi 5 na nchi 6, mikono na vidole vyake vilionesha hakuwa mtu wa kufanya kazi ngumu, vidole vya miguuni mwake vilionesha ni mtu wa kuvaa viatu mra nyingi. Wapelelezi walizidi kuvurugwa kwani walijua chunguzi za kitabibu zitawasaidia ila ndio zilizidi kuwakanganya, maana haijulikani alikufaje na wakati gani na kwanini! Maana ripoti ya kwanza ilisema alifia pale ufukweni mida ya saa nane usiku huku ripoti ya pili ikisema alifia eneo jingine na kuletwa pale ufukweni!

Walichofanya wapelelezi ni kusambaza picha zake maeneo mbalimbali nchini humo, maeneo mengine duniani yanayozungumza kiingereza kuona kama kuna anayemfahamu au kuwahi kumuona sehemu yoyote ile, pia wakazi wa Adelaide walipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti kwa matumaini wangeweza kumtambua na kusaidia uchunguzi wa tukio hilo. FBI na Scotland Yard ndio wakaingia kazini na kuanza upelelezi baada ya kuona huyo mtu anaweza kuwa wa taifa lao. Na kwa kuanzia upelelezi walichukua alama za vidole na kufananisha na rekodi walizonazo nchini mwao, siyo Marekani wala Uingereza kulikoweza kuja na majibu ya mfanano wa alama za vidole za mwanaume huyo. Ulipita mwezi ambapo ndipo mwaka mwingine unaingia yaani 1949 huku kukiwa hakuna mwanga wowote kwenye kwani hakuna aliejitokeza na kusema anamfahamu mwanaume huyo si ndugu, rafiki wala jamaa au hata taifa lolote lile kusema ni raia wake.

Ila bado wapelelezi walikuwa kazini wakilala na kuamka na kesi hiyo….

Wakati kesi hii ikizidi kupamba moto na sintofahamu zikiongezeka, akajitokeza jamaa moja kwenye mji wa Adelaide kwa majina John Freeman katika ofisi za wapelelezi wa kesi hiyo, akiwa na kitabu ambacho alikuja kuwakabidhi wapelelezi kwani kinaweza kuwasaidia katika uchunguzi wao. Huyo jamaa aliekuja na kitabu hicho, akawa kama vile alitumwa na shetani, kwani ndio alizidisha ugumu wa kesi hiyo maradufu. Wapelelezi walipokea kwa mikono miwili maana walihitaji sana taarifa kutoka kwa wananchi ili kuweza kumgundua huyo mwanaume. Wapelelezi baada ya kupokea kitabu hicho, wakaanza kukichunguza na kukuta kitabu hicho kina shairi la “The Rubaiyat of Omar Khayyam’’ kwenye kurasa zake za mwisho, wapelelezi wakapitia maneno yote ya kurasa za mwisho wakagundua kuna kipande kidogo kimechanwa.

IMG_20190730_204141.jpg


Ili kukigundua kipande hicho ikabidi wapelelezi walichukue shairi lote la “The Rubaiyat of Omar Khayyam’’. Baada ya kupitia shairi zima wakagundua hicho kipande hicho ni kipi na kuona msaada unaweza kuwepo hapo. Kipande hicho kilikuwa ni kile kipande walichomkuta nacho mwanaume huyo kwenye suruali yake kikiwa na maneno “Tamam shud” na wapelelezi kurudi kwenye kile kipande na kuanza kukipimia kwenye sehemu hiyo iliyochanwa kuona kama kitafiti ili wajihakikishie, kukiweka tu kikafiti na kujua kipande hicho kimetoka kwenye hicho kitabu.


Sasa wapelelezi wote macho na masikio yao wakayageuzia kwa msamaria mwema huyo aliyekileta hicho kitabu ili kuendeleza uchunguzi, msamaria huyo akasema mnamo mwaka 1948 mwezi Desemba siku ambayo mwili wa mwanaume huyo ulikutwa kwenye fukwe ya Somerton, na yeye alikuepo ufukweni hapo na alikuja na shemeji yake wakiwa na gari yao na ni kawaida yao kuja ufukweni hapo. Wakiwa wameliacha mita kadhaa kutoka ufukweni hapo, ndipo wakasikia habari za kuwa kuna mwanaume amekutwa amekufa eneo la ufukwe huo.


Ila kwa wakati huo, mwili wa mwanaume huyo ulikuwa umeshachukuliwa kwa maana hiyo hawakufanikiwa kuiona maiti yake, ila tu wakabaki wanasikiliza gumzo la kifo hicho kwa ukanda wote wa ufukwe huo maana ndiyo ilikuwa habari ya mjini kwa siku hiyo, yeye na shemeji yake wakaendelea na mambo yao yaliyowaleta hapo kisha wakondoka zao. Sasa wakiwa wanarudi kwenye gari lao, baada ya kufungua mlango na kuingia ndani ndipo walipokikuta kitabu hicho chini ya kapeti la gari yao. Kila mmoja akawa anahisi ni kitabu cha mwenzake, msamaria mwema akaamua kukikagua mpaka kurusa zake za mwisho na kukuta kuna kipande kimechanwa na akarudisha kumbukumbu zao na kumbuka zilishawahi kuchapishwa habari zinazohusiana na kifo cha mwanaume ufukweni na kipande kilichopatikana kwenye suaruali yake kikiwa kimeng’olewa mahali na ndipo alipoamua kwenda kukiripoti hicho kitabu kuona kama kinahusiana na kipande hicho………..ITAENDELEA

[Sehemu ya Pili #93; Mwisho #180]
 
List ya tags ni ndefu, utanisamehe kama uliniomba last time na nimekusahau….usisite kunikumbusha next time nikutag
mkuu nafuatilia sana nondo zako coz ni nondo dhahiri zilizopata kutokea na ni za kufikirisha sana na kuacha unsolved questions kama ile ya asha degree. Usiponitag unajua naweza nikaziondoa hizo nyota zako?? Unajuaje kama nikimaliza kutype hapa sitaondoka na hizo nyota zako. 😁
 
mkuu nafuatilia sana nondo zako coz ni nondo dhahiri zilizopata kutokea na ni za kufikirisha sana na kuacha unsolved questions kama ile ya asha degree. Usiponitag unajua naweza nikaziondoa hizo nyota zako?? Unajuaje kama nikimaliza kutype hapa sitaondoka na hizo nyota zako.
Hahahhaha mkuu nikidondosha sehemu ya pili nitakuita... Usiondoke nazo
 
Kazi nzuri sana.
Uandishi mzuri sana, mpangilio mzuri unaoshawishi na kuvutia.
Lugha nzuri sana na inayoeleweka kwa kila mtu.
Unacho kipaji mkuu.
Asante sana kwa kutusogezea vitu kama hivi. Leo nimepata story ya kuwahafithia wale watu.😂😂😂😂😂😂
Usichelewe sasa kuleta mwendelezo maana nitaaibika Mimi.
 
Back
Top Bottom